Mbute na chai
JF-Expert Member
- Jul 21, 2012
- 571
- 610
Hiyo miti ya zambarau sio imaraTukio lililonitokea nikiwa darasa la tatu.
Ikiwa muda wa masomo umemalizika, nikiwa na wanafunzi wenzangu, tunapita jirani na mti wa mzambarao. Mti ule ulikuwa umesheheni zambarao zilizoiva na nono zaidi, wale waliyopitia maisha haya nadhani wananielewa vizuri. Mti huo ulikuwa mrefu mithili ya futi 60 hivi za urefu basi, kwakuwa nilikuwa mtundu nikasema ngoja nikwee nikajiangulie yaliyo mazuri zaidi. Nilimkabidhi rafiki yangu mfuko wangu wa madaftari uliyojulikana kama sport enzi hizo, nikamwambia nikidondosha zambarao unanihifadhia. Nilipofika mtini nikasema ngoja nile kwanza halafu nitashusha zingine. Baada ya kutosheka kula nikaanza kuangua na kumdondoshea rafiki yangu ahifadhi.
Nilipokuwa nadondosha zile zambarao nilisikia huko chini wakibishana na yule rafiki yangu akiwaambia ‘mimi ndiye ninayemkusanyia.’ Juu ya mti zambarao zile nono huwa zinatabia ya kuwa kwenye matawi membamba ya pembezoni nikajisemea isiwe tabu, basi nikashika tawi nene mkono wa kushoto huku mkono mwingine nikijinyoosha kufikia hizo zambarao na kumbe lile tawi nene lilikuwa na wadudu ambao tulikuwa tunawaita nyugi (wasp) jamii kama ya nyuki. Kumbe nilivyokuwa najinyoosha ndivyo nilivyokuwa natingisha kile kijumba chao na nilipokaribia kukamata kitawi chenye zile zambarao nikasikia kama mtu kanidunga sindano ya sikio, kwa wenge nikaachia lile tawi nene, mama yangu!!!! Nilisikia pwaaaaaach, parapataaaaa, kurukunguuu…… nikiwa katika hali ya taharuki nasikia huko chini zinakuja nyingi naomba na sisi tukuokotee bila kujua kuwa nilikuwa mimi mwenyewe ndiye naporomoka kama jackie chan kwenye movie ya who am I. Mungu saidia nikanasa kwenye matawi ya katikati huku jasho uchafu ule unaotoka kwa kujificha vyote vimenienea. Ile kama napata hafueni lile tawi lililonikwamisha pale likavunjika bahati nzuri nikawa nimekanyaga mti wenyewe. USIOMBE YAKUKUTE.
"kwa wenge nikaachia lile tawi nene, mama yangu!!!! Nilisikia pwaaaaaach, parapataaaaa, kurukunguuu……"
Sio kwa muanguko huu..😂
Umenitenga sana sikuhizi!!
Mie niliwahi ng'atwa madondola nikiwa juu ya mwembe nilijikuta niko chini sema huo mwembe haukua mrefu sana,hii ya zambarau ilimuua kijana wa jirani yetu alianguka toka kwenye mzambarau akafa,pumzika kwa amani DeusTukio lililonitokea nikiwa darasa la tatu.
Ikiwa muda wa masomo umemalizika, nikiwa na wanafunzi wenzangu, tunapita jirani na mti wa mzambarao. Mti ule ulikuwa umesheheni zambarao zilizoiva na nono zaidi, wale waliyopitia maisha haya nadhani wananielewa vizuri. Mti huo ulikuwa mrefu mithili ya futi 60 hivi za urefu basi, kwakuwa nilikuwa mtundu nikasema ngoja nikwee nikajiangulie yaliyo mazuri zaidi. Nilimkabidhi rafiki yangu mfuko wangu wa madaftari uliyojulikana kama sport enzi hizo, nikamwambia nikidondosha zambarao unanihifadhia. Nilipofika mtini nikasema ngoja nile kwanza halafu nitashusha zingine. Baada ya kutosheka kula nikaanza kuangua na kumdondoshea rafiki yangu ahifadhi.
Nilipokuwa nadondosha zile zambarao nilisikia huko chini wakibishana na yule rafiki yangu akiwaambia ‘mimi ndiye ninayemkusanyia.’ Juu ya mti zambarao zile nono huwa zinatabia ya kuwa kwenye matawi membamba ya pembezoni nikajisemea isiwe tabu, basi nikashika tawi nene mkono wa kushoto huku mkono mwingine nikijinyoosha kufikia hizo zambarao na kumbe lile tawi nene lilikuwa na wadudu ambao tulikuwa tunawaita nyugi (wasp) jamii kama ya nyuki. Kumbe nilivyokuwa najinyoosha ndivyo nilivyokuwa natingisha kile kijumba chao na nilipokaribia kukamata kitawi chenye zile zambarao nikasikia kama mtu kanidunga sindano ya sikio, kwa wenge nikaachia lile tawi nene, mama yangu!!!! Nilisikia pwaaaaaach, parapataaaaa, kurukunguuu…… nikiwa katika hali ya taharuki nasikia huko chini zinakuja nyingi naomba na sisi tukuokotee bila kujua kuwa nilikuwa mimi mwenyewe ndiye naporomoka kama jackie chan kwenye movie ya who am I. Mungu saidia nikanasa kwenye matawi ya katikati huku jasho uchafu ule unaotoka kwa kujificha vyote vimenienea. Ile kama napata hafueni lile tawi lililonikwamisha pale likavunjika bahati nzuri nikawa nimekanyaga mti wenyewe. USIOMBE YAKUKUTE.
Duh mti ulikua mrefu sana eeh, maskini hadi kufa ni maumivu gani hayo aliyapitia😪Mie niliwahi ng'atwa madondola nikiwa juu ya mwembe nilijikuta niko chini sema huo mwembe haukua mrefu sana,hii ya zambarau ilimuua kijana wa jirani yetu alianguka toka kwenye mzambarau akafa,pumzika kwa amani Deus
Hii miti ni mirefu sana? Na inaonesha ni rahisi kukatika ama kuteleza, hadi mtu afe aiseeMizambarau inatabia ya kuteleza na miti yake rahisi sana kukatika, hasa kipindi cha mvua
Udogoni nilikua na dance sana juu ya matawi, hadi mwenzetu alipokata moto kwa kuanguka juu ya mzambarau pale kijijini mang'ula (mwaya )
Mazambarau mazuri yanakaa juu sana na mwishoni mwishoniHii miti ni mirefu sana? Na inaonesha ni rahisi kukatika ama kuteleza, hadi mtu afe aisee
Aisee pole, hadi unajiachia kwani hao dondola walikua bado wanakufata? Au ni maumivu yake tu hadi watu wanaachia mti na kuanguka? Kama nakuonà ulivobakiwa na manundu ya dondola😂😂Mazambarau mazuri yanakaa juu sana na mwishoni mwishoni
Ukichukulia na umri wa mtoto (8-14), kufa ni swala dogo sana ukianguka kutoka kwenye mti
Niliwai kukutana na NYIGU juu ya mti, wakaanza kunigonga
Akili ilicheza fasta, nikasema hapa nikiachia mti tu, basi nimekufa
Ilibidi nishuke kwenye mti kwa speed ya light, kukaribia na chini nikajiachia jumla
Nikatoka Mbio umbali flani ndio nikaanza kujikagua, michubuko na manundu ya dondola[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
When I was kid, nilikua mtundu sana[emoji119][emoji119][emoji119]
Umenitenga sana sikuhizi!!
Mi mzima sijui wewe..?Hata sijakutenga shughuli tu zimekuwa nyingi.
Mzima lakini?