Nimeamua kubadili dini na kuwa Mwislamu

Nimeamua kubadili dini na kuwa Mwislamu

Status
Not open for further replies.
Never judge a philosophy by its abuse. Tukianza kuzungumzia masuala ya ISIL/ISIS, bokoharam, Al-shabaab kama ndio dhana kuu ya uislam itakua sawa??
Give us another reason, may be you want to do so to secure your job. So far excuses ulizotoa hazina mashiko
Islam has nothing to do with those people, Islam as religion is so pure and so Clean. Islam is perfect but me as Muslim am not perfect.
 
Ni uamuzi wako mkuu.

Mbinguni hakuna Dini. Dini ni miradi ya Duniani tu! Dini ni sawa na mipaka ya nchi hii Kenya, hii Tz, hii Uganda, nk.
Dini ni sawa na njia za kusolve swali.
Hakika Umepata khasara kubwa mno najua kwa sasa huwezi kuelewa.
 
Umesahau tu kuwa ni utawala wa JK umehakikisha Ponda na mashehe wa uamusho wananyea ndoo kwa muda mrefu na ameondoka haijulikani watatoka lini.

Halafu hao uliwataja kuwa ni wakristo, umewapa daraja lisilo wahusu. Ili uamini siyo wakristo, wote uliowataja, wakusanye uwaweke kundi moja, halafu uone kama wataelewana kuhusu Mungu au kuhusu Kristo. Kila mtu anaamini lwake wakati yesu aliacha imani moja tu
Mashekhe wa Uamsho wapo ndani kwa sababu ya walaka toka kwa Mapadri acha kupotosha umma , Mapadri ni watu WABAYA SANA HAPA TZ NYUMA YA PAZIA ikimbukwe wale walikamatwa baada ya issue ya kuchomwa makanisa Zanzibar.
 
Ulianza vzr ila ulipoingiza hao Marais ndipo umekosea nakunukuu " wa Islam ni watu wa haki kuliko sisi wakristu" udhaifu wa hoja wew sio mkristu tena na Je Ni kigezo kipi Umetumia Kusema waislam ni watu wak?Pia kazi ya kohoji na kutoa hukum si ya mwanadamu huna mamlaka ya Kusema fulani yuko safi kwa hujui yako itakuaj mwenye mamlaka hayo ni Mungu tu, Kwa kuangalia watu wachache Ndio unapima, utakosea kama ulivyokosea Kuangalia wakina kagame na wengine, nakukumbusha Umesahau na al-qaeda, vp boko haram na Je kuhusu Al-shabab
 
Usimfananishe mfuasi kwa mfuasi mfananishe mwanzilishi kwa mwanzilishi

Mfananishe Yesu na Muhammad

Kwamba uislamu unakubali Yesu yu hai na atarudi ila Muhammad ni marehemu kama wengine,

kwamba Yesu alikemea pepo wabaya na aliponya magonjwa ila Muhammad hakuwahi kufanya hivyo

kwamba Yesu alihimiza kuwapenda watu wote maadui na marafiki na kuwaombea ila mtume aliongoza vita na kumwaga damu, kupora na kuteka nyara

Kwamba Yesu aliishi maisha ya kujinyima, kuomba, kuwatumikia wengine na kuwafundisha watu ila mtume alifanya mengi kuuridhisha moyo wake ikiwemo kuoa wake wengi huku mwingine akiwa na umri mara mbili ya ule wa mtume

Ila zaidi ni kitabu chake yaani Quran japo yeye mwenyewe hakujua kilichoandikwa humu kutokana na udhaifu wake wa utambuzi ktk lugha ya maandishi kukiri kwamba wale wenye mashaka nacho waende kujifunza zaidi ktk biblia
 
Islam has nothing to do with those people, Islam as religion is so pure and so Clean. Islam is perfect but me as Muslim am not perfect.
Good. If you need to be perfect. Convert into CHRISTIANITY. Islam is for people who are not perfect..kama wanajilipua Iraq, Afghanistan na Somalia.plus Mali plus northern Nigeria. Nchi za kikristu ushasikia mtu kajilipua na kuua wanaeake na watoto ili awahi mabikra Mia ? This means the person who believes in such nonsense is not perfect.
 
Sitaki kuamini hizo ndizo sababu zilizokufanya uhame dini ingawa bado siwezi kuuamini uzi wako kwa asilimia zote....

Ukristu ama uislamu haupimwi kwa vile watu wake huishi bali misingi inayoijenga dini husika....

Unaonekana una upungufu wa kimawazo na kihisia maana una sababu dhaifu sana..kamuone mshauri
 
Hatuokolewi kwa matendo yetu ila tu kwa neema ya Mungu, hatufanywi wenye kustahili mbele za Mungu kwa matendo yetu ila tu kwa neema zake tunaitwa na Mungu ili tufanye matendo mema kama sehemu ya kuuishi upendo wa Mungu.

Mkristo na ukristo vinaweza kuwa ni vitu viwili tofauti kabisa hususani pale mkristo anaposhindwa kuiakisi tabia halisi ya ukristo yaani kristo ndio maana tunaambiwa kielelezo cha ukristo ni kristo mwenyewe wala sio mtu yeyote ama mchungaji, papa, padri ama lusekelo hatupaswi kabisa kujilinganisha na binadamu ila maisha ya Yesu mwenyewe ndio maana imepelekea wewe kuikosesha nafsi yako kwa kuwatazama binadamu

Pia kuhusu uislamu yapo madhaifu mengi ambayo hujayajua ikiwemo Quran kumkiri Yesu kama neno la Mungu na kukiri kuwa Mungu aliumba vyote kwa neno lake, sasa hapo jiongeze

Ila kabla hujaamua kujikita kamili ktk uislamu tenga muda usome biblia walau kwa wiki mbili tu hlf ndio ufanye uamuzi ila nakupendekezea soma vitabu hivi viwili kitabu cha mwanzo na kitabu cha Mathayo visome sura zote hlf utafakari uamuzi wako ukiona bado uislamu ni bora ok chukua hatua
Biblia yenyewe hiyo mmeandika wenyewe binadamu yaani maneno ya watu wachache mkuu soma INJILI YA BARNABA mmoja wa wale wanafunzi 12 wa Yesu. Yeye anasema Yesu alikuwa Mwislamu naye aliswali kwa kurukuu na kusujuduu.
 
Pia nagundua Ulikua na maslai Binafsi ya kwenda huko ulikoenda, na sa iv ajira zinavosumbua ukaona isiwe tabu, lakin Kutokana na Andiko lako nachelea Kusema hukuwa umesimama na Mungu vzr, Ndio maana umeweza kuyumbishwa, na huko usipokua imara hauwez kurudia matapishi mwishowe utaona Hamna umuhimu wa kuwa na dini, sikatai kuhamia dini hiyo, ila njia uliyotumia kuondokea huku sio njia sahihi , waswahil wanasema usinyee kambi. Nenda kwa Amani na Sio kwa Shar, ukisema dini hii sio ya haki unakua unakosea. Hiyo siyo Kaz yako
 
Wana bodi habari za usiku.

Mimi ni mkristo wa kuzaliwa na kubatizwa, mwaka 2000 nilipata kipaimara yangu kama taratibu za kanisa letu zilivyo.

Sitaki kuwachosha sana kuna mambo ambayo yamenivutia sana na kupelekea kuamini kuwa dini ya kiislam ni dini ya kweli. Mimi ni mzaliwa wa kaskazini tena kijijini haswa, nimezaliwa na mpaka naanza shule ya msingi na kumaliza elimu ya msingi nilikuwa sijui kama kuna uislamu duniani, nilipoanza form one ndiyo nikaanza kusikia kwenye kipindi cha dini kuwa kuna dini ya kiislamu, nimesoma mpaka namaliza chuo sikuweza kuamini kabisa kuwa waislamu nao ni wacha Mungu kama dini zingine.

Baada ya kutoka chuo nilipata mkataba wa kufundisha shule ya kiislamu form one na two (math) kwa mkataba wa miezi sita, shule hiyo walimu zaidi ya 90% tulikuwa wakristo na wanafunzi zaidi ya 75% walikuwa wakristo, walimu wa math tulikuwa wawili wote wakristo, mkataba wangu ulianza mwezi July lakini baada ya miezi 2 tulibadilishwa mimi nikaanza kufundisha form III – IV.

Baada ya kama miezi 3 BAKWATA(W) walianza kuhoji kwanini shule ni ya kiislamu lakini walimu wengi ni wakristo? Shehe wa (W) sitaki kumtaja maana mpaka sasa hajahama pale alituita ofisini kwake walimu wote na kutueleza madai ya BAKWATA lakini yeye akasema tufanye kazi bila tatizo na yupo tayari kututetea popote pale. Baada ya mkataba wangu kuisha Dec Shehe alinitaka niongeze mkataba pamoja na kuongezewa maslahi kitu ambacho sikutaka sababu lengo langu ilikuwa kupata mtaji wa kuanzia maisha na kujikita kwenye mambo mengine. Kwa heshima ya Shehe nilikubali kuendelea bila mkataba pindi wakipata mwalimu mwingine wa math mimi niondoke, nilikaa miezi 4 hatimaye mwalimu mwingine akapatikana lakini shehe akasema nisiondoke mpaka shule ikifungwa mwezi May. Muda wote huo nyumbani kwetu hawakujua nafanya nini sababu nilijua nikisema home mambo yatakuwa mengine kulingana na mtazamo wa home juu ya uislamu.

Nimejaribu kufikiria matendo ya hawa ndugu zetu waislamu ukilinganisha na wakristo wenzangu hakika naona waislamu ni watu wa haki sana kuliko sisi wakristo. Nitatoa mifano michache,

1. Mhe Mwinyi amewahi kuzabwa kibao mbele za watu akasamehe.

2. Mzee JK kama siyo yeye mimi na jamaa zangu huku kijijini tusigepata hiyo elimu kidogo tulionayo sababu wazazi wetu ni mafukara sana.

3. Mzee JK wapinzani walimtukana sana lakini aliwaita Ikulu wakakaa, wakanywa na kuongea.

4. Mzee JK Maaskofu walimsema lakini kwenye harambee ndiyo alikuwa anaziendeshaa bila kujali maneno yoyote.

5. Mzee JK aliteua mpinzani ambaye ni mkristo kuwa mbunge.

6. Mzee JK alimsaidia mama mmoja kumpeleka mtoto wake India alipata ajali ya bodaboda, mama huyu anasema siku moja akiwa India JK alienda kumsalimia yeye pamoja na Watanzania wengine, mama huyu ni jirani yangu huku kijijini kwetu.

7. Mzee JK tukio lolote lilipotokea alikuwa mstari wa mbele bila kujali hadhi yake.

8. Mhe Buhari na Macky Sall wameamua kumwondoa Rais wa Gambia ambaye ni muislamu mwenzao baada ya kuona anataka kudhulumu haki ya wananchi.

9. Shehe Ponda amekuwa akitetea maslahi ya watu wote bila kujali rangi wala dini zao.


Hayo ni machache kati ya mengi, nikiangalia matendo ya wakristo wenzangu(Kagame, Nkurunziza, Mseveni, Kabila, Mugabe, Askofu Mokiwa, Mzee wa upako n.k) mpaka nakata tamaa kabisa kwa matendo yao. Kumbe dini ni matendo na siyo maneno.

Mtanisamehe kwa uandishi usio na mpangilio mzuri sababu mimi siyo mtaalamu wa fani hii. Pia huu ni mtazamo wangu binafsi


Nawasilisha jamani
Sawa Mwalimu

Alafu Trump hajawaita kwenye kuliombea TAIFA vipi tuna anzia wapi Vagi?
 
Hakika dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislam.
 
Biblia yenyewe hiyo mmeandika wenyewe binadamu yaani maneno ya watu wachache mkuu soma INJILI YA BARNABA mmoja wa wale wanafunzi 12 wa Yesu. Yeye anasema Yesu alikuwa Mwislamu naye aliswali kwa kurukuu na kusujuduu.
Uislamu umezaliwa miaka Mia tano baada ya kristo kuja duniani na kifo chake sasa nani kaiga kwa mwingine


Hlf ktk biblia hakuna kitabu kama hicho acha kusikiliza maneno ya vijiweni wanakudanganya tafuta biblia usome mwenyewe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom