Nimeamini wanaume hawaaminiki

Habari!
Nimekutana na mkasa ambao umenifanya niamini wanaume sio watu wa kuwaamini 100%

Mimi ni mtu ambae muda mwingi najifungia ndani, lakini ikitokea nimekua mpweke sana huwa napendelea kwenda kwa jirani mwenye nyumba inayofuata baada ya kwetu.

Tumeshakua ni washkaji japo yeye ni mtu mzima kiasi, ana mume na watoto watano. Ila mimi na yeye tunaongea lugha moja. Mshkaji wangu namwita Mama Cathe. Anapendana sana na mume wake familia yao ni bora yenye upendo, kuwaona wamekumbatiana na mume wake ni jambo la kawaida sana.

Nipo karibu nae nimejua baadhi ya mambo, mume wake huwa anarudi kila siku mchana kula, mama Cathe huwa anamsubiri mchana ili wale wote saa 9.

Kwa jinsi wanavyopendana usiku wanaweka msosi nje wanakula mume, mke na watoto kulishana ni jambo la kawaida. Siku zote ninavyowachora mume anampenda sana mkewe, nilikua naona hawezi hata kumsaliti, hata michepuko haijui. Nilikua naamini kuna wanaume ni waaminifu na huyu Baba Cathe nilimuweka kundi hilo kwa jinsi wanavyoishi.

Juzi asubuhi mama kanituma nikanunue mahitaji, natembea zangu kwenye uchochoro mpana nikasikia mtu ameniita 'Ephen!' nikageuka nyuma. Nakutana na Baba Cathe akaniambia 'Nilikuona wakati unatoka nikasema nikufate sababu kila siku navizia nafasi ya kuongea na wewe lakini siipati, kwani unaenda wapi?'

Mpaka hapo nikawa nimeshangaa sikutegemea hii kauli kutoka kwake, hapo anaongea kimahaba
Huyu mzee nilikua namuheshimu sana....Nikamwambia naelekea dukani.

Akasema 'basi naomba namba yako siku yoyote naweza kukupigia tukutane sehemu X, huwa unanivutia sana nahitaji tuongee zaidi' nikamjibu sina simu

Alarm ikalia kichwani kwangu kua ule uchochoro yeyote anaweza kutokea ikawa kesi, sikumjibu nikageuka nikaendelea na safari yangu. Mimi nipo mbele yeye nyuma hapo natembea chap niumalize uchochoro akawa anaongea maneno ambayo siwezi kuyaandika hapa.

Nikamaliza uchochoro na yeye nahisi huku nyuma aligeuza, muda wote nikawa najiuliza huyu mzee kapatwa na nini?

Kilichonishtua ni jana nimekaa kibarazani na mkewe mida ya mchana, karudi mke wake akasimama kumkumbatia, huyu mzee akanikonyeza. Namuona anakuja kwa kasi!

Wanaume wote kumbe wanacheat.....!
Angalizo , mwanaume wake ndio aaminiki. It funny kwakweli kama mwanaume mmoja au wachache wanafanya jambo lisilo sawa halaf lawama wanatupiwa wanaume wote duniani, including wale wema
 
Habari!
Nimekutana na mkasa ambao umenifanya niamini wanaume sio watu wa kuwaamini 100%

Mimi ni mtu ambae muda mwingi najifungia ndani, lakini ikitokea nimekua mpweke sana huwa napendelea kwenda kwa jirani mwenye nyumba inayofuata baada ya kwetu.

Tumeshakua ni washkaji japo yeye ni mtu mzima kiasi, ana mume na watoto watano. Ila mimi na yeye tunaongea lugha moja. Mshkaji wangu namwita Mama Cathe. Anapendana sana na mume wake familia yao ni bora yenye upendo, kuwaona wamekumbatiana na mume wake ni jambo la kawaida sana.

Nipo karibu nae nimejua baadhi ya mambo, mume wake huwa anarudi kila siku mchana kula, mama Cathe huwa anamsubiri mchana ili wale wote saa 9.

Kwa jinsi wanavyopendana usiku wanaweka msosi nje wanakula mume, mke na watoto kulishana ni jambo la kawaida. Siku zote ninavyowachora mume anampenda sana mkewe, nilikua naona hawezi hata kumsaliti, hata michepuko haijui. Nilikua naamini kuna wanaume ni waaminifu na huyu Baba Cathe nilimuweka kundi hilo kwa jinsi wanavyoishi.

Juzi asubuhi mama kanituma nikanunue mahitaji, natembea zangu kwenye uchochoro mpana nikasikia mtu ameniita 'Ephen!' nikageuka nyuma. Nakutana na Baba Cathe akaniambia 'Nilikuona wakati unatoka nikasema nikufate sababu kila siku navizia nafasi ya kuongea na wewe lakini siipati, kwani unaenda wapi?'

Mpaka hapo nikawa nimeshangaa sikutegemea hii kauli kutoka kwake, hapo anaongea kimahaba
Huyu mzee nilikua namuheshimu sana....Nikamwambia naelekea dukani.

Akasema 'basi naomba namba yako siku yoyote naweza kukupigia tukutane sehemu X, huwa unanivutia sana nahitaji tuongee zaidi' nikamjibu sina simu

Alarm ikalia kichwani kwangu kua ule uchochoro yeyote anaweza kutokea ikawa kesi, sikumjibu nikageuka nikaendelea na safari yangu. Mimi nipo mbele yeye nyuma hapo natembea chap niumalize uchochoro akawa anaongea maneno ambayo siwezi kuyaandika hapa.

Nikamaliza uchochoro na yeye nahisi huku nyuma aligeuza, muda wote nikawa najiuliza huyu mzee kapatwa na nini?

Kilichonishtua ni jana nimekaa kibarazani na mkewe mida ya mchana, karudi mke wake akasimama kumkumbatia, huyu mzee akanikonyeza. Namuona anakuja kwa kasi!

Wanaume

Mimi nimepumzika sasa naona hakuna umuhimu kabisaaa
 
kumwamini mwanaume kwamba hawezi kutongoza nje ni ujinga unaotokana na kukumbatia mafundisho ya wazungu, waliyoyaleta kwa maslahi yao, maana kwa asili kila kiumbe cha kiume kinazo sababu za asili kuwa na jike zaidi ya moja.
Ibrahimu baba wa imani ya kikristo alikuwa na wake wengi
japo uzinzi haukubariki,

soma hapa:
1: Ibrahimu wake 3 (1nyakati 1:32, na mwanzo 25:1 pamoja na 25:6)
2: Yakobo wake 4 (Mzo 31:17)q
3: Daudi wake wa 7 na masuria kadhaa [1nyakai 3 inaeleza wake 7 ]Basi hawa ndio wana wa Daudi, aliozaliwa huko Hebroni; Amnoni, mzaliwa wa kwanza, mwana wa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili, Danieli, wa Abigaili, Mkarmeli; wa tatu, Absalomu, mwana wa Maaka, binti 9Talmai, mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, mwana wa Hagithi; wa tano, Shefatia, wa Abitali; wa sita, Ithreamu, kwa Egla, mkewe. Sita alizaliwa huko Hebroni; na huko akatawala miaka saba na miezi sita; na huko Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu. Na wana wa Elioenai; Hodavia, na Eliashibu, na Pelaya, na Akubu, na Yohana, na Delaya, na Anani, watu saba.
1 Mambo ya Nyakati 3:1‭-‬4‭, ‬24 SRUVDC

1 Mambo ya Nyakati 3:1 Basi hawa ndio wana wa Daudi, aliozaliwa huko Hebroni; Amnoni, mzaliwa wa kwanza, mwana wa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili, Danieli, wa Abigaili, Mkarmeli | Swahili Revised Union Version (SRUVDC) | Pata programu ya bure ya Bibilia sasa hivi. -24.SRUVDC
(1samweli 27:3,)
4: Sulemani.wake700 na.masuria 300
(1Wafalme 11:3)
5: Rehoboamu wake 18 masuria 60
(2nyakati11:21)
6: Abia wake 14 (2nyakati 13:21)
7:Lameki wake wa2 (mwanzo.4:23)
8: Elikana wake wa2 (1samweli 1:2)
9: Shaharahim wake 2 (1nyakati 8:8)
10: Rehoboamalioa wengi (2nyakati11:21)
11: Beerhjaza wakewengi (Dan 5:2)
12: Yoashi wa 2 (2nyakati 24:3)
13: Elikana wa2 (1sam 1:2)
14: Gidioni wengi (Waamuzi 8:30)
 
1711968881156.jpg
 
Mwanamke mwenye hekima huwa hashangai mumewe akimcheat ndivyo tulivyo haturidhiki na K moja

Mfano mzuri ni aliyekuwa raisi wa Marekani Bill Clinton kwa miaka 2 alimcheat mkewe Hillary Clinton kwa kutoka na secretary wake. Na mkewe Hillary hakwenda mahakamani kudai talaka kwa sababu alijua ndivyo tulivyo

Men are polygamous by nature
Hamna cha nature wala nn kutetea tu uzinzi
 
Back
Top Bottom