Nimeamini US anaihofia sana China

Nimeamini US anaihofia sana China

Drone Camera

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2017
Posts
14,157
Reaction score
14,120
Ni kuhusu OpenAI. Karibuni hapa imetangaza kwamba developers wa China hawataweza kutumia API zao kutengeneza products.

Ikumbukwe kwamba nchi hizi mbili zipo kwenye vita ya kiuchumi na kiteknolojia. Na katika sekta ya teknolojia, hakuna ubishi kwamba akili mnamba ndo iliyoshika hatamu kwa sasa. Ila ni wazi kaka mkubwa anataka kushika portion kubwa ya keki hii kwa muda mrefu.

Mtandao wa kurank hizi LLMs (The tech powering ChatGPT) uitwao Hugging Face umeonyesha LLMs kutoka China umezishinda baadhi ya LLMs za kampuni kubwa za Marekani. Mfano, Qwen2 ya Alibaba imeishinda hata Llama 3 ya Meta.

China ndo taifa linaloweza kukabiliana na Marekani sekta hii. Na ni kama kaka mkubwa anaogopa kasi ya bwana mdogo hapa.

Mimi najiuliza, kama lengo la Marekani ni kulinda taarifa za raia wake dhidi ya washindani wake (kama ilivyokuwa ishu ya TikTok) basi ingependezwa na matumizi ya OpenAI China maana hii kampuni nasikia hata lengo lake la kuifanya gtp-4 iwe free ni ili waweze kukusanya data zaidi kisha wazitumie kutrain na kuzifanya GPTs zijazo ziwe more powerful. Sasa nashangaa inakuaje wanaacha kutumia hii chance ya kukusanya data za wachina.

Kama lengo ni kuifanya China iwe nyuma katika sekta hii, basi naona ni kama wamechelewa maana imeshapiga hatua sana uwanja huu kiasi cha kuwapa challenge halisi.

Siichukii Marekani wala si shabiki wa haya mabavu wanayooneshana ila penye ukweli ni vema kutia neno.

Hii pia ni alarm kwa nchi zingine kujipanga katika teknolojia hii ili kuepuka mambo haya siku za mbeleni kama source ilivyoshauri.

Source: The Batch, deeplearning.ai

Full Article: OpenAI Blocks China, Tests for Human-Level Models, Music Industry Sues AI Startups, Model Merging Evolves
 
Hata hizi "chip wars" sababu kubwa ni Mmarekani aliona mchina anakuja kwa kasi sana upande wa AI ndo maana akazuia makampuni yake na maswahiba zake yasiwauzie chip zozote(cpu,gpu) maana hii teknolojia ya AI pia inaenda kutumika kijeshi sasa mchina akimpiga gap kubwa mmarekani atamsumbua pia huko vitani ,japo na hivyo vikwazo vyote mchina bado anaonekana anaendelea kua tishio upande huo
 
Kadri Mmarekani anapojaribu kumzuia China asitumie bidhaa zake ndivyo Jinsi mchina anavyojichimbia LAB kutengeneza vya kwake mwenyewe.

Nchi yenye vichwa milion 400 haiwezi kulingana na nchi yenye vichwa bilion 1.5 vyenye akili hata siku moja!. NI SUALA LA MUDA TU NA MIPANGO MAKINI NA UTEKELEZAJI
 
Nadhani lengo la OpenAI ni kuizuia China kutumia model kama GPT 4o ku generate synthetic data kwa ajiri ya instructions tuning, hii ni method effective sasa hivi kupata training dataset wakati wa ku fine tune base models

Ila ni pointless kuizuia China, watunga sera wa Marekani sijajua ni wanafanya makusudi au kweli hawajui kuwa China kwa sasa ni mkubwa kuliko wao, tayari China ameshwapita kwenye uchumi tangu 2017 na ni China ndio inaongoza kuchapisha papers nyingi kwenye A.I

Pia Large language models sio ngumu kutengeneza, 100% ya sayansi yote ipo public, kama una computing power ya kutosha na access ya high quality data ni easy ku reproduce model yenye level ya akili kama Gemini au GPT 4

Hata huku tukiweza ku afford computing power, tunaweza develop na ku train local models zetu, LLM sio siri ya kumficha mchina

Na inachekesha kwasababu OpenAI wanaji brand kuunda A.I kwa faida ya binadamu wote, ila nadhani wachina sio binadamu tena
 
Marekani kwa sasa ina viongozi wajinga, Ni kama Tembo anayeogopeshwa na Nyati.
Uchumi wa Marekani ni joke anyway
Ume rely kwenye ku print dollars na over inflalated stock market huku 1% percentage ya wamarekani waki own 90% ya total wealth
Pro U.S wengi wa Africa wana ile image ya Marekani iliyosukwa na Hollywood....Mpaka leo najiuliza kivipi Elon Musk ni tajiri namba moja duniani?
 
China ndo taifa linaloweza kukabiliana na Marekani sekta hii. Na ni kama kaka mkubwa anaogopa kasi ya bwana mdogo hapa.
China sio bwana mdogo.

Marekani anaufahamu ukubwa wa China kitambo tu hata baada ya uhusiano wa China na Usoviet kuyumba miaka ya 70 marekani alifurahi sana akajisogeza karibu zaidi na China naye China akajenga uhusiano wa karibu na marekani kumbe kila mmoja alikuwa na target zake matokeo nafikiri sasa tunaanza kuyaona nani alimsoma mwenzake vyema.
 
Kama umefika Hong Kong na Shanghai na ukafika New York,Chicago na LA utaona kuwa mchina yupo mbali sana ya Marekani na Ulaya yake.
Taarifa mwenyekiti.......hiyo Hong Kong imejengwa kwanza na wazungu........harafu huwezi kufananisha ulaya na china........maana miji mingi ya ulaya au amerika ni ya kihistoria majumba mengi ya thamani ni ya miaka mingi tofauti na hii inchi ya Mao ambao hawana kipya zaidi ya ku copy and paste.......harafu ujiingize kwenye league ya ubunifu hapana kwa kweli...........
 
Taarifa mwenyekiti.......hiyo Hong Kong imejengwa kwanza na wazungu........harafu huwezi kufananisha ulaya na china........maana miji mingi ya ulaya au amerika ni ya kihistoria majumba mengi ya thamani ni ya miaka mingi tofauti na hii inchi ya Mao ambao hawana kipya zaidi ya ku copy and paste.......harafu ujiingize kwenye league ya ubunifu hapana kwa kweli...........
Hii forbidden city imejengwa toka miaka ya 1400
entrance-Gate-of-Divine-Might-Beijing-Forbidden.jpg


Unafikiri China imeanza baada ya Mao wewe jamaa bwana, sasa kati ya China na hiyo miji ya ulaya nani ni mkongwe
 
Marekani kwa sasa ina viongozi wajinga, Ni kama Tembo anayeogopeshwa na Nyati.
Siku zote siasa uvutia watu wajinga na wapumbavu zaidi kuliko wenye akili ....ku solve ili tatizo ni lazima .. kuwe na reseni ya kisiasa itakayo lipiwa pesa kama sh mil 4 kila miaka 5 na kuwe na marufuku wanasiasa kuwa wapiga kura kwenye chaguzi za kitaifa ...haya mambo mawili yatafanya vyama vya siasa kuwa na watu wachache makini.
 
Back
Top Bottom