Nimeamini kweli tanzania ni kichwa cha mwendawazimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeamini kweli tanzania ni kichwa cha mwendawazimu

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mahatma Gandhi, Jan 17, 2012.

 1. Mahatma Gandhi

  Mahatma Gandhi Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mambo vipi Wanajamii Forum???Naomba musome hapa kwa makini kisha tujadili katika hili.Juzi nilikuwa nasoma ripoti ya UNDP ya mwaka 2011 kuhusu hali ya maendeleo katika nchi 187 wanachama wa UN.Ripoti hiyo imezigawa nchi hizo katika makundi makuu manne;yaani nchi zenye maendeleo ya juu sana,ya kati,chini na maskini sana.Nchi za Norway,Australia,Uholanzi,Marekani,New Zealand,Canada,Ireland,Liechtenstein,Ujeruman na Uswisi ziko katika kumi bora kimaendeleo.Barani Afrika nako Ushelisheli ni ya 52 na ni ya kwanza katika Afrika ikifuatiwa na Libya(ya 64 ingawa kulitokea mapinduzi mwaka jana) na ya tatu ni Mauritius(ya 77).Tanzania yenye madini kibao (hususani Tanzanite),mito,maziwa,bahari na misitu inashika nafasi ya 152 na ni kati ya nchi zilizo katika kundi maskini sana pamoja na DRC yenye Diamond,misitu(kwa ajili ya mbao),mto Congo,ziwa kivu n.k inashika nafasi ya mwisho (187).Ebu waungwana sisi kama wadau wakubwa wa maendeleo ya nchi yetu na bara la Afrika kwa ujumla tufanye tafakuri.Hivi hizi rasilimali (nilizotaja hapo juu) zipo kwa ajiri ya kutufanya tuwe maskini wa kutupwa kila kukicha?,au Mungu alitupa kama laana bila sisi kujua(lakini nisingependa kumkufuru Mungu wangu)?,na je hatuwezi kuzitumia kujiletea utajiri kama Norway na Australia?? Hivi katika hili,tatizo ni nini????
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  Kama baba b.w.e.g.e, familia nzima ni b..w.eg.e.
   
 3. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  wizi mtupuuuuuuuuuuuu.
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono 100% na "baba" wa hili Taifa anajulikana.
   
 5. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kweli kuna Laana Africa, sijui tumemfanya nini Mungu wetu Waafrika.
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hayo ni matokeo ya kuchagua kuongozwa na watu wasio na nia ya kuongoza.
   
 7. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,065
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  CCM na watoto zake nyerere ,mwinyi ,mkapa na now mtoto dhaifu kuliko wote kikwete ,,,hao ndo baba wa taifa letu.
   
 8. N

  Nyalutubwi JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 572
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Tatizo ni mfumo wetu wa jinsi ya kuchagua watu wa kusimamia raslimali zetu.
  1. Kama bado tunawateua makada wa vyama vya siasa wasio na elimu wala utaalamu wa kusimamia masuala ya kiuchumi tusitegemee kupiga hatua za kimaendeleo.
  2. Kama viongozi wetu wa kitaifa tunaowachagua kusimamia raslimali za Taifa ndio hao tunawasikia kweye skendo za wizi kama EPA,Richmond,Meremeta,IPTL na Mikataba ya ovyo kwenye sekta mbalimbali zikiwemo za madini mbuga za wanyama una haja gani kuangaisha akili yako kujua tatizo la umasikini wa Tanzania unaletwa na nini?.
  3. Kama Taifa kupitia viongozi walioko madarakani linakuwa na sera mahususi ya kuua mfumo wa Elimu kwa Watu wake ili mradi tu watu wachache na familia zao waendelee kuendeleza tawala zao umasikini lazima ushike kasi.
  4. Madhara ya mfumo huo kiuchumi ni mengi na ya muda mrefu kuweza kuyaondoa katika mfumo mzima kiuchumi
  5. Ingawa kwa uchache nimejaribu kuonyesha hayo naachia wengine nao watoe maoni yao.
   
 9. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tusisingizie lolote hapa hivi maprezda wa Rwanda na Burundi kili watokeaga nini hapo miaka ya nyuma??
   
 10. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nyerere hapana ... Huyu babu alikuwa na upeo mkubwa sana ndio maana aliamua kuzibania rasilimali zote mpaka hapo Wa-TZ watakapoamka kutoka usingizini.
   
 11. sister

  sister JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,029
  Likes Received: 3,940
  Trophy Points: 280
  ubinafsi ndo unatusumbua kwa kweli, mtu anajifikilia yeye kama yeye nyie wengine mtajijua wenyewe. viongozi wetu hawana huruma hata kidogo we fikiria mtu akitaka kufanya changes ambayo viongozi wanaona watapoteza manufaa yao basi huyo mtu atafanyiwa kila njia anyamazishwe na asiendelee na mikakati yake. tunawadhamini wageni kushinda kitu chochote, wageni kwetu ni miungu watu, utakuta mzawa ana uwezo wa kufanya kitu apewi ile chance ila mgeni inapewa tena kwa mkopo na punguzo I HATE IT.
   
 12. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,382
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  Hii nchi inaitwa utajiju. Kila mtu na lake. Laisi na lake wmkuu na lake ikulu na lake bunge na lake wakuu wa mikoa na wilaya na ajenda zao wananchi na lao polisi na lao wasomi na lao wanasiasa na lao. Hamna maridhiano. No common goals kila niliyemtaja anaangalia majaliwa na maslahi yake pale alipo
   
 13. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mpaka kila mtanzania wa ngazi yoyote atakapojua maana ya uzalendo ndipo tunaweza kujikwamua
   
 14. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa, tena kuijua maana halisi ya maendeleo, sio blah blah za wanasiasa.
  Nakumbuka mwaka juzi kabla ya uchaguzi palikuwa na mdahalo mmoja ambao Eng. Stella Manyanya aliiwakilisha CCM alisema kuwa tumepiga hatua kubwa kimaendeleo na kufafanua kuwa kwa sasa watu wengi wanamiliki simu za mkononi kama moja ya mifano ya jinsi tulivyopiga hatua kubwa kama taifa! Nlijiuliza sana juu ya hiyo kauli yake, kwa Elimu yake na uhalisia mzima nikagundua na yeye ni wale wale wapayukaji...
   
 15. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #15
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  Kuna tofauti ya mfumo na ideology iki-fell na mtu as a single unit ku-fell

  Mfumo/ideology uki-fell tunasema mfumo/ideology b.w.e.g.e
  Na a single unit iki-fell tunasema baba b.w.e.g.e
   
 16. n

  nhyama Member

  #16
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  hili halina ubishi cha msingi tutafute mchawi na kumtoa na ni kama viongozi watolewe.
   
Loading...