Niliumizwa sana nashindwa kusahau

Ndugu zangu mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 35. Niliumizwa sana na mwenzangu baba wa mtoto wangu na nimeachana nae miaka 12 iliyopita.

Mtoto yuko Form One, baba hana hata habari nae, lakini nashukuru mungu nimejitahidi na nitajitahidi apate elimu. Tatizo ni kwamba kila nikiingia kwenye uhusiano mpya nakuwa muoga na sana imefikia hatua sihitaji tena kuwa na mwanaume. Yaani naogopa vitu vilivyonitokea mwanzo na mwisho nahisi sijui kumpenda mtu yaani kuubwaga moyo nakuwa na wasiwasi na kushindwa kujiachia.

Naombeni ushauri nifanyeje ili niwe sawa na wanawake wengine
Kwa hiyo wewe ni single mother?????
 
Back
Top Bottom