Nilivyompenda msichana mrembo na mchamungu

Nilivyompenda msichana mrembo na mchamungu

Ushimen

Platinum Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
44,832
Reaction score
113,201
Malengo yetu ilikua tukuje kuoana
baada ya muda.
Pasipo mashaka, nilijitoa sana kwa binti huyu na hata ndugu jamaa na marafiki wote waliniona mjinga, lakini hali ile haikuweza kunifanya nikate tamaa kwasababu ukweli ni kuwa nilimpenda msichana yule kwa dhati na hakika niliachana na makando yote yenye nilikua nayo.
Binti alipo maliza chuo, nikimsaidia na akapata job poa sana, na pia nilimshauri pamoja na kumkumbusha kuhusu mipango yetu ya maisha ya
maisha huko mbeleni. Na kila ilipo stimia usiku kabla ya kulala, nilikua nikisali na kumuombea pia.
Siku moja binti alikua anasherehekea siku
yake ya kuzaliwa...hivyo akaalika marafiki
zake, na watu wengine muhimu pamoja na mimi mpenzi wake.
Wageni wote walifika kwa wakati isipokua mimi nilichelewa kidogo... Hivyo
msichana akatumia muda ule ambao mimi nilikua bado sijafika kuwaelezea wageni
namna jinsi mimi nilivyokua wa muhimu ndani yake....
Ama kwa hakika inasemekana alinisifia sana, na akaweka wazi jinsi nilivyo muahidi kumvalusha pete ya uchumba hapo siku za karibuni, na akasema siku hiyo ya birthday yake anategemea zawadi kubwa sana kutoka kwangu mimi mpenzi wa
nafsi yake.
Baada ya muda sikitambo nami nikaingia na kuketi high table.. Muda wa zawadi ulipofika watu wakamtunza binti zawadi mbalimbali na mimi nikakua wa mwisho kwenda kumtuza mpenzi wangu zawadi... Basi hali hile ilipelekea wageni wote wakawa na hamu ya kutaka kujua
zawadi nitakayo kwenda kuntuza mpenzi wangu, na hali hii ilichochewa hasa baada ya mpenzi wangu yule kunisifia sana mbele ya wageni waalikwa.
Basi taratibu niliamka na kutoa mfuko.. kila mtu akataka kujua kilichokua ndani ya
mfuko ule, na kisha nikafungua mfuko na
kutoa mkate..!!
Lahaula...[emoji53] [emoji53] [emoji53]
Watu wote wakahamaki na kustaajabu..mkate[emoji134] [emoji134] [emoji134]
Lakini kabla sijasema lolote kuhusu ule mkate, ghafla mpenzi wangu alianza
kulia kwa kwikwi.... na pia alipandwa na jazba kama mkizi, akapandwa hasira kwa kuwa eti nili muaibisha..!!
Wakati akiendelea kulia kwa kwikwi, ghafla alinikwida shati na kunivuta tai yangu hadi ikajivua, alinimwagia juisi,
kisha akauchukua ule mkate na
kuutupa.!!
Ama kwa hakika nilifedheheka sana kwa jinsi mpenzi wangu alivyo utweza utu wangu.... [emoji29] [emoji29] [emoji29] niliamua kuukimbilia ule mkate na kuuokota, na kisha nikarudi high table na kusema "baby nakushukuru kwa yote..Huenda umenidharau kwa kuwa
nimekuletea zawadi hii ndogo kwenye
siku yako muhimu kama hii, lakini kama
ungetambua thamani ya zawadi hii,
usingefanya haya..".

Baada ya kusema yale, nilifungua ule mkate na kutoa vitu viwili alivyoficha ndani ya mkate.
Kwanza nitoa ufunguo wa gari, ambalo nilikuwa nime mnunulia mpenzi wangu na nilitaka/panga nimkabidhi siku hiyo muhimu ya kumbukumbu yake ya kuzaliwa.
Kisha nikatoa pete ya uchumba na kusema
"Nilimuomba Mungu anipe mwanamke
atakayenipenda katika hali yoyote.
Nilipanga leo nikuvalishe pete hii ili
kuelekea ndoto yetu ya ndoa..
..Lakini kwa kuwa uliangalia nje, uliona
mkate, badala ya pete hii ya thamani
iliyokua ndani.. Naamini mwanamke
niliyemuomba kwa Mungu bado
sijampata..
. Nashukuru kwa yote
uliyonifanyia, nimekusamehe, nawe
naomba unisamehe kama nimekukwaza. Msichana akaomba msamaha
lakini ilikua tayari amechelewa....
Kisha nikachukua mkate wangu, huyoo
akaondoka......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom