Niliyoyakuta Keko

Niliyoyakuta Keko

Hueleweki...

Kwahiyo kushibisha tumbo la mtu (kumpatia pesa ya chakula) hujamsaidia hapo?
Umeelewa ila unakaza tu shingo na hii ni shida Watanzania tunayo hatusomi kuelewa tunasoma kubishana.

Nimesema ”haimsaidii zaidi ya kushibisha tumbo lake” kwamba baada ya kuila na kuisha haipo tena kwenye mikono yake ila ukimpa million akaenda kununua shamba utakuwa msaada endelevu,wapo watu kumpa mtu hata Tsh 500/=  yao wanaona kama wanampa million.

NB:Hii ni kwa mujibu wa uelewa wangu binadamu tumetofautiana ufahamu!!!
 
Kashibishe wenye njaa, hapo Mungu wa kweli atakuongezea. Achana kushibisha matumbo ya watu, mwishowe yatapasuka, angalia walivyotuna kwenye picha. Eti mpe Mungu sehemu ya kumi.
 
Siku ile yule mdada kumbe alipewa noti bandia kwani alirudi na kuanza kuuliza kama kuna mtu anamfahamu.
Acha bhana, kwa mwonekano wa jamaa sidhani kama anaweza kufanya matendo ya uchungu kama hayo [emoji3]
 
Nikajua itaishia amemnyandua kimasihara. [emoji2][emoji2][emoji2]
[emoji3] Kuna muda wanawake wanasongwa na maisha hata ile hamu ya kuwanyadua unakosa, unamwona kama dada au mama yako.
 
Stori zisizoishia na happy ending uwe unakaa nazo tuu...

Nilidhani labda jamaa alimkunja ukiwa unaona live, na kavideo ungetutumia😂
 
Japokuwa umeichagiza hii habari kama kianzio ili watu washawishike kusoma tangazo lako la biashara,ni vizuri binadamu kusaidiana.

Inasemwa unapomsaidia mtu kama huyo wala hela utakayompa hataijengea nyumba au kununulia gari ila utakuwa umempunguzia maumivu na kumfariji wakati akisubiri mafanikio yake kesho na hii ni sadaka ambayo Mungu anaiona moja kwa moja,hata humu JF wapo watu wanafungua mada wakiwa ktk shida kama mtu una uwezo saidia tu 5K yako utakayompa haimsaidii zaidi ya kushibisha tumbo lake tu.

Wakati mwengine unakuta mlemavu wa macho anatembeza viberiti (nilimkuta K/koo) au mama mtu mzima anauza vitu kama limao au tangawizi (nilimkuta mmoja makutano ya Msimbazi &Twiga anakuwepo asubuhi) msaidie wala bidhaa yake usiichukue maana amejaribu kutokuomba akaona afanye kitu ili kuishi ukimsaidia umemfariji sana.

usiache kuchukua bidhaa anayouza,hii kisaikolojia itamjenga zaidi.

mfano umekuta dogo wa kike anauza mboga kachoka kachafuka na zimeshanyauka kwa kupigwa jua.

wewe toa ten au tano agiza fungu 2 mwachie chenji sepa kawape hata ng'ombe wako nyumbani au kuku,hii itamjenga kwamba hata msaada wenye heshima huambatana na masharti yenye utu ndani yake na hasa hakuna kitu cha bure duniani.
 
Unakuta mtu ananunua anashiriki baraka za ujenzi kwa laki tano alafu hajawai toa hata senti kwa omba omba au hata kumlipia nauli mwanafunzi😅 na anavimba yeye mtakatifu
 
Back
Top Bottom