Najua Php programmers watachukia kusikia hili ila mkuu angusha Php, iweke pembeni uipotezee kwa sasa, unaweza irudia baadaye ikitokea unaihitaji sana.
Umeanza HTML -> CSS -> ?
Your next step naona should be JavaScript.
Sasa kwa nini JavaScript?
1. Kama web developer ni lazima uijue kwa kua ndiyo language pekee inayotumika kweye front-end, yaani huwezi kuikwepa la si hivyo usijiite web developer.
2. Ukiimaster vizuri utaweza kuitumia kwenye backend pia, kuna Node.js ambayo inatumika kutengeneza server, ni pure JavaScript, na tukilinganisha na Php, iko faster zaidi ya 100 times kwenye benchmarks kibao. Ni rahisi pia kutengeneza server very fast kwa Node.js kuliko Php, naongea kama mtu ambaye ni advanced in both, hii najua some people might try to attack me ila ukweli ni ukweli.
3. JavaScript ina ecosystem kubwa sana, kuna React Native framework ambayo ni pure JavaScript, hii unaweza tengeneza mobile apps zinazorun kwenye iOS, Android na later Windows, kwa kutumia codebase moja, na uzuri wa hii framework ukilinganisha na nyingine ni speed, React Native apps zinakimbia kwa speed balaa sawa na zile zilizoandikwa kwa Java au Swift.
So uende hivi HTML -> CSS -> JavaScript -> Database system (MySQL recommended)
Kumaster JavaScript kutahitaji muda mrefu na determination ya kutosha, ila it does pay off well. Php sio language mbaya, ila there's something better out there, sioni sababu ya kuhangaika na Php.
Sema pia ningekushauri kusoma general purpose language kama Java, C++ hizi zitakufundisha mambo mengi yanayofanyika ndani ya computer ambayo yatakuasidia sana in general kua developer mzuri, ukienda kichwa kichwa hutojua jinsi memory inavyofanya kazi, unavyoaccess data kama ni efficient au hapana, ndiyo maana kuna software nyingine zinaenda polepole balaa na nyingine zinakimbia. Hakuna kitu cha muhimu kwenye programming kama kujua "Data Structures na Algorithms" hizi courses mbili zinafunga kila kitu, ndipo utofauti wa serious software developer na amateur unapoonekana.