Nilivyotumiwa laki 7.5 kimakosa

Nilivyotumiwa laki 7.5 kimakosa

Mimi nilishakuta milioni 1 kwenye account ambayo niliifungua tu kwa wale vijana wa barabarani na sikuwahi kuweka hela yoyote. Nikasubiri sana kama miezi mitatu kila nikichungulia imo! Ah nikaona ujinga nikaamua kuipiga na ile akaunti nikaitelekeza.

Mpaka leo ni zaidi ya miaka minne wala sijawahi kutafutwa na mtu.
Hata mimi nimewahi telekeza account yangu ya NMB kwa miaka zaidi ya mitatu na wakati naitelekeza nilikuwa nimeisafisha haina hela kabisa. Mwaka jana nataka kuifufua naenda kucheki nakuta ina 1.8M. Nilianza kutoa laki 3 nikalipa deni kuna mtu alikuwa ananidai. Iliyobaki nikaendelea kuitumia mdogo mdogo na account ipo mpaka sasa hivi naitumia sijawahi kutafutwa ni zaidi ya mwaka sasa.
 
me waliweka mil 4 sikuigusa sababu nilikuwa sijui.... walikuja kuitoa laiti ningekuwa natembelea mara kwa maraa ningejuaa
 
Hata mimi nimewahi telekeza account yangu ya NMB kwa miaka zaidi ya mitatu na wakati naitelekeza nilikuwa nimeisafisha haina hela kabisa. Mwaka jana nataka kuifufua naenda kucheki nakuta ina 1.8M. Nilianza kutoa laki 3 nikalipa deni kuna mtu alikuwa ananidai. Iliyobaki nikaendelea kuitumia mdogo mdogo na account ipo mpaka sasa hivi naitumia sijawahi kutafutwa ni zaidi ya mwaka sasa.
Usipotafutwa inakua bonge la zar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilieanda kwa wakala wa bank(Equity) maeneo flani ya Mbezi Malamba Mawili nilimpatia pesa aniwekee kwenye account yangu)nilimpatia na ATM Card yangu) baada ya kujaribu kwa zaidi ya mara 3 kudeposit alinirudishia pesa na card yangu na kuniambia kuwa mtandao unasumbua kwa hiyo huduma haikufanikiwa,nikasepa.
Ila kufika saa 5 usiku sms ikaingia kutoka Equity Bank kuwa kiasi flani cha pesa kimewekwa kwenye account yangu (kiwango kile nilichokua nimempatia wakala), bahati mbaya siku inayofuata asubuhi na mapema nilikua na safari ya mkoani,nilichokifanya ni kutoigusa hiyo pesa na kusubiri muhusika arudishe muhamala, baada ya siku 4 nikapokea sms ya pesa kutolewa.
 
Pamoja na kumiliki laini 3 za simu hakuna mtu amewahi kukosea muamala na kunitumia kwenye namba yangu, wala mimi kukosea kutuma kwa ujumla hii kadhia sija wahi kukutana nayo namshukuru Mungu aliye juu [emoji120]
 
Ilikuwa mwez wa 11 nilishangaa ujumbe kwenye simu yangu kutoka tigo nikifahamishwa kupokea laki 7 unusu kutoka namba ya wakala.

Kwa wakati ule biashara zilikuwa zinatembea sana kwa hiyo ile pesa haikunipa tamaa kiviile nikaachana nayo nikaendelea na shughuli zangu nikisubiri jamaa wasitishe muamala ili niondokane na ile zahma.

Mwezi wa kwanza mwishoni soko liliungua na mimi nikaunguliwa biashara zangu zote.

Baadhi ya jamaa zangu wakawa wananitumia pesa ili niweze kujiweka sawa na hapo nikastaajabu kumbe ile pesa ambayo niliamini ilitumwa kimakosa bado ipo.

Kutokana na uhitaji wa pesa kuwa mkubwa kutokana na kutokuwa na biashara nikajikuta ile pesa naanza kuipigia hesabu na nikajiwekea lengo kuwa ikifika mpaka mwez wa nne tarehe 15 ule muamala haujasitishwa basi ile pesa nitaitumia.

Na kwel hiyo siku ilifika nikaenda kwa wakala nikatoa kwa njia ya "Lipa" na nikaitumia vizuri tu.

Huwezi amini mwezi wa 7 nikapigiwa simu naitwa central polisi saa mbili asubuhi niwe nimeshafika.

Asubuhi na mapema nipo kituoni hadi yule askar alinishangaa kwa namna nilivyofika mapema, nikaambiwa kosa langu na mimi nikawaelezea kilichotokea mwishowe ikakubalika kuwa wote wawili tuna makosa kwa hiyo tukae chemba tuyajenge.

Tumekubaliana nilipe laki kila mwezi mpaka deni litakapoisha na sikusita kumshukuru kwa kunikopesha pesa yake ilhali hanifahamu tena bila riba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna rafik yangu alitumiwa laki 5 na wakala akaniambia muda huo huo, nilivo na roho mbaya nikachukua sim yake nikajitumia kwenye airtel yangu alafu tukaitoa. Wakala akapiga sim jamaa akamwambia nimeitoa na mimi nilikua na matatizo nimeitumia
 
Huu nao ni uhuni mwingine, we una uhakika gani kama aliyetuma pesa alikosea kweli
Unajua tu madame sometimes unawapigia simu wote wawili unawaweka conference mwizi anajulikana tu, pia hela hairudi kwa mwenyewe mpaka wote waridhie unless waende polis wote wawil apo mwiz anakuaga mpole tu
 
mwaka juzi niliwahi kuiingiziwa mishahara miwili kwenye account yangu.

yaani mshahara wangu na wa boss mmoja hivi pale kazini. halafu jamaa anavuta kama milioni sita hivi kwa mwezi.

nikawapigia simu maafisa wa bank kuwajulisha kwamba nimewekewa pesa nyingi kwenye account yangu ya mshahara, waondoe kiasi kilichozidi waniachie mshahara wangu.

wakanijibu wao hawana access ya kuhamisha pesa kwenye account ya mtu binafsi mpaka muhusika aridhie kwa maandishi.

siku iliyofata nikapigiwa simu na HR, akaniomba nitoe kiasi kilichozidi, akaniambia ni mshahara wa mtu mwingine.

akasema kuna kosa lilifanyika wakati wana submit account za wafanyakazi kwa maofisa wa bank ambayo inatumika kutupitishia mshahara.

nikaenda zangu bank ku withdrawal milioni sita, nikajaza vile vibunda kwenye kimfuko cha kaki na kumpelekea HR ofisini kwake, wakati naingia pale ofisini, nikamkuta yule boss anasubiri, nikakabidhi na kusepa zangu.

mengine ya huku nyuma sikutaka kujua. nikawaacha peke yao ofisini.
Makato alikatwa nan???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna rafik yangu alitumiwa laki 5 na wakala akaniambia muda huo huo, nilivo na roho mbaya nikachukua sim yake nikajitumia kwenye airtel yangu alafu tukaitoa. Wakala akapiga sim jamaa akamwambia nimeitoa na mimi nilikua na matatizo nimeitumia
Halaf ikawaje???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom