SoC02 Nilivyotengeneza helkopta

Stories of Change - 2022 Competition

Theorist Mosses

JF-Expert Member
Jul 16, 2022
345
253
Habari, ndugu jamaa na marafiki kwa jina naitwa Moris, nilizaliwa mkoa wa mara nilisoma na kumaliza masomo ya sekondari na kufaulu vizuri mkoani mara.

Baada ya kumaliza masomo ya sekondari nili jiusisha na kazi ya ufundi umeme wa majumbani, ambapo kazi hii hapo awali alikuwa akifanya baba yangu.

Ndoto yangu ilikuwa nikuja kuwa rubani wa ndege na nilipenda sana maswala ya utafiti na uchunguzi. lakini pia nilipenda kushirikiana na watu wadogo kwa wakubwa, pamoja na kujifunza "kinaganaga" vitu vingi sana.

Kama vile usomaji wa vitabu mbalimbali vikiwemo vitabu vya dini na bidii katika kazi ya ufundi umeme ilinisaidia sana. lakini pia nilifanya bidii katika ibada, ambapo nilikuwa nikifanya bidii ili nije kutimiza ndoto yangu ambayo ni kuja kufanya kazi ya urubani wa ndege.

Katika chunguzi na tafiti zangu Kwa mara ya kwanza nilifanikiwa kutengeneza mashine ya kuzarisha umeme, ambayo ilifanya kazi vizuri lakini nakumbuka mashine hii ilinipa "wigo" msukumo mzuri wa kuiboresha mashine iwe bora zaidi. sikuishia hapo lakini nilijiendeleza kwa kujifunza kupitia vitabu vya kisayansi, ambapo baadae nilipata "shauku" iliyo nipelekea kufanikiwa kwa wazo la kutengeneza helikopta.

Nadhani nilitengeneza kitu bora na cha tofauti kuliko ninavyokielezea hapa. lakini kwa sababu sikuwa na vibali maalum kutoka vitengo husika vya kiserikali pamoja na mamlaka ya anga ilinipelekea kufungiwa kwa sababu ya kukosa vigezo sababu nyengine sikuwa na reseni.

Pengine wapo vijana wenzangu wengi sana mitaani, ambao hawaja fahamika "kinagaubaga" Kutokana na kazi zao. Ingawa pamoja na mapinduzi makubwa ya teknolojia walio yafanya ndani na nje ya Tanzania, wenye ndoto sawa na zangu lakini wame fukiwa kwenye shimo "kindakindaki" hata wasiweze kupewa nafasi ya kuonesha maarifa walio nayo na vipaji vyao.

Matokeo yake wanatokea watu wenye jicho la "husuda" ambao wasiokuwa na maslahi bora kwa vijana pamoja na taifa kwa ujumla. ambao wanafanya kazi ya kuzima vipaji kupitia madaraka na siyo kwamba nchi yetu hatuwezi kuendelea kwenye maswala ya kisayansi na kiteknolojia "la hasha" kumbe tunajiangamiza wenyewe na kujiteketeza "kimasomaso" bila kujua.

Kupitia kwa vijana wanao zaniwa kuwa wao siyo kitu na kufungiwa kazi zao kwasababu zisizo za msingi, matokeo yake wanaendeleza watu wasio na ujuzi wowote kwenye hizo fani ambapo inapelekea taifa kuzidi kushuka kimaendeleo na kiuchumi.

Nina imani kwamba kitaka kila kizazi kipya ndani ya kila miaka mitano, lazima kuna vijana wenzangu wanao chipuka kwenye fani mbalimbali kwenye nyanja zote ambao naweza kusema ni vijana hodari sana ambao hawaja somea kwenye hizo fani walizopo.

Taifa zuri hujengwa na vijana, watu wengi wamekuwa wakishuhudia vijana ambao tunaishi nao tu mitaani. wengine ni ndugu zetu tumeona vipaji vyao walivyo vionesha kwa njia mbalimbali lakini kwa sababu ya kutoendelezwa imewapelekea kualibikiwa kisaikolojia matokeo yake kuanguka kwenye "ngada" na madawa ya kulevya.

Najua wapo vijana wenzangu miongoni mwetu walio fanikiwa kutengeneza vitu vingi vikubwa zaidi yangu, lakini wameshindwa kujiendeleza katika nyanja zote ikiwemo katika sayansi na teknolojia. pamoja na kwamba vitu walivyo vitengeneza vimeonekana lakini kwa sababu ya kuto kizi vigezo vya kiserikali wamefungiwa.

Hivyo naungana pamoja na vijana wenzangu kutoa "lai" kwa serikali, iangalie kwa ukaribu namna bora ya kutuendeleza sisi vijana kwenye nyanja zote. kwamba vijana wapewe kipaumbele itapelekea vijana wengi kupata "hulka" ya ajira na kujiamini pamoja na kuimarika kisaikolojia.

Hakika"penye nia pana njia"Itasaidia sana pia kuwavuta vijana wengine wa mitaani kupata fursa kuacha tabia ambazo ni mbovu mara moja. kama vile "panya road" tabia ambazo zinaweza kuyumbisha au kuangusha kabisa uchumi wa taifa, jambo ili nalitazama kwa mapana zaidi kwa sababu vijana ni "mbegu" ambazo zina paswa kuangaliwa ili ziweze kustawi vizuri zitazamwe Kama kitovu cha taifa la kesho.

Serikali ihakikishe vijana wanapata haki zao za msingi, iwapo kama ikitokea kuna kijana amegundua kitu flani ndani ya sayansi na kwamba kipaji chake kimeonekana na kuthibitishwa tayari.

Serikali isimfungie kwa sababu kwa kufanya hivyo itamuharibu kijana kisaikolojia, kama ikatokea ajakizi vigezo asifungiwe lakini iangaliwe namna bora ambapo kijana aweze kupata kibali pamoja na elimu zaidi. kwasababu kwakufanya hivyo taifa litakuwa linapanda "mbegu" iliyo bora na imara zaidi kwa ajiri ya maendeleo bora na kupata vijana wenye ujuzi.

Kama ikitokea kijana hana elimu ya kutosha kwamba ameshindwa kupata kibali kwa sababu ya elimu ndogo aliyo kuwa nayo. Lakini tukirudi kwenye uwezo wake na ujuzi kwamba kipaji chake tayari kime onekana pamoja na kuthibitishwa na wataalam mbalimbali wa serikali basi kijana asomeshwe.

Serikali na vyombo husika vichukulie kwa mitazamo mipana sana na kwaajiri ya sayansi na teknolojia ya taifa la kesho. ili kijana anapo maliza masomo afanye kazi ya ndoto zake kwasababu kipaji ni "kimwasu" naamini kwa namna moja ama nyengine kwa njia hii nchi yetu itaendelea kiuchumi katika nyanja zote ikiwemo kwenye ajira, sanaa, elimu, michezo, sayansi na teknolojia.

Lakini pia wazazi na walezi muhakikishe mnakuwa mstari wa mbele kuhakikisha vijana wanapata malezi na ushauri mzuri ulio bora wenye tija ndani yake. ambayo ni njia itakayo wafanya vijana kujisikia kuwa wao ni watu wa muhimu sana wanaohitajika na wenye mchango mkubwa ndani ya jamii inayo wazunguka. Ili waimarike vizuri kisaikolojia pamoja na kuwakumbusha vijana kwenda na kuhudhulia kwenye nyumba za ibada ili kukomesha tabia chafu za vijana Kama vile. kushinda kijiweni mda wote, kujiunga na makundi ya kijambazi, kuuza na kusafirisha madawa ya kulevya.
 
" kuwakumbusha vijana kwenda na kuhudhuria kwenye nyumba za ibada ili kukomesha tabia chafu za vijana Kama vile. kushinda kijiweni muda wote, kujiunga na makundi ya kijambazi, kuuza na kusafirisha madawa ya kulevya".
 
" kuwakumbusha vijana kwenda na kuhudhuria kwenye nyumba za ibada ili kukomesha tabia chafu za vijana Kama vile. kushinda kijiweni muda wote, kujiunga na makundi ya kijambazi, kuuza na kusafirisha madawa ya kulevya".
Vijana wajifunze kiroho, kiakili na kimwili
Nimekupiga kura 1 mkuu
Asante Sana kwani "umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu"
 
Vijana wa Tanzania wakiacha ujinga wanaweza kutengeneza shule ya wana anga za mbali
Ni miongoni mwa ndoto zangu kwa sasa nimejifunza concept Kama za kurusha rocket, pia nime jifunza theory kama vile za kina Einstein ( general relative, quantum physics, newton theory of gravity" lakini katika kujifunza huku nimefanikiwa kutengeneza theory yangu mwenyewe inayo husu "big bang" namuomba sana mungu nitimize ndoto yangu ya kuja kufungua kampuni binafsi ya anga hapa nchini. nadhani kila kitu kinawezekana kwa vijana itabidi tuwaombe Sana vijana wa ki-Tanzania wabadirike wawe "chanya" Lakini pia tusisahau kuwaombea vijana wale waliopo mahututi hospitalini.
 
Tafadhali, ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura yako kwa kubonyeza arama ya kimshare "^" chini kabisa ya post hii kuniwezesha kuibuka mshindi.
 
Tafadhali, ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura yako kwa kubonyeza arama ya kimshare "^" chini kabisa ya post hii kuniwezesha kuibuka mshindi.
 
Mimi nikiwa shule ya msingi nilitengeneza pampu ya kuvuta maji kisimani, nilitamani kufanya makubwa zaid, but haikuwezekana.

Ni hivyo tu na haijawai kuwezekana, nailaumu serikali, na mifumo yake yote ya elimu ya kipumbavu.

Pia mikataba waliyosaini wakuu wetu wa nchi ndiyo inakandamiza raia na kuwazuia wasibuni vitu vitakavyokuja kuuwa biashara za wakubwa huko uzunguni na uarabuni bila kusahau uchina na uhindini.

Huwezi amini kwa nchi kama yetu kuna madini ya uranium kwa wingi ambayo yakitumika vzr yanaweza kuzalisha umeme ambao ukaja kufuta tatizo la umeme nchini DAIMA bila kutegemea chanzo kingine chochote kile cha nishati.

So wakubwa wa nchi za mabwana huko dunia ya kwanza waliwasainisha viongoz wetu wasifanye mining yoyote ya uranium sababu madini hayo ndyo hutumika ktk uzalishaji wa Atomic bombs(nuclear), so mabwana wakahusisha kuwa tutapata nguvu na kuleta hatar ya kuunda manyuklia ambayo tunaweza yatumia kuwafurumusha pia tukipata nishati ya kutosha tutapata uwekezaji mkubwa wa viwanda ambavyo vitauwa uingizaji wa bidhaa zao afrika.

Usishangae vijana wengi wanaunda siraha, mitambo ya radio, umeme, magari yasiyotumia mafuta, na mengi makubwa, haya yote yanazibwa sababu kuu ni ushindani wa kibiashara kwa kuzididimiza nchi za kiafrika zisiendelee bali zibaki kuwa soko kuu la bidhaa zao.

Ukombozi wa haya yote utakuja pale tutakapopata kiongozi sahihi asiyeamini ktk misaada na utegemezi wa wazungu, or otherwise tutabaki kulaumiana humu kila siku
 
Mimi nikiwa shule ya msingi nilitengeneza pampu ya kuvuta maji kisimani, nilitamani kufanya makubwa zaid, but haikuwezekana.

Ni hivyo tu na haijawai kuwezekana, nailaumu serikali, na mifumo yake yote ya elimu ya kipumbavu.
Kaka kwanza nikupongeze Sana kwa kutengeneza "pampu" ni kazi kubwa sana uliyo ifanya wakaishia kukufungia inauma sana pamoja na kwamba wao awajui hata "kutengeneza mashine ya kufyatulia tofali" manually.

umeongea jambo La msingi Sana unajua "uchumi" ni vita, ambayo inapiganiwa Sana kwa maslahi mapana ya taifa flani.

nchi "huru" nzuri na imara ni ile inayo angalia misingi yake pasipo kuangalia mikataba flani, ambayo inaweza kufanya viongozi kuwa na tamaa ya madaraka na kupokea rushwa.
 
Tafadhali, ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura yako kwa kubonyeza arama ya kimshare "^" chini kabisa ya post hii kuniwezesha kuibuka mshindi.
 
Tafadhali, ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura yako kwa kubonyeza arama ya kimshare "^" chini kabisa ya post hii kuniwezesha kuibuka mshindi.
 
Tafadhali, ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura yako kwa kubonyeza arama ya kimshare "^" chini kabisa ya post hii kuniwezesha kuibuka mshindi.
 
Tafathali, ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura kwa kubonyeza arama ya kimshare "^" chini kabisa ya post hii kura yako itaniwezesha kuibuka mshindi.
 
Frankdunia Upo sahihi ndugu serikali iangalie namna bora kwamba vijana wapate fursa ya ajira pamoja na haki ya kujiajiri.

Vijana waruhusiwe pia kujiajiri kwenye upande wa teknolojia na sayansi, siyo tu kwenye kilimo na boda boda, ili nchi iendelee kwenye nyanja zote kwa ajiri ya taifa bora la kesho.
 
Back
Top Bottom