Nimeambiwa nirithi mke wa kakaangu

Nimeambiwa nirithi mke wa kakaangu

hiden

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2015
Posts
376
Reaction score
691
Habari wana jamvi,

Jana ilikuwa arobaini ya kaka yangu. Kaka alifariki kwa ajali. Kaacha mke na mtoto mwenye miezi 7 wakiume. Walioana mwaka jana.

Mimi ndie nilie mfata broh na ni wa mwisho. Tunatofautiana miaka 3.

Mimi bado sijaoa, na wala sina mchumba zaidi ya mademu ambao sina malengo nao.

Sasa katika kikao cha wazee leo asubuhi, ndio likaja hilo wazo kwamba binti huyu ana mtoto wa miezi 7, hana kazi atakwenda wapi na ataishi wapi? Na pia familia yetu ilimpenda sana na haiko tayari kuja kushuhudia kuolewa na mtu mwingine baki.

Baba ana nyumba mbili Dsm bado alikuwa ajatukabidhi, moja itakuja kuwa yangu, nyingine angepewa kaka, lkn ndo mauti yashamkuta.

Na kiukweli sisi wachaga hatupendi kupoteza mtoto. Ndipo wazee wakaniita na kuniuliza kama nina mchumba, nikawajibu hapana.

Wakanieleza kwa taratibu za mila na desturi za zamani hali kama hii ikitokea ina bidi mdogo mtu arithi jukumu la kaka ili gurudumu liende mbele.

Nilipokuwa namwazia shemeji angu ambae ni mke wa kaka angu jinsi alivyo poa na bado anaita, nikaona sio mbaya kupokezana vijiti.

Kiukweli mimi na shemeji yangu tulikuwa tunaheshimiana sana, kila mara alikuwa anauliza nitaoa lini. Alikuwa kama rafiki yangu, japo sikuwahi waza jambo kama hili laweza kuja tokea.

Wazee wameamua kuwatafuta wa mama wa makamo wamweleze shemeji jambo hili waone msimamo wake.

Kwa upande wangu sina tatizo kabisa, kwani kwa tabia yake, ukarimu, upendo kwa marehemu kaka, namuona ni mke mwema ambae naweza ishi nae.

Nasubiria kikao cha Akina mama na shemeji juu ya maamuzi yake.

Vipi wadau, kwa huko kwenu huu utaratibu upo?
Kwa wewe binafsi unaichukuliaje?
 
Vizuri umekubali bila wasi
Kwa kabila langu.. siyajui kama yapo au hayapo.

Tunasubiria uje utupe mrejesho.. kwa ku update post yako ya kwanza
 
Habari wana jamvi,

Jana ilikuwa arobaini ya kaka yangu. Kaka alifariki kwa ajali. Kaacha mke na mtoto mwenye miezi 7 wakiume. Walioana mwaka jana.

Mimi ndie nilie mfata broh na ni wa mwisho. Tunatofautiana miaka 3.

Mimi bado sijaoa, na wala sina mchumba zaidi ya mademu ambao sina malengo nao.

Sasa katika kikao cha wazee leo asubuhi, ndio likaja hilo wazo kwamba binti huyu ana mtoto wa miezi 7, hana kazi atakwenda wapi nanataishi wapi? Na pia familia yetu ilimpenda sana na haiko tayari kuja kuolewa na mtu mwingine baki.

Baba ana nyumba mbili Dsm bado alikuwa ajatukabidhi, moja itakuja kuwa yangu, nyingine angepewa kaka, lkn ndo mauti yashamkuta.

Na kiukweli sisi wachaga hatupendi kupoteza mtoto. Ndipo wazee wakaniita na kuniuliza kama nina mchumba, nikawajibu hapana.

Wakanieleza kwa taratibu za mila na desturi za zamani hali kama hii ikitokea ina bidi mdogo mtu arithi jukumu la kaka ili gurudumu liende mbele.

Nilipokuwa namwazia shemeji angu ambae ni mke wa kaka angu jinsi alivyo poa na bado anaita, nikaona sio mbaya kupokezana vijiti.

Kiukweli mimi na shemeji yangu tulikuwa tunaheshimiana sana, kila mara alikuwa anauliza nitaoa lini. Alikuwa kama rafiki yangu, japo sikuwahi waza jambo kama hili laweza kuja tokea.

Wazee wameamua kuwatafuta wa mama wa makamo wamweleze shemeji jambo hili waone msimamo wake.

Kwa upande wangu sina tatizo kabisa, kwani kwa tabia yake, ukarimu, upendo kwa marehemu kaka, namuona ni mke mwema ambae naweza ishi nae.

Nasubiria kikao cha Akina mama na shemeji juu ya maamuzi yake.

Vipi wadau, kwa huko kwenu huu utaratibu upo?
Kwa wewe binafsi unaichukuliaje?

Je, atakupenda?
 
Rithi tu maana hata wewe unamaidi
 
Kumbe mambo ya kurithi mke bado yapo! Hongera, ila mimi hapana
 
Vizuri umekubali bila wasi
Kwa kabila langu.. siyajui kama yapo au hayapo.

Tunasubiria uje utupe mrejesho.. kwa ku update post yako ya kwanza
Mkuu haina shida kwa mtazamo wako?
 
Ndio nasubiri kusikia atawajibu vipi akina mama.

Japo hakuwahi nishuhudia na tabia zangu za kihuni, nilikuwa namficha sana.

Kiufupi hatujawahi gombana, nilikuwa nikija kwa broh lazima nilete mapochopocho.
Aliniambia nitakuja kuwa baba mzuri
Hapo mwisho tu Jibu ni kuwa KESHAKUBALI we jiandae kurithi majukumu
 
Back
Top Bottom