Nimeamua kubadili dini na kuwa Mwislamu

Nimeamua kubadili dini na kuwa Mwislamu

Status
Not open for further replies.
Comments unazozipata hapa zinadhihirisha huko ulipotoka kuna waumini wenye tabia za aina gani....
Hustahili kufanyiwa kejeli kama hivi maana ni maamuzi yako baada ya kuuona ukweli katika imani.

Ninyi mnaomkejeli mlipaswa kwanza kuhuzunika kumpoteza muumini mwenzenu na walao mjaribu kumwonesha kwanini hakupaswa kuhama...badala yake mnamtukana...watu wa ajabu sana.
Kilichonifurahisha kuanzia leo nimefahamu hapa JF tuna watu wa aina gani, nimecheka sana mkuu. Usiku mwema ndg zangu.
 
Da broo hilo la jk linaniuma sana .,viongozi wengi wa dini ya kikristo walimuandama sana jk kwasababu ya iman yake.
Ila huyu hata afanyanye madudu gani utasikia wanasifia tuu...wengine wanaimba hadi kamatia chini madhabauni..
Nkiwa kanisani nkamsikia mchngaji anasema au anamtaja rais wa sasa kwenye sala huwa natoka fasta njeeee...
Sipendagi kujikombakomba mm
 
Hakika umefanya jambo jema sana katika Maisha yako, umefungua ukurasa mpya kabisa katika maisha yako na unafaida moja kubwa sana tofauti na Mimi kwamba umeanza upya kitabu chako hivyo usikichafue tena. Kila la kheri katika Maisha yako mapya na Karibu katika Uislam.
 
Dah! mpaka leo kuna watu wanaamini isis na boko haram ni vikundi vya kiislam? Kweli tunatofautiana uelewa
Kama wanataja neno Allah wakati wakichinja binadamu unataka tuamini ni wayahudi ? Kama wanakataza elimu ya nimagharibi unataka tuelewe ni wa Hindu ? Wanajiita wanamgambo sio jeshi. Ushasikia kuna wanamgambo wa kikristu. Wakristu ni majeshi sio wanamgambo.
 
Hakika umefanya jambo jema sana katika Maisha yako, umefungua ukurasa mpya kabisa katika maisha yako na unafaida moja kubwa sana tofauti na Mimi kwamba umeanza upya kitabu chako hivyo usikichafue tena. Kila la kheri katika Maisha yako mapya na Karibu katika Uislam.
Sawa
 
Karibu san kweny uislam.Hayo ni machache saan unayoyajua.Hakika kuna meengi mzur huyajui.Jifunze uislam utakubali maneno yang
 
Da broo hilo la jk linaniuma sana .,viongozi wengi wa dini ya kikristo walimuandama sana jk kwasababu ya iman yake.
Ila huyu hata afanyanye madudu gani utasikia wanasifia tuu...wengine wanaimba hadi kamatia chini madhabauni..
Nkiwa kanisani nkamsikia mchngaji anasema au anamtaja rais wa sasa kwenye sala huwa natoka fasta njeeee...
Sipendagi kujikombakomba mm

Nilichokuwa nakitaka hapa JF leo nimekipata nitatoa ufafanuzi siku nyingine Mungu akipenda, asanteni sana.
 
Wana bodi habari za usiku.

Mimi ni mkristo wa kuzaliwa na kubatizwa, mwaka 2000 nilipata kipaimara yangu kama taratibu za kanisa letu zilivyo.

Sitaki kuwachosha sana kuna mambo ambayo yamenivutia sana na kupelekea kuamini kuwa dini ya kiislam ni dini ya kweli. Mimi ni mzaliwa wa kaskazini tena kijijini haswa, nimezaliwa na mpaka naanza shule ya msingi na kumaliza elimu ya msingi nilikuwa sijui kama kuna uislamu duniani, nilipoanza form one ndiyo nikaanza kusikia kwenye kipindi cha dini kuwa kuna dini ya kiislamu, nimesoma mpaka namaliza chuo sikuweza kuamini kabisa kuwa waislamu nao ni wacha Mungu kama dini zingine.

Baada ya kutoka chuo nilipata mkataba wa kufundisha shule ya kiislamu form one na two (math) kwa mkataba wa miezi sita, shule hiyo walimu zaidi ya 90% tulikuwa wakristo na wanafunzi zaidi ya 75% walikuwa wakristo, walimu wa math tulikuwa wawili wote wakristo, mkataba wangu ulianza mwezi July lakini baada ya miezi 2 tulibadilishwa mimi nikaanza kufundisha form III – IV.

Baada ya kama miezi 3 BAKWATA(W) walianza kuhoji kwanini shule ni ya kiislamu lakini walimu wengi ni wakristo? Shehe wa (W) sitaki kumtaja maana mpaka sasa hajahama pale alituita ofisini kwake walimu wote na kutueleza madai ya BAKWATA lakini yeye akasema tufanye kazi bila tatizo na yupo tayari kututetea popote pale. Baada ya mkataba wangu kuisha Dec Shehe alinitaka niongeze mkataba pamoja na kuongezewa maslahi kitu ambacho sikutaka sababu lengo langu ilikuwa kupata mtaji wa kuanzia maisha na kujikita kwenye mambo mengine. Kwa heshima ya Shehe nilikubali kuendelea bila mkataba pindi wakipata mwalimu mwingine wa math mimi niondoke, nilikaa miezi 4 hatimaye mwalimu mwingine akapatikana lakini shehe akasema nisiondoke mpaka shule ikifungwa mwezi May. Muda wote huo nyumbani kwetu hawakujua nafanya nini sababu nilijua nikisema home mambo yatakuwa mengine kulingana na mtazamo wa home juu ya uislamu.

Nimejaribu kufikiria matendo ya hawa ndugu zetu waislamu ukilinganisha na wakristo wenzangu hakika naona waislamu ni watu wa haki sana kuliko sisi wakristo. Nitatoa mifano michache,

1. Mhe Mwinyi amewahi kuzabwa kibao mbele za watu akasamehe.

2. Mzee JK kama siyo yeye mimi na jamaa zangu huku kijijini tusigepata hiyo elimu kidogo tulionayo sababu wazazi wetu ni mafukara sana.

3. Mzee JK wapinzani walimtukana sana lakini aliwaita Ikulu wakakaa, wakanywa na kuongea.

4. Mzee JK Maaskofu walimsema lakini kwenye harambee ndiyo alikuwa anaziendeshaa bila kujali maneno yoyote.

5. Mzee JK aliteua mpinzani ambaye ni mkristo kuwa mbunge.

6. Mzee JK alimsaidia mama mmoja kumpeleka mtoto wake India alipata ajali ya bodaboda, mama huyu anasema siku moja akiwa India JK alienda kumsalimia yeye pamoja na Watanzania wengine, mama huyu ni jirani yangu huku kijijini kwetu.

7. Mzee JK tukio lolote lilipotokea alikuwa mstari wa mbele bila kujali hadhi yake.

8. Mhe Buhari na Macky Sall wameamua kumwondoa Rais wa Gambia ambaye ni muislamu mwenzao baada ya kuona anataka kudhulumu haki ya wananchi.

9. Shehe Ponda amekuwa akitetea maslahi ya watu wote bila kujali rangi wala dini zao.


Hayo ni machache kati ya mengi, nikiangalia matendo ya wakristo wenzangu(Kagame, Nkurunziza, Mseveni, Kabila, Mugabe, Askofu Mokiwa, Mzee wa upako n.k) mpaka nakata tamaa kabisa kwa matendo yao. Kumbe dini ni matendo na siyo maneno.

Mtanisamehe kwa uandishi usio na mpangilio mzuri sababu mimi siyo mtaalamu wa fani hii. Pia huu ni mtazamo wangu binafsi


Nawasilisha jamani
Mkubwa upo sahihi maana Mungu tunayemuamini ni mmoja. Hakuna la tofauti sana ni sawa na kupanda basi tofauti na ulilokuwepo mwanzo kukufikisha unapoenda ambapo wote wanaenda huko. Hakuna Mungu wa Waislam wala rc wala sabato wala pentekoste. Mungu ni mmoja. Cha msingi ipi ni njia sahihi au gari sahihi kwa utashi wako kupanda ufike safari yako.
 
Umetaja viongozi then ukaweka n.k.
Ungemtaja tu huyo n.k hahaa
 
Noted
Mkubwa upo sahihi maana Mungu tunayemuamini ni mmoja. Hakuna la tofauti sana ni sawa na kupanda basi tofauti na ulilokuwepo mwanzo kukufikisha unapoenda ambapo wote wanaenda huko. Hakuna Mungu wa Waislam wala rc wala sabato wala pentekoste. Mungu ni mmoja. Cha msingi ipi ni njia sahihi au gari sahihi kwa utashi wako kupanda ufike safari yako.
 
Never judge a philosophy by its abuse. Tukianza kuzungumzia masuala ya ISIL/ISIS, bokoharam, Al-shabaab kama ndio dhana kuu ya uislam itakua sawa??
Give us another reason, may be you want to do so to secure your job. So far excuses ulizotoa hazina mashiko
 
Uislam ndo DINI ya haki Ulimwenguni kote na ndio maana ndio dini pekee inayopigwa vita Duniani na huu ndio USHAHIDI TOSHA KUWA UISLAMU NDIO DINI YA HAKI JAPO WAISLAMU WANAMAPUNGUFU YAO MENGI TU.
 

Kama ni ke, namwambia wala hajui anachokiwaza wala kukiwazia. Kwetu tunasema wazi wazi bila hata kushusha lepe; Mwanamke hana dini. Hivyo unaposema ati nimeamua kubadili dini, unaibadili ipi uliokuwaga nayo?? Huwezi omba chenchi ya shs elfu 5 wakati huna elf 2. Karibu tu umpate mume hata yaweza kuwa unambambia huyo shekhe wa watu. Haya ukifika tuambie tu
 
Kama wanataja neno Allah wakati wakichinja binadamu unataka tuamini ni wayahudi ? Kama wanakataza elimu ya nimagharibi unataka tuelewe ni wa Hindu ? Wanajiita wanamgambo sio jeshi. Ushasikia kuna wanamgambo wa kikristu. Wakristu ni majeshi sio wanamgambo.
Hizo ndo propaganda za Dunia kuuchafua UISLAMU kama kuwapotosha WATU(kama wewe) juu ya UISLAMU.

MUSLIM CAN NEVER BE TERRORIST, AND TERRORIST CAN NEVER EVER BE MUSLIM EVEN IF IS JUMA, AISHA, HASSAN OR OTHMAN AND MENTION ALLAH ALL THE TIME.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom