Thomas10
JF-Expert Member
- Mar 9, 2017
- 841
- 2,268
Rafiki yangu wa karibu, aliachwa na mwenzi aliyemhudumia kwa miaka takribani sita (6) hivi. Alianza nae mahusiano binti akiwa amemaliza kidato cha nne, aliapata ufaulu wa daraja la nne (div 4 point 28)
Alijitoa kumlipia ada na mahitaji mengine ya kibinadamu tangu alipoanza masomo ya ngazi ya cheti, akaunganisha stashahada, na kisha akaunga shahada.
Kwa kipindi chote hicho, ahadi kuu ya mahusiano yao ilikuwa kuoana. Baada ya binti kumaliza, aliamua kumwambia jamaa kuwa hawezi tena kuendelea naye na hivyo atafute mwanamke mwingine. Kwakuwa binti tayari alipata kazi kwenye taasisi fulani, akamuomba amrudishie pesa yake kidogokidogo hadi itakapokwisha.
Jamaa alikosa cha kuamua, akaja kwangu amevurugwa mno, amejawa roho ya kuua, akaniomba ushauri. Hapo nilikumbuka mafunzo ya mjomba wangu kuhusu mke na maisha ya ndoa. Nikalazimika kumpa ushauri ambao ulikuwa kwa mtindo wa maswali ambapo sikumtaka ajibu, bali atafakari na akipata majibu, afanye uamuzi;
Kwako wewe (rafiki) mke ni nani na ndoa ni nini?
Unapofikiria kuhusu kuoa, unalenga kuoa ili iweje?
Mke utakayemuoa, unataka akutimizie wajibu gani?
Katika wanawake uliowahi kuwa nao na unaowaona mtaani, wamepungukiwa nini linapokuja suala la mke?
Unataka kuoa kutimiza hisia au kutengeneza familia?
Ukimuoa mwanamke uliyemgharamia utakuwa umepata mke bora au umepata mwanamke wa kuoa?
Maswali hayo mepesi kabisa, nilimwambia aende akayajibu moyoni mwake usiku ule, hata wiki hadi mwezi. Akiona majibu yote yanaangukia kwa huyo mwanamke aliyemgharamia, basi amuue (kama alivyopanga) na akiona wapo wanawake wengi wanajibu hayo, basi amsamehe na aendelee na maisha yake.
Sasa ni miezi miwili, ameamua kumsamehe yule binti, amemwambia hata pesa asimrudishie.
Anaumia sana, lakini anaamini itaisha.