Not_Yet_Uhuru
JF-Expert Member
- Oct 11, 2010
- 1,304
- 431
Wadau;
Hii Sio siri tena! Tumekuwa tukilisema hili na kurudia kuwa, ili wanaoiamini sana CCM ya sasa wajirudi na kuwa upande wa umma, wawe wazalendo. Na kuwa, watanzania wa sasa sio wale ambao walikuwa 'wanaleweshwa' na nyimbo za CCM, na kulewa sifa za kutungwa, kupewa hongo za pombe, khanga, t-sheti, kofia, pilau na kubebwa ktk magari ya matarumbeta na nyimbo za TOT na kuambulia kushiba kwa siku mbili au tatu huku wakiuza Kura zao kwa 'ujira wa mlo' au 'uniform' na kuteseka kwa miongo na miongo ya miaka!
Kauli hizi nzito, zinatoka kwa baadhi tu ya watu 'nguli' ambao ndio 'wenye CCM' na zinawahakikishia washabiki wanaoiamini sana CCM ya kuwa itabaki madarakani, 'wajiandae' maana CCM haielekei kuhimili mabadiliko, na Kimbunga cha hasira ya Umma, na kuvuka salama ktk Kura Oktoba 2015!
My Take;
Taifa linakwenda kukombolewa ifikapo Oktoba. Welcome Tanganyika Mpya!
Huu ndio ujumbe wa Ukombozi kwa wazalendo na UKAWA chini ya LOWASSA! Bado wale 'wachumia tumbo' Lizaboni, Simiyu Yetu, MwanaDiwani, Ritz et al..na 'vitendea kazi' wengine wa Gamba's kuwa huu ni wakati wao 'kujiunga na ukombozi wa Umma', MAKOMEA atawahi kulala tarehe 25/10/2015 '...Utawala wa UKAWA ni Mpango wa Mungu...hauna muda wa kulipiza kisasi!' - by F. A. Mbowe, [UKAWA, 24 May 2015]
Tunakumbushia tu na kuweka dira sawa...Ndiko tunakoelekea??

- Jaji Joseph Warioba na Joseph Butiku kwa nyakati tofauti, walishaitahadharisha CCM na uongozi wake kuwa kwa walipoifikisha CCM na taifa kwa sasa, hii sio CCM waliyoijua ya wakulima na wafanyakazi, wananchi wanaweza kuiondoa madarakani. Baadhi ya Viongozi wa sasa wa CCM wakawabeza na kusema wamezeeka vibaya.
- Mh. Cleopa David Msuya (waziri mkuu mstaafu), amesema mara kadhaa na kurudia tena wiki hii kuwa CCM isipoangalia vyema ina uwezekano mkubwa wa kuondolewa Madarakani mwaka huu.
- Mh. Frederick Sumaye (waziri mkuu mstaafu), naye ameshasema mara kadhaa kuwa kwa jinsi CCM ilipofikia sasa, isipofanya maamuzi sahihi, kuna wasiwasi wa kushinda hapo Oktoba Mwaka huu.
- Mama wa Taifa, mama Maria Nyerere alishawaambia CCM kuwa kwa jinsi walivyokwishavuruga maadili ya Taifa yalivyoasisiwa na Baba wa Taifa, wananchi wa sasa sio wa enzi za Mwalimu, na wanaweza kuchagua Vyama vungine kutawala.
- Mh Balozi Paul Ndhobo; aliyekuwa mtu muhimu sana ktk Uongozi na Utawala wa CCM awamu wa 1 na 2, alisema wazi kuwa kwa jinsi CCm ilipofikia pabaya, na nguvu ya Upinzani kukua, kuna hatari ya CCM kung'olewa.
- Mh. Njelu Kassaka; ameshasema na kurudia mara kadhaa kuwa Mwaka huu CCM ipo ktk hatari kubwa ya kuondolewa Madarakani kwa kushindwa kuona nini jamii imekuwa ikikitafuta na sasa Wapinzani wanayo majibu.
- Mh. Rais JK; katika matukio mbalimbali, JK amesisitiza akirudia kuwaambia wanaCCM wenzake kuwa "siwatishi ila ukweli ni kuwa 'Watanzania wa sasa wameamka' na CCM ijiangalie sana" na hivi juzi tu ktk Vikao vya CCM Dodoma, ameongea 'macho makavu' akirudia yaleyale, ...watanzania wa sasa sio wale waliokuwa 'wanaelekezwa' tu kuichagua CCM...kuwa CCM inaweza kuondoka, na ikiondoka hairudi tena, na akatoa mifano ya Vyama vya Ukombozi ktk mataifa kadhaa vimetokweka kabisa baada ya kung'olewa.
- Mh Edward Lowassa (Waziri Mkuu aliyejiuzulu); ambaye sasa ndiye anayeonekana tishio ktk watakaogombea Urais kupitia CCM, Hapo jana tu, amesema yale yale Rais JK aliyosema majuzi ktk Vikao vya CCM. Lowassa amesema wazi kuwa 'hali sio njema' hata kidogo, kwa Mwenendo wa CCM, na "Upinzania wamejiandaa na Wanajiandaa sana", akasema, "tusipojiangalia vizuri, historia ya CCM itaondoka, tutaondolewa ktk uchaguzi Oktoba" naye akasisitiza na akatoa mifano ya Vyama vya Ukombozi ktk mataifa kadhaa vimetoweka kabisa baada ya kung'olewa! Akaitahadharisha CCM.
- Kauli hizi na nyingine kali za waanzilishi wa CCM, ni ishara ya kuwa 'Malaika wa Ukombozi' anawaangazia na hivyo MKiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva atambue 'maono' haya, alinde HAKI, asiharibu huu Ukombozi.