Niliyechaguliwa na wazazi simtaki.

Niliyechaguliwa na wazazi simtaki.

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,933
Reaction score
11,865
Nimezaliwa mkoa wa mara miaka kadhaa iliyopita katika familia ya watoto 6 watoto 4 wa kwanza ni wakike huku wavulana tukiwa 2 na mimi ndo mkubwa, Nikiwa darasa la 6 dada zangu wawili waliolewa na kutolewa mahari ng'ombe 10 kila mmoja hivyo jumla 20.
 
Kulingana na hali ya wizi wa ng'ombe wazazi wangu waliamua kunioza nikiwa std 7 kwa kisingizio kuwa wale ng'ombe wasije wakaibiwa, binti walieniozesha alikuwa ni mkubwa kidogo kwangu na kulingana na udogo wangu walitutenganisha ili nikue kwanza.
 
Kitendo hicho kilimkasirisha mjomba wangu na kuamua kunichukua kwenda kwake Tabora ambapo nilianza kidato cha 1 hadi 4 bila kurudi nyumbani mara baada ya kumaliza wazazi wangu waliniita nyumbani, nilipofika nilimkuta yule mwanamke yupo bado.
 
Kwa taratibu za Mara huyo ni mkeo tu, hata ungemkuta amezaa pia watoto wangekuwa wako.
 
Mweh Mweh Mweh... Kweli jamii forum ni zaidi ya social network..

Naona kimekuwa kijiwe cha vituko
 
hebu malizia kwanza hlafu nikwambie jambo.

khaaa! mie mambo ya mara sina hamu nayo manake nyumba ntobhi ni huko huko
 
Kitendo hicho kilimkasirisha mjomba wangu na kuamua kunichukua kwenda kwake Tabora ambapo nilianza kidato cha 1 hadi 4 bila kurudi nyumbani mara baada ya kumaliza wazazi wangu waliniita nyumbani, nilipofika nilimkuta yule mwanamke yupo bado.
huyo mwanamke analipa?
Boobs , kafungasha etc? Wazazi wako bado wapo? Na hio mahari unaweza kuwalipa wazazi wako?
 
Baada ya kufika nilikabidhiwa yule mwanamke rasmi nikawa nalala nae, baada ya wiki 2 mjomba aliniamuru kurudi Tabora kuendelea na tuition ya kidato cha 5 kwani uwezo wangu darasani ulikuwa mzuri na mjomba alijua nitafaulu tu nikaamua kurudi Tabora
 
Baada ya muda matokeo yaliyotoka nikiwa nimefaulu, nilichaguliwa kwenda A-level kuendelea masomo na baada ya kuhitimu nilifaulu tena kwenda chuo kikuu ambapo hivi sasa nimemaliza tangia mwaka jana na nimepata kazi kinachonichanganya sasa ni kwamba
 
Nikiwa mwaka wa 2 chuoni kuna binti tulikutana nae tukatokea kupendana sana na mpaka sasa hivi tuko nae kanisaidia mambo mengi sana ila sijamwambia kuhusu hili swala na kule nyumbani yule mwanamke bado yupo na kibaya zaidi anataka kuja mjini.
 
ndo mana nilisema malizia kwanza ndipo nikupe ushauri
 
Nikiwa mwaka wa 2 chuoni kuna binti tulikutana nae tukatokea kupendana sana na mpaka sasa hivi tuko nae kanisaidia mambo mengi sana ila sijamwambia kuhusu hili swala na kule nyumbani yule mwanamke bado yupo na kibaya zaidi anataka kuja mjini.
Anakuja mjini kwa nani? Mnawasiliana?
 
Kibaya zaidi yeye amekuwa mkubwa sana kiasi kwamba hata nikiwaambia watu ni mamangu watakubali nimeshindwa nifanye nini kumueleza huyu ukweli nashindwa kwa sababu naona nitampoteza nifanyeje nifaidi chaguo langu si lile la wazazi?
 
Kama ulivyo tueleza hapa tumekuelewa. Bila shaka ukifanya the same kwa mpenzi wako atakuelewa bila shaka.
Kwa mda ambao hampo pamoja na mke wako wa mara. Bila shaka kuna mtu kule atakuwa anamtimizia haja zake. Wewe mwambie asije mjini kwa mda huu. Mwambie bado unajipanga ili kumpanga vyema mpenzi wako.
Mengine nawaachia wajuzi wa jukwaa hili wakuhabarishe
 
Back
Top Bottom