Niliwahi kuchoma moto shamba la kijiji

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,791
Nimesoma kwa mshtuko adhabu mpya ya kuchoma misitu ni miaka 15 jela kifungoni! Pengine pia kuna viboko na faini. Halafu nikatafakari mioto inayoendelea kuunguza mabanda na vibanda vya wafanyabiashara ndogo ndogo nchini.

Hapo juzi ilikuwa Dar mwenge leo ni Tunduma, sijui baada ya Tunduma ni wapi? Wenye ratiba wanajua japo hawataki kutuweka wazi lakini inavyoelekea kazi bado inaendelea mpaka tumalize mikoa yote!

Ni jadi ya kiafrika na pengine na huko duniani kwingine kutumia moto kama njia ya kusafisha mashamba na mapori kwa nia ya kuyaandaa kwa ajili ya msimu wa kilimo ama kufukuza na kuharibu makazi ya wanyama hatari na waharibifu. Njia ya kuchoma moto pamoja na athari zake kimazingira lakini ni nyepesi, rahisi na inaokoa pesa na muda.

Huko vijijini tumeitumia sana njia hii ya moto kama njia rahisi na nzuri ya kuwafukuza na kuharibu makazi ya papasi, mende, viroboto, nyoka, panyabuku nknk!

Kampeni ya kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo wanaofanya biashara zao kwenye maeneo yasiyo rasmi na yasiyoruhusiwa iliyoasisiwa Dsm inaendelea vema nchi nzima kwenye miji mikuu.. Lakini bado kuna maeneo yana upinzani na ukinzani wa hapa na pale kwa visingizio na sababu tofauti tofauti.

Kuna mwanko mkubwa wa serikali kujenga masoko nchi nzima kwenye miji mikuu.. Masoko haya yanahitaji kuwa active ili yasigeuke makazi ya popo na panyabuku na vijiwe vya bangi na madanguro.. Bila kuwa na mkakati wa kuwavuta wafanyabiashara wayatumie .. Itakuwa ni hasara kubwa.

Kuna gharama kubwa ya kuhamisha watu eneo wanalolipenda na kulizoea, lakini kwa 'bahati mbaya' ikitokea ajali ya moto na kuunguza mabanda na bidhaa zao zote kwa hakika watatafuta pa kukimbilia ili maisha yaweze kusonga. Na hakuna pengine zaidi ya masoko rasmi yasiyo na wapangaji

Kufyeka pori ama kichaka ili kuwafukuza wanyama na wadudu hatari na waharibifu kuna hatari za gharama zake kubwa tu. Lakini moto hurahisisha yote. Vip kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara zao maeneo yasiyo rasmi na yasiyoruhusiwa?
 
Unacheka hii tu! Ipo na riwaya yake nyengine alibaka demu halafu chupi akaweka mfukoni alipofika homu si chupi ikaanguka mbele ya wazazi..
Ukiambiwa tutafika motoni haraka sana ndo matukio Kama haya..!
Eti riwaya...
 
Nimesoma kwa mshtuko adhabu mpya ya kuchoma misitu ni miaka 15 jela kifungoni! Pengine pia kuna viboko na faini. Halafu nikatafakari mioto inayoendelea kuunguza mabanda na vibanda vya wafanyabiashara ndogo ndogo nchini.

Hapo juzi ilikuwa Dar mwenge leo ni Tunduma, sijui baada ya Tunduma ni wapi? Wenye ratiba wanajua japo hawataki kutuweka wazi lakini inavyoelekea kazi bado inaendelea mpaka tumalize mikoa yote!
Naongezea.

Ilianza Kariakoo.


Juzi ilikuwa Mabibo Hostel.
 
Back
Top Bottom