Nilivyomtapeli Tapeli hadi akalia

Nilivyomtapeli Tapeli hadi akalia

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Posts
2,931
Reaction score
4,549
Mwaka 2009 nilipata binti mrembo kwenye mtandao akaniambia anaishi Marekani ila ana asili ya Gambia,kadri tulivyoendelea kuchat ndivyo alivyokuwa akinipa ushawishi wa kwenda US,nikashtulia na rafiki yangu kuwa hawa huwa ni matapeli nikae chonjo.

Siku moja akaniambia kuwa kulikuwa na kongamano la dini US la vijana na angeniunganisha kwa anko wake aliyeko Gambia ili niende,kweli nikaanza mawasiliano na huyo anko ambaye aliniambia nikusanye vijana 20 na kila kijana awe na $300 kama ada ya kiingilio.

Nikamwambia nina ndugu zangu kijijini wapo 10 na nitaenda kuwaambia ila sina nauli ya kunipeleka huko kama anaweza anitumie pesa ya nauli niende nikauze ng'ombe ili pia niwalipie ada hao ndugu zangu 10,akaniuliza idadi ya ng'ombe tunaomiliki nikamwambia ni zaidi ya 200,sikuamini aliponitumia $120.

Ili ikibidi nipande ndege niwahi kuuza ng'ombe na kulipia ada ya watu 10 alituma kwa WESTERN UNION,nilipoichukua hiyo pesa nikamwambia na wewe nimekutapeli,alinipigia simu analia akisema hiyo ni pesa ya Kanisa niirudishe upesi.
 
Vizuri sana maana wasumbufu mno Kila siku HI MTU humjui Mara Email wapuz
 
Huyo alikuwa tapeli mwanafunzi..Trick yako ipo veeeery open such that hata mjanja mjanja tu wa town anastukia
 
Yani ungeuza ngo'mbe ungempa hela zote hata hiyo naulie ingekua ndogo kwa hela ambayo ungempa
 
Mwaka 2009 nilipata binti mrembo kwenye mtandao akaniambia anaishi Marekani ila ana asili ya Gambia,kadri tulivyoendelea kuchat ndivyo alivyokuwa akinipa ushawishi wa kwenda US,nikashtulia na rafiki yangu kuwa hawa huwa ni matapeli nikae chonjo.

Siku moja akaniambia kuwa kulikuwa na kongamano la dini US la vijana na angeniunganisha kwa anko wake aliyeko Gambia ili niende,kweli nikaanza mawasiliano na huyo anko ambaye aliniambia nikusanye vijana 20 na kila kijana awe na $300 kama ada ya kiingilio.

Nikamwambia nina ndugu zangu kijijini wapo 10 na nitaenda kuwaambia ila sina nauli ya kunipeleka huko kama anaweza anitumie pesa ya nauli niende nikauze ng'ombe ili pia niwalipie ada hao ndugu zangu 10,akaniuliza idadi ya ng'ombe tunaomiliki nikamwambia ni zaidi ya 200,sikuamini aliponitumia $120.

Ili ikibidi nipande ndege niwahi kuuza ng'ombe na kulipia ada ya watu 10 alituma kwa WESTERN UNION,nilipoichukua hiyo pesa nikamwambia na wewe nimekutapeli,alinipigia simu analia akisema hiyo ni pesa ya Kanisa niirudishe upesi.

wewe ni kiboko
 
Back
Top Bottom