Asante kwa kuniita huku, huwa nahisi fahari sana pale natoa mchango wangu kuwasaidia wanaoanza mambo haya.
Kwa sababu unasema tayari umejifunza CSS na HTML, nafikiri kwa wewe kuifuata PHP ni jambo nzuri. Lakini pamoja na kwamba PHP ni bora na ina mambo mengi muhimu, ila ina mapungufu fulani hususan kwa wanaonza programming. Ipo legevu sana kiasi cha kufanya uwe mzembe unapoandika codes zako. Huwa inaachia au kusamehe sana mapungufu mengi kwenye suala la umakini.
Ingekua bora ukaanza na lugha zinazohimiza umakini kama vile Java, C# au C++ halafu baada ya hapo ndio ufuate PHP. Naomba usinielewe vibaya, sipondi PHP, ni lugha ambayo naipenda sana na imenisaidia katika kutegeneza solutions nyingi na nimeitumia kwa miaka mingi sana. Kuna watu kwa unafiki wao hupenda kuiponda ilhali wanaitumia kupiga hela. Nina solutions nyingi ambazo nimetumia PHP na zinafaidi jamii.
Ni lugha yenye mambo mengi ya maana na inawezesha sana. Kwanza ukiielewa vizuri halafu ujifunze Javascript na framework yake kama JQuery, baadaye ufuate framework ya PHP kama Lavarel na pia usisahau DBMS kama MYSQL. Hapo utakua umeanza vizuri.
Zingatia nilivyo orodhesha, usianze kuingia kwenye frameworks kabla hujaelewa lugha husika. Yaani soma Javascript kabla ya kujaribu JQuery au Mootools n.k. Hakikisha umeelewa PHP vizuri kabla ya kufuata frameworks kama vile Yii, Codeignitor n.k.
Jifungie chumbani na vitendea kazi, laptop nzuri, download videos, vitabu vya PDF, IDE nzuri, ingia kwenye forums...pambana tu na kitaeleweka. Pia tafuta kitabu kinachofundisha concepts za software development cycles kwa undani. Jinsi unaweza kuangalia shida fulani kwa jamii, ukaiwazia suluhisho na kudadavua/analyse hadi upate mtiririko wake na kuitatua kwa software.
Nakutakia kazi njema....