Niliwalaumu Uhamiaji bila sababu kuhusu utoaji Pasi za Kusafiria kutotegemea taarifa za NIDA. Aliyevuruga mfumo yupo, 20% wenye ID si watanzania

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Leo nikiwa hapa Russia nimepata kuongea na Afisa uhamiaji ambaye amesema taarifa anazotoa ni nyeti na wala serikali isingependa zijulikane kwa raia wake maana zitaonesha Udhaifu wake.

Tumejadili yafuatayo:

1. Kwanini ukienda Uhamiaji unaombwa Birth Certificate wakati umeshai submit kwenye NIDA application ya ID?

Kanipa maelezo ambayo nimeridhika

Maelezo yake:

"Kazi inayofanywa na NIDA kimsingi ilipaswa kufanywa na uhamiaji Tanzania, maana watu wengi sasa wana national ID ambao kiukweli si watanzania, pia ndio maana hatuziamini sana Taarifa za NIDA ndo maana tunajiridhisha, kimsing suala hili limefanywa kisiasa"

Akaendelea...

"Siku hizi ukienda kufungua akaunt NMB hakuna haja tena ya kubeba makaratasi ya Serikali za Mitaa wala vitambulisho, cha msingi ni NIN yaani ID number ambayo wanaweka kwenye Portal inayowalink na NIDA kupata taarifa zako, lakini hiyo inakuwa haina madhara sana kwa NMB, kuliko sisi kutumia Portal hiyo tutawapa wasiopaswa pass, inabidi zoezi hili la NIDA lifanywe na Uhamiaji"

Akamalizia kwamba:

"Hata serikali ukiwauliza watakupa sababu zisizo za msingi juu ya hili, lakini ukweli ni kwamba hatuziamini sana taarifa za NIDA maana wakimbizi wengi wanazo hizo ID"
 
Bado tuko nyuma sana.Ilipaswa system zote ziwe integrated na zina ongea zenyewe.Yaani kuzaliwa ,kufa ,kusoma,kazi ,kulipa kodi ,leseni nk.Kwa sasa naona kila mtu anajaribu kufanya vya kwake.Nchi nyingi zilizoendelea hicho kitu wamekiweza ,nilikuwa naangalilia US immigration information wametoa data za kwa nini population growth slowed down.Web site yao ni USAFacts | Non-partisan Government Data .Yaani wanachukua watu waliozaliwa toa waliokufa ,wanaangalia na walioingia hawakutoka wanajua kabisa growth ya pppulation yao.Sisi mpaka tuombe hela ya sensa
 
Mbona mimi nimehakikiwa na uhamiaji kabla ya nida kuprocess FORM. Sasa kama na wenyewe hawaamiani hawana sababu kuwepo
Uko sahihi mkuu. Mimi nilikuwa na passport za zamani. Walipotangaza kuwa tubadilishe kupata hizi za kieletroniki nilijua data zangu wanazo maana ni wao ndo walitupa za zamani. Cha ajabu process ilifanyika kama vile sijawahi kuwa na passport kabisa. Kimsingi na wao hawana tofauti na hao NIDA wanaowatuhumu kuhusu data.
 
Hata uhamiaji hawapaswi kufanya kazi hiyo bali ilipaswa mtoto anapozaliwa tu imediately anaingizwa kwenye system hivyo kila mahali anapokwenda taarifa zile zinatumika
Sasa ukiangalia mamlaka zote za serikali zinategemea taarifa kwako wewe muombaji sasa hapo unategemea nini lazima taarifa zitofautiane
Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani wewe mkuu ungekuwa huku Lingusenguse ningekupa HIGH FIVE,mfumo wetu umeoza na unatoa mafunza na unanuka mno;hapa ilitakiwa hii wizara ya mambo ya ndani ivunjwe na utengeneze wizara mbili,POLISI na MAMBO YA NDANI(hawa ndio watakuwa custodian wa population register ya nchi),motto akizaliwa tu kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani anakuwa na birth certificate yake yenye ID NIMBER(HII ITAKUA NAYO NA KUFA NAYO),sasa linapokuja kwa motto huyu kuomba ID tayari informations zote zimo ndani ya systems na atakapoamua kuomba passport anakwenda na ID book,card only!!
 
Umeongea point ila tatizo linakuja sio kila mtoto anazaliwa Hospitali wengine wanazaliwa kwa wakunga wa jadi ikiwemo kwa WAGANGA WA KIENYEJI
Hata uhamiaji hawapaswi kufanya kazi hiyo bali ilipaswa mtoto anapozaliwa tu imediately anaingizwa kwenye system hivyo kila mahali anapokwenda taarifa zile zinatumika
Sasa ukiangalia mamlaka zote za serikali zinategemea taarifa kwako wewe muombaji sasa hapo unategemea nini lazima taarifa zitofautiane
Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani wanachukua watu waliozaliwa toa waliokufa ,wanaangalia na walioingia hawakutoka wanajua kabisa growth ya pppulation yao.Sisi mpaka tuombe hela ya sensa
Lakini si hata wao bado wanafanya sensa; kwani hawafanyi?
Kila kitu kina sababu zake mbalimbali hata kama kuna hiyo 'integration' kati ya taasisi unayoisema.

Lakini naona katika kusoma taarifa hiyo kwenye 'website' uliyoweka hapo, baadhi ya uliyoeleza kwenye andiko lako sio sahihi. Yaani umetia jumvi!
 
Back
Top Bottom