Nimeamua kuachana rasmi na Vodacom

Nimeamua kuachana rasmi na Vodacom

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,204
Reaction score
37,555
Heshima sana wanajamvi,

Wiki mbili zilizopita simu yangu ilikwapuliwa na watoto wa mjini kwakuwa nilikuwa na safari nyingi nje ya mkoa sikupata nafasi ya kurenew line yangu.

Leo nikaamua kwenda ofisi za Voda Uhuru road kwanza nikakutana na foleni kubwa kiofisi kidogo hewa gongana nikataka kuondoka lakini nikaona isiwe taabu ngoja nikomae.Kwanza nikapewa fomu nikatakiwa kujaza simu tano za mwisho,m pesa tano za mwisho,sijui kifurushi cha internet......Mara kitambulisho nikamaliza kupeleka fomu kwa mdada mwenye maringo ya kijinga kaona ajira ya Voda mali sana imemwezesha kupaka wanja na kubadili vigauni vya mtumba kabonyeza bonye computer kanirejeshea fomu namba za watu wa mwisho kuongea nao tatu sio sahihi nikamwambia kwakuwa mbili ni sahihi na simu iliibwa wiki mbili zilizopita si rahisi kukumbuka zote.Kachukua fomu kaandika loss report nenda polisi wakakujazie ebo nikamwambia nani kakwambia nina muda mchafu kwani Voda ipo yenyewe kwa taarifa yako nina line nyingine za mitandao 3 hizi si zama za TTCL na ukiritimba za enzi za Mwl nikachana fomu nikaitupia kwenye dustbin nikamwambia Vadacom kwaheri.

Masharti ya kupata line mpya iwapo simu imepotea/imeibwa yamekaa kizamani sana kama taarifa zangu zipo sahihi eg kitambulisho nilichosajilia simu,majina na nk yapo sawa kwanini wanaleta urasimu wa kuangaisha wateja.
 
Hehehe mkuu voda majanga na watazidi kupoteza wateja zao....
 
Nilikuwa nikitumia Voda kwaajili ya Mpesa mtandao wa Airtel uko poa sana ukijiunga na yatosha 20,000/= unapatiwa 375 dakika,3500 sms and 300 MB.

Voda wana dharau sana kuanzia wakurugenzi wao hadi wafanyakazi wao
Hawana customer care nzuri, Naskia sahv wameitoa uhuru intenet ile ya tsh 1000
Bora wakimbiwe tu
 
Nimeshangaa sana sijui wanafanyakazi katika dunia ipi nina uhakika wataondolewa kwenye soko iwapo hawatabadili aina ya wafanyakazi sijui wameiba vyeti au ndio zile ajira za kushikwa mkono.Unapoingia hizo ofisi za Vodacom zipo counter 3 kushoto na moja kulia halafu kuna dawati amabalo ndipo alipo mdada mweusi mjinga wa viwango vyote hana kauli,hajui nani ni nani kwa muda wa dakika 15 nilizokupo pale nimeshuhudia akikwaruzana na wateja watatu.

Voda wana dharau sana kuanzia wakurugenzi wao hadi wafanyakazi wao
Hawana customer care nzuri, Naskia sahv wameitoa uhuru intenet ile ya tsh 1000
Bora wakimbiwe tu
 
Si kwamba ni utaratibu wa TCRA? Maana wizi wa kutumia simu umekithiri sana.

Pia ni muhimu ukaripoti polisi upotevu wa simcard yako, maana inaweza kutumika vibaya halafu ikakuletea shida nyingine tena. Loss report ya polisi inakusaidia wewe endapo simu yako au simcard/namba yako ikijatumika kwenye uhalifu.

Lakini kwa vyovyote vile urasimu unakera sana.
 
Eti nenda Polisi kaandikiwe loss report sijui wanafikiri tuna muda mchafu.Polisi mtu unakwenda kama kuna issue ngumu si mahali pa kwenda hovyo hovyo na vi issue vya kijinga.

Umekutana na mpuuzi sana. Mi nlikua sijatumua line ya tigo mwaka mzima na nlikua sikumbuki namba hata moja ya mwisho wala tigo pesa ila kitambulisho kiko sawa wakarenew hapo hapo. Na airtel nliibiwa simu hata hawakuhitaji huo upuuzi mwingi hvy. How does a person remember all that shit? Umechelewa kugundua kwamba voda ni wajinga. Mi siku hizi voda simu inakaa home. Naitumia kama mtu ananitumia pesa na hana mtandao mwingine
 
Mbona Airtel hakuna huo upuuzi.Wakikupatia line maana yake line iliyoibwa haiwezi kufanyakazi tena.Loss report ni kama nilikuwa nataka kuifatilia simu yangu lakini si muda huo hata kidogo.

Si kwamba ni utaratibu wa TCRA? Maana wizi wa kutumia simu umekithiri sana.

Pia ni muhimu ukaripoti polisi upotevu wa simcard yako, maana inaweza kutumika vibaya halafu ikakuletea shida nyingine tena. Loss report ya polisi inakusaidia wewe endapo simu yako au simcard/namba yako ikijatumika kwenye uhalifu.

Lakini kwa vyovyote vile urasimu unakera sana.
 
Polisi kwenyewe unaenda wanakuzingua kisa cha kujipeleka kwa sababu ya line tu ni nini? Labda kama ingekua ina milion mpesa ndo ningejipeleka ili niitoe na kuwasahau
 
Ukienda polisi kwanza wanakupatia fomu ya loss report wanakwambia katoe photocopy ukikutana na nja kali wanakuomba hata nakala kumi hivi wakikujazia utasikia sasa Mzee maana yake 5,000/= au 10,000/= ikutoke ndio maana nikasema polisi labda ingekuwa ni kitu kikubwa kweli kweli si simu ambayo nina uhakika siwezi kuipata tena.

Umenikumbusha kuwa kesho naenda kununua line ya mtandao wa halotel na tigo. voda nitakuwa napokelea simu za kazini kwangu. Voda hovyo kabisa.
watu tunaadimika internet kisa vifurushi wanazidi kupunguza mb.
 
Ukienda polisi kwanza wanakupatia fomu ya loss report wanakwambia katoe photocopy ukikutana na nja kali wanakuomba hata nakala kumi hivi wakikujazia utasikia sasa Mzee maana yake 5,000/= au 10,000/= ikutoke ndio maana nikasema polisi labda ingekuwa ni kitu kikubwa kweli kweli si simu ambayo nina uhakika siwezi kuipata tena.

Niliripoti simu nikaishia kutongozwa. Kwa heri simu yangu note4
 
Heshima sana wanajamvi,

Wiki mbili zilizopita simu yangu ilikwapuliwa na watoto wa mjini kwakuwa nilikuwa na safari nyingi nje ya mkoa sikupata nafasi ya kurenew line yangu.

Leo nikaamua kwenda ofisi za Voda Uhuru road kwanza nikakutana na foleni kubwa kiofisi kidogo hewa gongana nikataka kuondoka lakini nikaona isiwe taabu ngoja nikomae.Kwanza nikapewa fomu nikatakiwa kujaza simu tano za mwisho,m pesa tano za mwisho,sijui kifurushi cha internet......Mara kitambulisho nikamaliza kupeleka fomu kwa mdada mwenye maringo ya kijinga kaona ajira ya Voda mali sana imemwezesha kupaka wanja na kubadili vigauni vya mtumba kabonyeza bonye computer kanirejeshea fomu namba za watu wa mwisho kuongea nao tatu sio sahihi nikamwambia kwakuwa mbili ni sahihi na simu iliibwa wiki mbili zilizopita si rahisi kukumbuka zote.Kachukua fomu kaandika loss report nenda polisi wakakujazie ebo nikamwambia nani kakwambia nina muda mchafu kwani Voda ipo yenyewe kwa taarifa yako nina line nyingine za mitandao 3 hizi si zama za TTCL na ukiritimba za enzi za Mwl nikachana fomu nikaitupia kwenye dustbin nikamwambia Vadacom kwaheri.

Masharti ya kupata line mpya iwapo simu imepotea/imeibwa yamekaa kizamani sana kama taarifa zangu zipo sahihi eg kitambulisho nilichosajilia simu,majina na nk yapo sawa kwanini wanaleta urasimu wa kuangaisha wateja.

CC: Vodacom Tanzania
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom