Nilizaa nje ya ndoa, nitahalalishaje hili suala?

Nilizaa nje ya ndoa, nitahalalishaje hili suala?

usungilo

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2012
Posts
522
Reaction score
332
Habari ndugu zangu,

Poleni na majukumu ya kila siku.Nahitaji ushauri wenu ni muhimu.

Tukiwa kwenye uchumba na huyu mke wangu kuna kitu kilijitokeza mpaka nikafanya yaliyotokea.Ni miaka miwili imepita sasa tangu tukio litokee ila hata ndugu zangu hawajui. Huyu mke wangu alikuwa anataka kubeba mimba kabla hatujakamilisha taratibu zote hiyo kunilazimu na mimi nikubaliane naye.

Nilimwambia haina uharaka lakini yeye akawa anasisitiza tulijaribu mara kadhaa bila mafanikio mpaka akaanza kujihisi ana matatizo na akawa na wasiwasi hii ilinitia hofu na mimi kuwa yawezekana nina matatizo kwani sikuwahi kumpa ujauzito binti yeyote katika mapito yangu.

Ilinibidi nichepuke na binti mmoja kwa kumvizia mpaka siku zake za hatari na akapata ujauzito. hapo nikawa na uhakika kidogo niko fit huyu mwenzangu nikaendelea kumsisitizia kuwa kuna vitu Mungu ndie anapanga aafu ili ijulikane una tatizo kuna muda ambao ni lazima uwe umepita mkishirikiana na jamaa yako.

Mtoto alipozaliwa anafanana nami ila nilimwambia mama yake anilindie ndoa yangu na kaweka siri.Nimeoa niko na huyu mke wangu na ana mtoto sasa hivi na tunaishi kwa amani yule mtoto mwingine namlea kwa siri sana kwani namtumia tu matumizi mama yake na tunaishi mbali mbali.

Nataka ifike kipindi niweke mambo wazi kwani sitapenda iendelee kuwa siri mke wangu nampenda sana, naogopa ataumia sana ni presha zake ndio zilinitia hofu na mimi mpaka yakatokea yaliyotokea nitaanzaje kulihalalisha hili suala?

Naombeni mawazo yenu

Habari ndugu zangu,

asante mkuu. ngoja niwasubiri maana naumiza kichwa sana.
 
Mkuu mwambie ukweli kama uliosema hapa kuwa ulienda kujaribisha kama uko fit baada ya yeye mwenyewe kukutia wasiwasi, aaah sipati picha hivyo reaction yake!! ila ndo ukweli wenyewe kwa mujibu wa maelezo yako.

Hahaaa hizi ndoa zina vituko jamani loh!!
 
Ukimwambia na yeye atatafta wa nje ili ngoma iwe droo. Hata ka ningekua Mimi usitegemee huyo mtoto mkeo ampende.
 
yani iliujue kama uko functional badala ya kwenda hospitali kupima vipimo vya bei ila bila madhara ya baadae ukaona uchukue the other more expensive alternative, expensive cz sasa uko kwnye matatizo..na mkeo ataumia kweli, uaminifu kwish-neh, ila mwambie mgombane yaishe kuliko kwa bahati mbaya asikie kwa wengne au siku ukaaga dunia ndio mama mtu anajitokeza, hataelewa na ataumia mara tatu zaidi
 
Mkuu sasa tungeenda kupima ili iweje.?
mimi nilikuwa naamini tupo vizuri ila mwenzangu akawa ananitia stress nikaingiwa na wasi wasi mpaka nikadhamiria kujaribu kwingine.
ndio naomba ushauri namna ya kumuingia ili anielewe
 
Ukimwambia na yeye atatafta wa nje ili ngoma iwe droo. Hata ka ningekua Mimi usitegemee huyo mtoto mkeo ampende.

assume ni wewe ndio umemsababishia jamaa jamba jamba ya kuwa yawezekana hatuzai.
akichepuka utamchukia?
na baadaye inagungulika mko safi bila hata kufanya vipimo vyovyote.
maana aliniandama zaidi ya nusu mwaka
 
Sana tu ka alikua hajiamini siku hizi kuna hospital mngeenda kupima kiroho safi tu. Mjue tatizo huyo Dada alikua kipoozeo chake tu na alidhamiria.
Kwa mkeo huo ni usaliti hata ukimwambia akakubali ujue rohoni hajaamanisha na uaminifu utaisha kabisa. Na huyo mtoto hatakua na amani.
 
Mbona hiyo ipo open tu , mwache mtoto akue kidogo afu badae akifika miaka 5 mchukue , mweleze mkeo huyu ni mtoto

wangu full stop sitaki maswali , ujue sisi wanawake tuna roho ya korosho ila wee kuwa mbishi ni mtoto wako there is no

way utamkwepa DNA content zako na huyo dogo. mwambie live tu japo ataumia
 
mkuu sasa tungeenda kupima ili iweje.?
mimi nilikuwa naamini tupo vizuri ila mwenzangu akawa ananitia stress nikaingiwa na wasi wasi mpaka nikadhamiria kujaribu kwingine.
ndio naomba ushauri namna ya kumuingia ili anielewe

ungeenda kupima mwenywe sio wote wawili, si ulikuwa na doubts usijeukawa na tatizo? ila ndio hivyo ishatokea...mwambie tu, sasa utaweka siri mpaka lini? siri itakukondesha, kaeni chumbani muongee
 
mbona hiyo ipo open tu , mwache mtoto akue kidogo afu badae akifika miaka 5 mchukue , mweleze mkeo huyu ni mtoto

wangu full stop sitaki maswali , ujue sisi wanawake tuna roho ya korosho ila wee kuwa mbishi ni mtoto wako there is no

way utamkwepa DNA content zako na huyo dogo. mwambie live tu japo ataumia

duh!! umeongea mkavu kweli.
ukiwa ni wewe utakubali?
 
Sana tu ka alikua hajiamini siku hizi kuna hospital mngeenda kupima kiroho safi tu. Mjue tatizo huyo Dada alikua kipoozeo chake tu na alidhamiria.
Kwa mkeo huo ni usaliti hata ukimwambia akakubali ujue rohoni hajaamanisha na uaminifu utaisha kabisa. Na huyo mtoto hatakua na amani.

Nilikuwa namueleza kuwa mimi najua tuko vizuri wote ila yeye ndio akawa hajiamini.
akawa na wasiwasi sana mpaka akanitia hofu.
huyo dada nilikuwa karibu naye tu ila sikuwahi kuchepuka naye.
nilijikuta nachepuka baada ya kufikiria hilo.
tangu ajifungue miaka miwili imepita hatujawahi hata kukumbushia kukutana kimwili tena. huwa namtumia tu hela za matunzo ya mtoto
 
Sana tu ka alikua hajiamini siku hizi kuna hospital mngeenda kupima kiroho safi tu. Mjue tatizo huyo Dada alikua kipoozeo chake tu na alidhamiria.
Kwa mkeo huo ni usaliti hata ukimwambia akakubali ujue rohoni hajaamanisha na uaminifu utaisha kabisa. Na huyo mtoto hatakua na amani.

mhhh...ila siyo wanawake wote wanafanana....!! bila shaka ingekuwa ni wewe kingenuka ile mbayaa...!!!
 
mhhh...ila siyo wanawake wote wanafanana....!! bila shaka ingekuwa ni wewe kingenuka ile mbayaa...!!!
Hahaaaa yani sana tu ile mbaya ndio mkewe anaweza kukubali hata huyo mtoto wakaishi pamoja ila asimpe special care. Mi wanawake nawajua vizuri tu.
 
Hahaaaa yani sana tu ile mbaya ndio mkewe anaweza kukubali hata huyo mtoto wakaishi pamoja ila asimpe special care. Mi wanawake nawajua vizuri tu.

ahaaa kwa namna hii Tz si pakuoa.....!!!! labda michepuko tu.......Diva Beyonce changamkia tenda...natafut mchepuko MMU.
 
Uhuni wako tu....

Kwa nini usingeenda kufanya sperm analysis ili kujua upo fiti????

Jiandae kuharibu ndoa tako......ujue litamuumiza mkeo na things will never be the same again.....
 
Nenda kamwambie kwamba pressure aliyokupa ya wewe kumpa ujauzito ilikutia hofu kwamba labda nawe una matatizo huna uwezo wa kujaza mimba hivyo ulicheza nje na bahati nzuri ukampa mimba huyu binti hivyo kuthibitisha uko fit. Sasa uko tayari kumchukua mtoto na unataka amlee kwa upendo wake wote, ila kuna hatari hili linaweza kabisa kutia dosari kubwa sana katika ndoa yako hivyo inabidi uwe makini sana.
usungilo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom