Inatokea post namba 97.
Sikukaa sana, kabla kiza hakijaingia vijana wa babu wakarudi na kama nyavu za mkono zile zile zina fimbo ndefu kushikia. Wakanambia twende tukavune kamba wa kuchoma. Tukaenda mtoni, tukapita lile dimbwi la kamba, kulikua na kamaba wengi sana, tukalipita tukaenda mbele kidogo, kama kuna kichaka hivi, kukipita, kati kati ya kichaka tukakuta dimbwi lingine kubwa, limefichwa kabisa na kichaka, kama haujui kama lipo pale hulioni. Mmoja akasema "chimbo la babu hili" yeye ndio katuonesha, haingii mtu huku kama hajaoneshwa na babu. Nikamuuliza, mbona mimi hajanionesha? Akajibu si ndio tunakuonesha hivi kwa idhini yake mwenyewe. Mmoja alikua kaja na kapu kubwa, tukaanza kuvuna kamba pale, haikuchukua hata dakika kumi, kapu limejaa. Kamba wakubwa wakubwa , yaani ukiwala wawili au watatu umeshashiba. Tukaondoka pale tukarudi karibu na pangoni, mmoja kaja na kamba, akasema kalete lile bakuli kubwa, akawajaza wengine kwenye bakuli, wengine akashuka nao kwenye bwawa lile la kamba wadogo, akafunga kikapu chake, akakiingiza kwenye bwawa, akasema muda watabaki wazima nahawaribiki hata mwezi, hawatoki kabisa. Nikajisemea moyoni, kweli kila mtu na ujuzi wake.
Tyuliporudi pangoni mmoja akaingia kichakani kuleta kuni za kuchomea kamba, mmoja nikaja nae akatoa kwenye kapu walilokuja nalo, kama bakuli hivi lina rojo nene la viungo vilivyopikwa, vinanukia. Akasema wale tunaowachomaote tuwatie humu wakae nusu-u saaa, maagizo ya bibi, ndio baadae tuwachome, tusiwachome kaba ya kuwaroweka kwene rojo kwa nusu saa. Na wengine kasema tuwachome bila viungo, bali tutachovyea wkati wa kula, kuna vitu vingine hapa bibi kapika, Lakini kasema hii ina pilipili mbichi imesaagiwa, hii ya kupika ina pilipili manga. Haya jamani kwa raha zetu.
Alieenda kuchukua kuni akarudi na rundo la kuni na rundo la majani fulani hivi mabichi, mengi tu. yapo kwenye matawi yake. Akasema haya majani ya babu, akipika nyama choma au samaki choma lazima ayaweke haya kabla nyama hazijawiva zijae moshi wake. Nikayakumbuka. Kweli, hata tukifanya nyama choma nyumbani mjini, baba huwa anayaleta kwa wingi, Nayajua, yanafanya nyama inakua na harufu nzuri na mwenyewe anasema ukiyapondea kwenye nyama haya, dakika kumi tu, hata uwe ni mshipa mgumu vipi utalainika. Nikauliza jina la yale majani, wakanitajia jina la kizigua sijui la Kidigo. wakanambia haya tutakuchumia ukiondoka, pale karibu ya nyumbani kwa babu yapo mengi sana, babu aliyapanda. Haiwi miti mikubwa kama mibaazi ya kusimama tu, ukikuwa sana ni futi sita au saba haizidi hapo.
Basi tukatayarisha kamba wetu huku moto unawaka halafu wakauzima ukabaki mkaa tu unawaka, wakatia majani yale ya kunukia juu, yakawa yanatoa moshi kwa wingi, walikuwa wamechonga na vijiti virefu vingi tu, unawaingiza kamba watatu wanne tu wale wakubwa, mnachoma mnakula hapo hapo, wengine tunaweka kwenye sahani, Mpaka babu akaja, na yeye tukawa tunachoima nae, aknambia bibi yako kanipa haya mandazi ile masala ya kupaka ya kulia kamba. Basi mambo yakawa mazuri pale, ikawa ni kamba kwa wingi, maongezi kidogo. Mandazi makavu ya bibi kwa kamba, yaani wale kamba na zile pilipili za kupika za bibi ilikuwa kiboko, Haijapita muda, babu akasema nitilieni kamba wa bibi yenu, nimpelekee, babu mimi ntarudi baadae. Babu akachukua kamba kwa wingi tu, akasema wanatosha hawa, kama hawatoshi watachoma wa nyumbani, kuna wageni watatu na kazi nao, nikimaliza narudi huku, akondoka na kijana wake mmoja, nikabaki na yule partner wangu wa kila siku. Nikakaa kidogo nikaona imekaribia saa tatu, nikamwambia narudi sasa hivi, nikaelekea mtoni nikanawa, nikaenda kwenye uwanja wa kumuita jini. Kufika nikaanza kuita kama mara mbili tatu, nikakaa kimya nikaita tena nikatoa na salaam, mara nikassikia, aah bwana mkiubea vipi hali yako? Nikaitikia salama, akanambia kaa chini. Nikakaa, akanambia haya umeniita unasemaje? Nikamwambia si ulinambia nije saa tatu, akasema ndio, nataka uniulize maswali yako uliyonayo.
Nikamuuliza, mbona hutaki nikuone, kwanini sauti tu? Akanambia mimi hiuwezi kuniona kwa sasa lakini umeshawahi kuniona sana sema hunijui tu mimi ni nani. Nikamuuliza wewe jini? Akasema mimi ni mtu kama wewe lakini naweza kua chochote kile nipendacho, nikamuuliza kama ni mtu, mbona huonekani? Akanambia hiyo ni elimu tu, na wewe leo si umepewa mizizi ukiila utakua huonekani? Nikamwambia ndio alivyonambia, umejuaje? Akasema si nimekwambia mimi najua mambo yako yote, huweizi kunificha kitu. Nikamwambia sasa nitakula ile mizizi usinione, akanambia ile, kwa yeye hata nikiila atanipona tu, haimzuwii yeye kuniona. Akanambia yeye kutokuonekana hatumii mizizi, anatumia tekbolojia nyingine kabisa, akanambia kuna siku za usoni utaijua. Nikamuuliza nitaijuaje, Akasema mimi nipo hapa kukufundisha mengi usioyajua. Ni lazima nikupe elimu usiyoijua wewe na wasioijua binadam wengine. Nikamwambia watu wanajua mambo mengi utasemaje kuna elimu hawaijui? Akacheka akasema kweli binadam wana elimu tofauti tofauti nyingi sana., lakini kuna ambazo hakuna mwenye nazo dunia nzima, sio binadam sio jini, mimi ninazo. Utaziona tu. Kidogo kidogo, una swali lolote?Sikumjibu. Akasema mimi najua unataka kuuliza nini lakini unaona haya kuuliza. Nikamwabia huwezi kujua nilikua nataka kukuuliza nini, aaknambia nikwambie? Nikamwabia nambie. Akanambia unataka kujua kama naweza kukufundisha kusafiri kwa haraka sana. Nikamwambia umejuaje, akasema hiyo haikuhusu, kwa sasa, sema ni kweli ulitaka kuuliza hivyo? Nikamwambia hilo lilikua moja tu, akasema nafahamu, sasa wewe kaa kimya mimi nakujibu maswali yako bila kuuliza.
Akaanza, ndio, mimi naweza kusafiri kwenda popote duniani kwa muda mfuoi sana, na sio mimi tu, naweza kukuafirisha na wewe na mizigo yako, Hata kama una gari, mimi naweza kukusafirisha wewe na gari lako nikakupeleka popote Tanzania ndani ya dakika tatu au chini kabisa ya hapo. Hapana huo sio uchawi, hio ni elimu tu. Utaijua kidogo kidogo. Halafu dunia haipo duara bwana mkubwa, dunia ni kama zulia lililotandikwa. Mnadanganywa na wasomi wenu, wanafahamu hilo, lakini hawataki kua wa kweli. Kuna mengi sana wanayaficha kwa faida zao, na mengine ukiyajua watakuua. Ndio zipo dunia saba. Na zote zina viumbe wake.
Nikawa nashangaa, hayo yote nilikua nataka kumuuliza, yeye anajibu kabla sijamuuliza, Nikamwabia unanitisha. Akasema kwanini? nikamwambia unajuaje ninachotaka kukuuliza, Akasema hio ni elimu ya "telepathy", hivo hivo kwa Kinegreza. Akasema ni mawasiliano tu ya hali ya juu, utayajua tu, akasema hizi simu zenu za siku hizi, miaka 100 nyuma ungemwambia mtu zinavyofanya kazi angekuona mchawi, mtu yupo London mnaonana na mnaongea wakati huohuo. Sasa teknolojia imepungua, zamani ilikua kubwa sana, mimi naifahamu, nimebahatika kuwepo zamani na sasa hivi. Kwa hio ninayo teknolojia iliofichwa, wakikujua na wewe unaijua wanakuua, hawakuachi. Maadui ni wengi sana, hawataki uwazidi kitu. Mimi hawawezi kuniua, najua mbinu zao zote, wamejaribu sana wameshindwa, sasa wananiogopa sana.
Nikawa nashangaa shangaa akanambia, nadhani umeelewa machachelakini hayakuingii akilini. Kila tukikutana uwe unauliza uyatakayo, chukulia hii kama mwanzo tu. Nikamuuliza naweza kuja kukurikodi? Akasema unaweza kuja kunirekodi na chochote na utaweza kurikodi sauti, picha yangu huwezi kuipata labda nitake mwenyewe. Mikamwambia natamani sana nikuone, unaonesha una hekima nyingi, Akasema kawaida tu, nikija siku nyingine nitakufundisha kuhusu dunia saba zilizopo, lakini nawea kukufundisha kuhusu nne tu, ya tano, sita na saba, siwezi. Nikawa nawaza tu. Tukaagana kabla hajaondoka nikamwambia sasa ndio yamenijia maswali mengi sana, akasema anajua lakini vizurini uwe na maswali yasiozidi matatu ili anifahamishe kwa kina na niwe na rikodi. Tukaagana akaondoka.
Nikarudi pangoni, nikamkuta kijana wa babu bado anachoma kamba pale karibia na lango la pangoni. akanambia nimekula kamba mpaka mdomo unawasha, nimeona niwamalizie kuwachoma hawa kwenye bakuli, tutawala tukisikia njaa usiku au tukiamka kusali alfajiri. Nikamwambia poa. Nikachukua kamba nikaanza kuwala, nikala watatu nikajisikia nipo full kabisa. Nikamwambia babu alisema atakuja lakini mimi nasikia usingizi wa shibe, akanambia hata mimi naosha vyombo halagu nalala, nikamsaidia tukaosha vyombo tukaufukia moto na michanga akasema huu hauzimiki, tutaukuta mpaka asubuhi unawaka ndani ya mchanga, akachomeka vijiti vya kuni kuuzunguka alipoufukia moto, akasema vibwengo baharini vinapenda kufanya utundu, hivi nimezuwia visiuchezee moto. Nikacheka, nikamwambi hawa vibwengo nasikia tu sijawaona, akasema wapo wengi huku lalini haya mapango hawayasogelei, babu anasema kuna viumbe vikali sana humu mapangoni. Vibwengo watauliwa wakifanya mchezo, nikacheka. Nikasema babu ana mikwara ya kizamani. Kijana wake akacheka, akasema babu yako mtaalamu yule, Usimchezee, Tanga nzima hii na Mombasa yake wakishindwa mgonjwa wanamletea yeye. anamtibu. Anajua sana tiba. Nikacheka nikamwambia mimi nalala akija ataniamsha. Akasema babu yako, hana tabia ya kumwamsha mtu akilala. Anaweza kukuacha ulale hata siku mbili hakuamshi. ukimuuliza kwanini hupendi kumuamsha mtu anasema mwache anakua dunia nyingine pale. Utamkatiza raha za ndoto zake.
Itaendelea.
Simba.