Baby M
JF-Expert Member
- Apr 18, 2012
- 1,037
- 415
duh!! umeongea mkavu kweli.
ukiwa ni wewe utakubali?
wewe ni muoga, jikaze kama ulivyojikaza kwenda kujaribu nje.. ataumia but better amejua ukweli from you. Period!
duh!! umeongea mkavu kweli.
ukiwa ni wewe utakubali?
Mkuu mwambie ukweli kama uliosema hapa kuwa ulienda kujaribisha kama uko fit baada ya yeye mwenyewe kukutia wasiwasi, aaah sipati picha hivyo reaction yake!! ila ndo ukweli wenyewe kwa mujibu wa maelezo yako.
Hahaaa hizi ndoa zina vituko jamani loh!!
Hahahaaaa! Yaani hizi ndoa jamani!! Hivi kumbe ukihisi unatatizo hutakiwi kwenda hospital ila ni kuchepuka tu!! Ye aseme tu ukweli wote kama alivyoueleza hapa, mengine atajua baada ya kuueleza huo ukweli.
Hayo maumivu atakayoyapa duh roho inaweza kuacha mwili...
We nae utakua umezaa na mume wa mtu na hujaolewa si bure....eti amchukue then hataki maswalI.?? Ndoa haiendi hivyo nikwambie..ni swala la kufikisha ujumbe na kujadiliana..lkn sio ukatili km wako eti full amri khaaa kwani umeahakikishiwa mwanamke atakataa..mumewe akiongea nae kwa ustaarabu ishu itasovika...hujaolewa hujui ndoa ni niniMbona hiyo ipo open tu , mwache mtoto akue kidogo afu badae akifika miaka 5 mchukue , mweleze mkeo huyu ni mtoto
wangu full stop sitaki maswali , ujue sisi wanawake tuna roho ya korosho ila wee kuwa mbishi ni mtoto wako there is no
way utamkwepa DNA content zako na huyo dogo. mwambie live tu japo ataumia
Ushawah kumwambia mkeo ikitokea una mtoto wa nje utampenda?U never know akampenda mwanao ...Wangapi tunawaona wanalelewa vizuri tu.Habari ndugu zangu,
Poleni na majukumu ya kila siku.Nahitaji ushauri wenu ni muhimu.
Tukiwa kwenye uchumba na huyu mke wangu kuna kitu kilijitokeza mpaka nikafanya yaliyotokea.Ni miaka miwili imepita sasa tangu tukio litokee ila hata ndugu zangu hawajui. Huyu mke wangu alikuwa anataka kubeba mimba kabla hatujakamilisha taratibu zote hiyo kunilazimu na mimi nikubaliane naye.
Nilimwambia haina uharaka lakini yeye akawa anasisitiza tulijaribu mara kadhaa bila mafanikio mpaka akaanza kujihisi ana matatizo na akawa na wasiwasi hii ilinitia hofu na mimi kuwa yawezekana nina matatizo kwani sikuwahi kumpa ujauzito binti yeyote katika mapito yangu.
Ilinibidi nichepuke na binti mmoja kwa kumvizia mpaka siku zake za hatari na akapata ujauzito. hapo nikawa na uhakika kidogo niko fit huyu mwenzangu nikaendelea kumsisitizia kuwa kuna vitu Mungu ndie anapanga aafu ili ijulikane una tatizo kuna muda ambao ni lazima uwe umepita mkishirikiana na jamaa yako.
Mtoto alipozaliwa anafanana nami ila nilimwambia mama yake anilindie ndoa yangu na kaweka siri.Nimeoa niko na huyu mke wangu na ana mtoto sasa hivi na tunaishi kwa amani yule mtoto mwingine namlea kwa siri sana kwani namtumia tu matumizi mama yake na tunaishi mbali mbali.
Nataka ifike kipindi niweke mambo wazi kwani sitapenda iendelee kuwa siri mke wangu nampenda sana, naogopa ataumia sana ni presha zake ndio zilinitia hofu na mimi mpaka yakatokea yaliyotokea nitaanzaje kulihalalisha hili suala?
Naombeni mawazo yenu
Habari ndugu zangu,