Niliwalaumu Uhamiaji bila sababu kuhusu utoaji Pasi za Kusafiria kutotegemea taarifa za NIDA. Aliyevuruga mfumo yupo, 20% wenye ID si watanzania

britanicca,

Mheshimiwa Britanicca, hata huko uhamiaji pia bado hawatumii data za kweli. kwa sababu unaenda kuomba passport wanakuambia ulete cheti cha kuzaliwa cha baba au mama yako. baba alizaliwa 1937 au 1940. mimi sikuwepo alipozaliwa lakini wanakuambia utakipata hapa hapa. unajaziwa form na kuambiwa ukalipie stempu ya ushuru. huyo anayekudhamini kuwa alimwona baba yako akizaliwa unakuta ana miaka 20 alimwona wapi baba yangu? wonders will never end in this unforgetable Tanzania
 
Umbea na uongo wa dhahiri, Eti umeambiwa na afisa uhamiaji, usichojua kule Nida ni lazima uhojiwe na uhamiaji na ndie anaesign upate kitambulisho..
Mleta mada acha uzandiki

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa ana exaggerate, 20 % siyo mchezo ..... yaani anamaanisha kuwa kama vitambulisho vimeshatolewa 10 million mpaka sasa ina maana kuwa 2 million siyo Watanzania. Kama ni 20 million, 4 million waliopewa siyo Watanzania. Sasa kwa hiyo hesabu anatakakutuambia kuwa Tanzania ina wageni kiasi gani?

Yaani ukijaribu ku extrapolate hiyo namba anayoisema ina maana, kwa hesabu tunayoambiwa kuwa tuko 55 million ina maana kuwa kuna Wageni kama 11 million .....!!
 
Kiukweli Tanzania ni nchi maskini sana, ingawa kuna watu wanajidai hawalioni hilo.
Ishu ni ndogo sana, tunatakiwa kuwa na mfumo ambao ni rafiki kwa kazi za kijamii. Kila hospitali, zahanati, na vituo vya afya kunatakiwa kuwe na " Electronic Data Machine" ambapo mtoto akizaliwa, majina matatu, tarehe ya kuzaliwa, jinsia, majina ya wazazi wote wawili, na vingine vya muhimu vinajazwa na kutumwa kwenye Data Base ya msajili wa vizazi na vifo. Vivo hivyo mtu akifariki dunia.
Sasa kwetu hapa mtu anakuwa na majina tofauti kila atakavyo kwa sababu hatuna kinu cha kutunzia taarifa zetu.
Kama tungekuwa katika mfumo huo maana yake wakristu wangebatizwa majina waliyopewa wakati wa
kuzaliwa. Kila dakika, saa, na sekunde, idadi ya watu wanaozaliwa ingeendelea kujumlishwa kwenye kinu /kibubu cha taarifa.
Kutegemea sensa ya miaka kumi ni kudanganyana idadi ya watu.
Huduma za kijamii tunashindwa kuzipanga na kizisimamia sababu hatujui idadi ya watu kwa mahali patakiwapo huduma.
Yaani wewe mkuu ungekuwa huku Lingusenguse ningekupa HIGH FIVE,mfumo wetu umeoza na unatoa mafunza na unanuka mno;hapa ilitakiwa hii wizara ya mambo ya ndani ivunjwe na utengeneze wizara mbili,POLISI na MAMBO YA NDANI(hawa ndio watakuwa custodian wa population register ya nchi),motto akizaliwa tu kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani anakuwa na birth certificate yake yenye ID NIMBER(HII ITAKUA NAYO NA KUFA NAYO),sasa linapokuja kwa motto huyu kuomba ID tayari informations zote zimo ndani ya systems na atakapoamua kuomba passport anakwenda na ID book,card only!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
britanicca, Watanzania halisi ni kina nani? Mbona tunahangaika sana na mambo ambayo kimsingi hayana majibu rahisi kama wengi mnavyotaka. nasikia Bukoba ndio worse. karibu wote sio watanzania. What about that?
 
Unalosema kweli kapendekeza kuwa mtoto anapaswa kupewa ID anapozaliwa, pia ni vema ku review upya hizi taarifa za BC
Marekani wana ID za aina mbili, kuna ya mtoto mdogo kuanzia akiwa ana sikumoja tokea kuzaliwa hadi akiwa na miaka kumi na saba. Akifikisha miaka kumi na nane ambapo anahesabiwa ni mtu mzima then anapewa ya mtu mzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado tuko nyuma sana.Ilipaswa system zote ziwe integrated na zina ongea zenyewe.Yaani kuzaliwa ,kufa ,kusoma,kazi ,kulipa kodi ,leseni nk.Kwa sasa naona kila mtu anajaribu kufanya vya kwake.Nchi nyingi zilizoendelea hicho kitu wamekiweza ,nilikuwa naangalilia US immigration information wametoa data za kwa nini population growth slowed down.Web site yao ni USAFacts | Non-partisan Government Data .Yaani wanachukua watu waliozaliwa toa waliokufa ,wanaangalia na walioingia hawakutoka wanajua kabisa growth ya pppulation yao.Sisi mpaka tuombe hela ya sensa
Kuna watu ambao wana maslahi yao mfumo ukiwa umetawanyika hivi, kwao kuunganisha hivyo inawaharibia ulaji wao.

Ila very soon wananchi tutakapo anza kuwashikia mafagio viongozi wafanye kazi kwa adabu ndipo tutasikilizana vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli Tanzania ni nchi maskini sana, ingawa kuna watu wanajidai hawalioni hilo.
Ishu ni ndogo sana, tunatakiwa kuwa na mfumo ambao ni rafiki kwa kazi za kijamii. Kila hospitali, zahanati, na vituo vya afya kunatakiwa kuwe na " Electronic Data Machine" ambapo mtoto akizaliwa, majina matatu, tarehe ya kuzaliwa, jinsia, majina ya wazazi wote wawili, na vingine vya muhimu vinajazwa na kutumwa kwenye Data Base ya msajili wa vizazi na vifo. Vivo hivyo mtu akifariki dunia.
Sasa kwetu hapa mtu anakuwa na majina tofauti kila atakavyo kwa sababu hatuna kinu cha kutunzia taarifa zetu.
Kama tungekuwa katika mfumo huo maana yake wakristu wangebatizwa majina waliyopewa wakati wa
kuzaliwa. Kila dakika, saa, na sekunde, idadi ya watu wanaozaliwa ingeendelea kujumlishwa kwenye kinu /kibubu cha taarifa.
Kutegemea sensa ya miaka kumi ni kudanganyana idadi ya watu.
Huduma za kijamii tunashindwa kuzipanga na kizisimamia sababu hatujui idadi ya watu kwa mahali patakiwapo huduma.

Sent using Jamii Forums mobile app
safi mkuu but hii sio rocket science,why hawa wanasiasa wetu hawafanyi hili?wenzetu kila unakokwenda kitu cha kwanza unaulizwa ID book ,kama huna tayari huduma zao kwako zishaingia walakini kuanzia vituo vya polisi,Mabank,mahospitali,maduka ya kukupesha lazima uwe na ID book ,kwetu sisi ninagonga mtu mtwara,ninakimbilia lingusenguse na kubadilisha majina na maisha yanaendelea!!.
 
Acheni ujinga wa kukimbilia kutoa lawama...
Katika usajili wa NIDA.. uhamiaji walikuwa na verification section yao...
Haya mengine ni kutaka tu kujimwambafy... Na ni mwendelezo ule ule wa idara na taasisi za serikali kufanya kazi kwa kujitenga tenga..!
Imefanyiwa na NIDA au Uhamiaji au whatever-the-name bado ni hiyo serikali moja inatoa vitambulisho au vibali kwa watu wake..!!
We definitely need to sit down and correct ourselves.. Tunajichoresha sana...!!
Shame on us all!
 
Mbona tunao ishi nje ya nchi tumeweza kubadili passport bila ya nida?
Nadhani utaratibu wa nida ulikuwa uwendane na passport, kama huna nida unaomba passport wakuletee pamoja hio nida na passport
Kutokana na usumbufu usio wa lazima, walio nje walisamehewa kuwa na kitambulisho cha NIDA, ndiyo maana ubalozi wanaomba ID/DL ya sehemu muhusika.
Bado kuna mambo uhamiaji wata beba lawama. Kwanini hata wenye pass za zamani lazima watoe shahada za wazazi... Nk. Kwani hawana data base ya watu ambao wana wapatia pass??
Sababu ni kuwa zamani pasi nyingi zilipatikana kiudanganyifu, hivyo uhakiki inabidi ufanyike upya.
Marekani wana ID za aina mbili, kuna ya mtoto mdogo kuanzia akiwa ana sikumoja tokea kuzaliwa hadi akiwa na miaka kumi na saba. Akifikisha miaka kumi na nane ambapo anahesabiwa ni mtu mzima then anapewa ya mtu mzima.
Hakuna kitu kama hicho.
 
Sasa hizo basic information ,ndio everything kwa taarifa yako hapa imetushida nini?kama cheti cha kuzaliwa lazima uzunguke nacho kwenye hizo idara zote
Wewe uliandika "everything", ndio maana nikakujibu nilivyojibu. Huoni kuwa kuna tofauti ya "everything" na "basic information"?
 
Acheni ujinga wa kukimbilia kutoa lawama...
Katika usajili wa NIDA.. uhamiaji walikuwa na verification section yao...
Haya mengine ni kutaka tu kujimwambafy... Na ni mwendelezo ule ule wa idara na taasisi za serikali kufanya kazi kwa kujitenga tenga..!
Imefanyiwa na NIDA au Uhamiaji au whatever-the-name bado ni hiyo serikali moja inatoa vitambulisho au vibali kwa watu wake..!!
We definitely need to sit down and correct ourselves.. Tunajichoresha sana...!!
Shame on us all!
Wwatu wengi nawajua hakuna cha Uhamiaji wala nini waliitwa jumapili usiku na kujaza form upande wa mbele, na ule wenye saini na masuala ya serikali za mtaa na kata wakascan ya ambaye alishajaza lakin wakafuta saini na ye akasaini zake, aisee chunguza
 
Leo nikiwa hapa Russia nimepata kuongea na Afisa uhamiaji ambaye amesema taarifa anazotoa ni nyeti na wala serikali isingependa zijulikane kwa raia wake maana zitaonesha Udhaifu wake.

Tumejadili yafuatayo:

1. Kwanini ukienda Uhamiaji unaombwa Birth Certificate wakati umeshai submit kwenye NIDA application ya ID?

Kanipa maelezo ambayo nimeridhika

Maelezo yake:

"Kazi inayofanywa na NIDA kimsingi ilipaswa kufanywa na uhamiaji Tanzania, maana watu wengi sasa wana national ID ambao kiukweli si watanzania, pia ndio maana hatuziamini sana Taarifa za NIDA ndo maana tunajiridhisha, kimsing suala hili limefanywa kisiasa"

Akaendelea...

"Siku hizi ukienda kufungua akaunt NMB hakuna haja tena ya kubeba makaratasi ya Serikali za Mitaa wala vitambulisho, cha msingi ni NIN yaani ID number ambayo wanaweka kwenye Portal inayowalink na NIDA kupata taarifa zako, lakini hiyo inakuwa haina madhara sana kwa NMB, kuliko sisi kutumia Portal hiyo tutawapa wasiopaswa pass, inabidi zoezi hili la NIDA lifanywe na Uhamiaji"

Akamalizia kwamba:

"Hata serikali ukiwauliza watakupa sababu zisizo za msingi juu ya hili, lakini ukweli ni kwamba hatuziamini sana taarifa za NIDA maana wakimbizi wengi wanazo hizo ID"

Kuna tofauti ya passport na hichi kitambulisho kwa mawazo yangu. Kila mtu anatakiwa awe na kitambulisho na kama sio raia kwenye stystem zao wanajua. Kwasababu ID ni ya shughuli kama kufungua simu au account ya bank. Passport ndiyo ya raia pekee. Hivyo ni lazima kila mtu zaidi ya miaka 18 wawe na vitambulisho. Hili zoezi lipo nchi nyingi mbona
 
Leo nikiwa hapa Russia nimepata kuongea na Afisa uhamiaji ambaye amesema taarifa anazotoa ni nyeti na wala serikali isingependa zijulikane kwa raia wake maana zitaonesha Udhaifu wake.

Tumejadili yafuatayo:

1. Kwanini ukienda Uhamiaji unaombwa Birth Certificate wakati umeshai submit kwenye NIDA application ya ID?

Kanipa maelezo ambayo nimeridhika

Maelezo yake:

"Kazi inayofanywa na NIDA kimsingi ilipaswa kufanywa na uhamiaji Tanzania, maana watu wengi sasa wana national ID ambao kiukweli si watanzania, pia ndio maana hatuziamini sana Taarifa za NIDA ndo maana tunajiridhisha, kimsing suala hili limefanywa kisiasa"

Akaendelea...

"Siku hizi ukienda kufungua akaunt NMB hakuna haja tena ya kubeba makaratasi ya Serikali za Mitaa wala vitambulisho, cha msingi ni NIN yaani ID number ambayo wanaweka kwenye Portal inayowalink na NIDA kupata taarifa zako, lakini hiyo inakuwa haina madhara sana kwa NMB, kuliko sisi kutumia Portal hiyo tutawapa wasiopaswa pass, inabidi zoezi hili la NIDA lifanywe na Uhamiaji"

Akamalizia kwamba:

"Hata serikali ukiwauliza watakupa sababu zisizo za msingi juu ya hili, lakini ukweli ni kwamba hatuziamini sana taarifa za NIDA maana wakimbizi wengi wanazo hizo ID"
zamani nilikuwa naamini sana taarifa zakompaka ulipotupiga kamba kuhsu Dr shika na kujifanya umefuatilia mkasa wake na umethibitisha. Ndipo nikajua mengi yanayoandikwa humu ni yakufikirika.
JF bwana kila mtu ana access na watu wazito na siri nzito za serikali.
Ila ulichokiandika whether hata kama umekitoa kwenye mawazo yako kina ukweli asimilimia 98
 
Wwatu wengi nawajua hakuna cha Uhamiaji wala nini waliitwa jumapili usiku na kujaza form upande wa mbele, na ule wenye saini na masuala ya serikali za mtaa na kata wakascan ya ambaye alishajaza lakin wakafuta saini na ye akasaini zake, aisee chunguza

Hiyo ni weakness ya system... Walipaswa vitu kama hivyo wavijue kabla havijatokea...
Hivi watu wa intelijensia wapo kwa ajili ya nini?
Ona sasa... Tutakuwa na Watanzania wenye vitambulisho vya Taifa vinavyotambuliwa rasmi ndani nchi... Na Watanzania wasiokuwa na sifa za kusafiri nje ya nchi kwa sababu hawana passports...
Mi nadhani Trump angetuwekea vikwazo ili turudi kwenye drawing table!
We are not yet serious!
 
Sasa matatizo kama hayo

Ndo maana Nipa Ina Expire date
 
Back
Top Bottom