Muuza viatu
JF-Expert Member
- May 14, 2020
- 3,839
- 7,924
Ilikuwa mwez wa 11 nilishangaa ujumbe kwenye simu yangu kutoka tigo nikifahamishwa kupokea laki 7 unusu kutoka namba ya wakala.
Kwa wakati ule biashara zilikuwa zinatembea sana kwa hiyo ile pesa haikunipa tamaa kiviile nikaachana nayo nikaendelea na shughuli zangu nikisubiri jamaa wasitishe muamala ili niondokane na ile zahma.
Mwezi wa kwanza mwishoni soko liliungua na mimi nikaunguliwa biashara zangu zote.
Baadhi ya jamaa zangu wakawa wananitumia pesa ili niweze kujiweka sawa na hapo nikastaajabu kumbe ile pesa ambayo niliamini ilitumwa kimakosa bado ipo.
Kutokana na uhitaji wa pesa kuwa mkubwa kutokana na kutokuwa na biashara nikajikuta ile pesa naanza kuipigia hesabu na nikajiwekea lengo kuwa ikifika mpaka mwez wa nne tarehe 15 ule muamala haujasitishwa basi ile pesa nitaitumia.
Na kwel hiyo siku ilifika nikaenda kwa wakala nikatoa kwa njia ya "Lipa" na nikaitumia vizuri tu.
Huwezi amini mwezi wa 7 nikapigiwa simu naitwa central polisi saa mbili asubuhi niwe nimeshafika.
Asubuhi na mapema nipo kituoni hadi yule askar alinishangaa kwa namna nilivyofika mapema, nikaambiwa kosa langu na mimi nikawaelezea kilichotokea mwishowe ikakubalika kuwa wote wawili tuna makosa kwa hiyo tukae chemba tuyajenge.
Tumekubaliana nilipe laki kila mwezi mpaka deni litakapoisha na sikusita kumshukuru kwa kunikopesha pesa yake ilhali hanifahamu tena bila riba.
Sent using Jamii Forums mobile app