Nimeamua kuanza kujifunza computer programming (back end development)

Kwa certificate kuna chuo kipo chini ya udsm university of dar es salaam computing center kipo dar...wako vizuri pia!!

All in all chuo hakikufanyi uwe bora...what matters ni juhudi zako na passion ya IT!! Karibu sana mkuu
shukran mkuu,,mekupata vizur.sana
 
MESEJI NZURI SANA HII BRO
 
yani nimefuatilia huu uzi na comments za watu, mpaka sijui nianze na kipi maana naona vyote vizur, baada ya kuwa na uelewa wa html, css, php na java, nikasema ngoja nianze kukomaa na language moja moja nikiimaster ndio nashift kwa nyingine, nikasema nianze na java huku nikiwa natumia android studio ili nianze kwa kudevelop simple apps, lakin kutokana na errors za kwenye android studio nikaona kama natumia nguvu nyingi kujifunza vitu viwili kwa wakati mmoja, nikasema okay fine ngoja nihamie kwenye php maana niliiona haina complications nyingi compare to java, nikiwa katika hyo safari akaja classmate mmoja na idea yake kwamba tubuild android app kwa kutumia react native basi nikaweka kapuni php na kuanza kujifunza react native, nikaenda nayo mpaka sehem fulan,ikafika sehemu mawasiliano na jamaa yakapotea so project iliishia njian, nikasema sasa ngoja nirudi tena kwenye web development nikapiga piga bootstrap nikawa familia nayo. sasa nikasema nakomaa na php no matter what, yan siangalii pemben mpaka niive na niweze walau kutumia hata framework moja nikawa nimeichagua codeignitor, nikazama w3schools.com na kuanza php from the bottom, sasa leo nimepita humu nakuta na hii post ikisema ni vema kuanza na javascript yan hapa nmedata nashindwa kuchagua kama niendelee na php au nianzane na hii javascript..... naomba unishaur kidgo.
 
HTML,CSS na JS ni core technologies kwenye web development. Sasa kusoma JS sio option ni lazima kama unataka kuwaweb developer. Faida moja wapo ya JS inatumika kote front-end and backend Ila ecosystem ya JS inaumiza sana usipokua na umakini utakata tamaa, JS ina framework na Library nyingi mno mpaka ina changanya kama utakua na pupa ya kutaka kujua kila FW and LB. Ila JS ni popular sana na programers wengi wanaitumia. Kwa backend ukijua Python ni nzuri zaidi, PHP ni old technology ila bado websites nyingi zinatumia
 

Hapo ulipo kwenye PHP nenda nayo tu maana ulishaianza, PHP ya leo 7.3 ni nzuri sana, wameboresha mambo mengi sana, isome na ufanye lots of practice, japo pia pembeni unaweza ukawa unajifunza na Javascript pia, haikwepeki likija suala la web development, ila kwa zote hakikisha umeanza na core languages zenyewe kabla framework yoyote.
Cha msingi kwa chochote utakachokifanya, usiwe na pupa au haraka ya kutaka kumaliza, tumia muda wako na nguvu nyingi, kuwa mvumilivu hatimaye utashinda.
 

Komaa na kitu kimoja, kielewe vizuri, ukirukaruka utaishia kua shallow pote.
Personally sipendi php na javascript, napenda static typed languages, javascript nafanya kwa kua tu web frontend hakuna choice nyingine zaidi ya hiyo, nadhani kila developer ni muhimu ajue javascript, php naichukia, language ya kijinga sana hata aliyeitengeneza anajua kua php is shit, ila kwa market ya bongo wengi wanatumia.
 
Ulilosema php ni old technology ulikuwa unamaanisha nini mkuu
 
Ulilosema php ni old technology ulikuwa unamaanisha nini mkuu
Ni ya zamani kwenye backend, languages nyingi mpya huwa zinajaribu kusolve some problems that other din't do well. Pyhton, Go, Dart na NodeJS sinafanya vizuri, ila PHP being old imetumika Sehemu nyingi sana ndio maana kuwa replaced kirahisi inakua ngumu
 
Mkuu endelea na php javasrcipt ni simple kama una ka project umeamua fanya lugha nyingine unajifunza njiani.
 
Soko hakuna.... Labda ujifunze tu kwa burudan... Maaana iyo kitu ina raha saana unatengeneza kitu na unakiona unajikuta kama mwanasayans na wewe
 
Mkuu, ili uweze kujifunza Programming vizuri inabidi ujue ni kitu gani unataka kukitengeza kwa muda huo maana mambo ni mengi sana na ni ngumu sana kujua kila kitu. Hizi languages ni kama tools za kutusaidia kutatua tatizo letu tulilonalo. Cha msingi jitahidi uweze kumaster japo lugha mbona. Wabongo wengi ni Jack of all trades, master of none. We piga code tu. Ukiweza nunua course za Udemy zipo vizuri mno
 

Huu ushauri mzuri sana, maana nakumbuka kuna kipindi nilikomaa nikasoma 20 programming languages lakini mwishowe nikajikuta hamna hata moja niliyokua tayari kuandika solution yoyote, niliishia kuwa mweupe, ilibidi nibadilishe mkakati na kutumia lugha moja kutatua tatizo specific.
Nakumbuka pia nimewhi kujifunza lugha fulani kisa mteja alihitaji mfumo wake utumie hiyo lugha, lakini baada ya kukamilisha mradi wake yaani hiyo lugha baadaye ilinitoka, ikafutika kwenye akili yangu mpaka leo hata siwezi kuitumia kuandika 'hello world'.
Kimsingi, ni kuchagua lugha moja most efficient kwenye aina ya solutions unazotaka kuwa nazo, kisha ukomae na hiyo moja na kuitumia hadi advanced level.
 
Ok
Okey okey
 
Basi kwa kuwa umeamua kudeal na web application development, unaitaji msingi utakaokusaidia kujua namna ya kudeal na web application development.

Angalia hapa;
je unajua ili uendeshe pikipiki lazima ujifunze pikipiki Wala si baiskeli, Sasa kwanini ujifunze baiskeli na wakati unataka pikipiki, sio wote wanaoendesha pikipiki wanaweza baiskeli ila kilicho sababisha wamudu pikipiki ni malengo na msukumo.

angalia hapa;
wengi ushauri kuanza na lugha flani flani lakini si kitu cha kujadili Sana hapa maana ushakuwa na lengo maalum.
Kama una kichwa kizuri nenda direct acha kupoteza muda.
zingatia;
Hatua nzuri za kufikilia unapojifunza lugha kulingana na lengo lako.
1.angalia upatikanaji wa materials ya lugha husika
Ushauri: Kama hayapo ya kutosha angalia lugha nyingine

2.angalia utumiwaji wa lugha hiyo je ni mkubwa au la
Ushauri: Kama utumiwaji ni mkubwa chukua lugha hiyo maana itakuwa na material ya kutosha

3.usiumize kichwa kujiuliza soko linasemaje au watu wanasemaje
Kuhusu lugha Bali wewe unatakiwa kuwa na uwezo wa kubadilika kulingana na mahitaji ya client wako
Pia,
Kwa kuwa unaanza na php usiogope ila ujue kitu kikubwa ni security ukianza kujifunza security ya php lazima baadae uwe na uwezo wa kutengeneza function zako mwenyewe kwa ajili ya security kulingana mahitaji ya app yako na sio utegemee tu built-in function za php.

Mwisho kabisaàaa,

Usilemae ukapitiwa tambua web developer mzuri ni yule anayeweza kuswitch to new technology bila kujitetea na ni kulingana na maitaji ya client wake.
Technology za backend nzuri after php jifunze python.au hata ruby ni mtazamo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…