Let's go..............
Ilikuwa mwaka jana mwezi wa 8 nilipopata wazo hilo nikaona inafaa bas nikaona so shida nimshirikishe Yuda.
Nilishangaa baada ya kumwambia tu kwamba nimepata wazo la kutafuta frem ya retail jamaa akastuka tulikuwa dukani kwake tumekaa nikaona mwamba akauliza kwa kuhamaki kama mtu ambaye hakuskia vzr jambo aloambiwa vile.
Jamaa akauliza umesema?? Nikamuliza mbona umestuka hvo? Jamaa akavunga, mimi nilirudia tena yale maelezo. Jamaa akacheka kwa dharau akanambia "unadhani kufungua duka ni kama kunywa maji" sio rahisi wewe endelea na kazi yako tu achana na hilo wazo.
Asee to be honest ilinikata sana ile issue, mm nilimfata yule jamaa kwasababu niliona ni mjanja kuliko wale wengine na machimbo mengi ya dar anayajua lakini pia anambinu nyingi za kuwawin wateja ukizingatia hata kwenye mauzo na kufungasha anawazidi wale wa2 wengine.
Jamaa niliona ni bora nimfate yeye kwasababu huwa tunapata time ya kuzungumza na kushauriana vitu.
Tulikuwa tunashirikiana katika kudizaini visibility ya maduka yake.
Jamaa anawadogo zake wa2 plus yeye pia walikuwa na tabia chafu sana kwahyo kwa kadri nilivoweza niliwashauri na kiwabadilisha na wakawa wanabadilika slowly mpka wakafanikiwa atleast kuwa watu wa maana.
Kuna kipindi waliweka tangazo wakaambatanisha na mziki wa Dayoo ule huu mwaka mtaniita boss, mimi kiukweli niliona siyo sahihi kuwaambia wateja ambao ndo maboss wako kwamba huu mwaka watake wasitake watakuita Boss kibiashara niliona haiko sawa tangazo kuliambatanisha na ule wimbo nimfata jamaa nikamwambia. Jamaa akapanic akanitolea maneno mazito, akaniita mimi snitch kifupi aliona kma vile kapatia sana hundred percent kuweka ule wimbo kwenye tangazo. Jamaa nikamuonba fair tu nikamuonba msamaha anisamehe kama anaona nimemkosea. Mimi nikakaa kimya.
Baada ya kama siku tatu hivi wateja wakapita pale karibu na duka lake walikuwa wanapiga njiani jamaa huwa wanatabia ya kuwakaribisha wateja yani kifosi vile.
Wateja wakalopoka "yani unatuamrisha tukuite Boss hafu unategemea tuje tukuungishe" mimi nilikuepo lakin kulikuwa na makelele ya mziki na matangazo, nilisikia walichoongea lakini nikavunga kama vile skuskia.
Jamaa akapanik na huwa hatak kushindwa akawafokea wateja akamwambia sepeni ntauzia wengine, yote niliskia lakin nikajifanya sjaskia.
Walikuwa na tabia ya kuwatongoza hovyo wateja hasa wanachuo, nikawambiateja hatongozwi mtapoteza wateja wengi sana, mwanzo waliniona fala baadae wakapruv wenyewe kwamba ni kweli mteja hatongozwi kwasababu kuna mambo walipitia yaliwaharibia reputation wakakumbuka maneno yangu na waka apologize kwamba ni kweli walikuwa wanakosea.
Sasa baada ya lile tukio la wale wateja kumchana msela kwamba anawaamrisha wamuite Boss huu mwaka, na kumchana kwamba hawawez kumuungisha jamaa alipoa sana na nashukuru alidhania kwamba sikusikia kumbe nilikuwa nimesikia yote na nilishuhudia kwa macho na maskio yangu.
Tutaendelea.........