Niliugua sana mpaka nikafikia hatua ya kutamka aheri waliokufa kuliko walio hai

Ni kweli mkuu,ukiwa na afya njema ndio kila kitu,hebu jaribu kufikiria una mamilioni ya pesa halafu unaumwa,kwa siku sio chini ya vidonge kumi hapo kuna faida gani,hapo unaweza hata kutamani utajiri wote uondoke ili ubaki na afya njema,cha muhimu ni kumtanguliza Mungu katika kila jambo ili atujalie maisha yenye afya njema kila wakati...
Kweli ni kama una cash halafu mashine haifanyi kazi
 
Ni kweli mkuu,ukiwa na afya njema ndio kila kitu,hebu jaribu kufikiria una mamilioni ya pesa halafu unaumwa,kwa siku sio chini ya vidonge kumi hapo kuna faida gani,hapo unaweza hata kutamani utajiri wote uondoke ili ubaki na afya njema,cha muhimu ni kumtanguliza Mungu katika kila jambo ili atujalie maisha yenye afya njema kila wakati...
Upo sahihi sana. Kuna jamaa yangu mmoja yeye alikua anaumwa kichwa tu hakuna lingine. Jamaa kichwa kilikua kinamuuma mpaka anachanganyikiwa yaani ni analia kama mtoto hawezi kufanya chochote. Zunguka hospitali zote hakuna kitu maumivu yako palepale. Daah aisee hakuna utajiri mkubwa zaidi ya afya hapa duniani.
 
dah pole mkuu mi pia niliwahi ugua miaka karibu mitano nipo kitandan nkapoteza shule,ndugu jamaa marafiki girlfriend,,yaan mwshowe hadi simu ikawa si ya maana sana maana hakuna anayepiga hata mwezi unapita, nlipopata nafuu nkaanza kila kitu na upya hadi marafiki ninao wapya
Kama hujawahi pitia changamoto za kuumwa magonjwa yakukuweka chini kwa muda mrefu na kuvuruga kila kitu kwe maisha yako mshukuru sana Mungu kwa hilo usiache kumuomba Aisee
 
dah pole mkuu mi pia niliwahi ugua miaka karibu mitano nipo kitandan nkapoteza shule,ndugu jamaa marafiki girlfriend,,yaan mwshowe hadi simu ikawa si ya maana sana maana hakuna anayepiga hata mwezi unapita, nlipopata nafuu nkaanza kila kitu na upya hadi marafiki ninao wapya
Kama hujawahi pitia changamoto za kuumwa magonjwa yakukuweka chini kwa muda mrefu na kuvuruga kila kitu kwe maisha yako mshukuru sana Mungu kwa hilo usiache kumuomba Aisee
vipi girlfriend wako aliekukimbia yupo?
 
Shukuru kwa yote ndugu bado huko hai, na pia pole Sana kwa hali ngumu uliopitia.
 
mara ya mwisho kuwasiliana naye alikuwa dar kwasasa sijui alipo, ila si kwamba alinkimbia, alinisupport kadri alivyoweza kwa karibu miaka mitatu hivi then baadae nayeye alichoka akamove on, namshukuru tu kwa vile alivyojitoa,kokote aliko Mungu ambariki sana
atakuwa alijua utakufa
 
atakuwa alijua utakufa
hahaha inawezekana aisee, ila nlichojifunza kwe haya maisha kila mtu anabeba mzigo wake mwenyew usije ukajidanganya eti huyu ni rafiki yangu wa kufa na kuzikana acha kabisa pia kuna kipindi inafika damu inakuwa sio nzito tena kuliko maji, dunia ni sehemu katili sana
 
Kila Mtu amewahi kuumwa Mkuu, some times kuliko wewe, wewe sema uliumwaje, wakt ingine km mimi hivi...

Niliumwa Malaria siku kadhaa wee! nikakonda kiasi cha kutosha , Ilianza kama uchawi uchawi hivi, hadi kuhisi nimerogwa nini? kilicho nifanya nihisi uchawi ni km ifuatavyo;


Asubuhi hadi mchana wote nakuwa Mzima kabisaaa wa Afya njema, kwa maana kuwa nacheka nacheza, nakula, napiga story kijiweni km kawa, ngoma inakuwa nzito kuanzia km saa kumi jioni kuelekea usiku wa manane, sometimes inaanza kuwa mbaya mbaya sana mapema ya saa mbili usiku, na kuendelea hadi usiku wa manane!

Hali hii inaambatana na homa kali na kichwa kuuma sana, kukosa nguvu mwilini, kuharisha, pia sipati hamu ya kula kitu hapo ujue, sikuwa nakula vizuri hata kidogo , kila nipatapo nafasi ya kulala kidogo tu, Naota madude madude makubwa mithili ya MIlima mikubwa kwa midogo mifupi fupi hivi ikinielekea

Ma-milima hayo!!! nayoota yako yenye umbile zuri yenye rangu ya pinki lkn kwa ujio ule yanatisha, yanakuwa yameungwa na vichwa vya minyoo mikubwa km chatu,

kiwiliwili cha minyoo hiyo kimezama kwenye ardhini ya milima, yanapanua madomo na kugeuza geuza shingo zao km yanataka meza mtu hali ile nilikuwa siifurahiisi kuiona,

kwa mpango huo huo pia yapo mamilima nilio kuwa nayaota kuwa Mabaya meusi tii yenye ukoko! Mara km yanataka kunimeza yanaacha! au yanakuja yanaenda, Nastuka naamka. sijui ndiyo cerebral Malaria ilikuwa inaanza sijui! lkn niliumwa jamani mwee!

Mauza uza na maneno yakaanza kwa ndugu na Marafiki eti nimemkula mke wa mtu sitaki kusema, mara nimekumbwa na majini yenye upepo mbaya mara Babu wa bab anataka nirithi mikoba nk

Msosi hata uwe mzuri vipi nahisi km makapi tu, maji ya kunywa nahisi yana kuwa machunguuu! nikilazimisha kuyanywa natapika, mapigo ya moyo yanaenda mbiyo ajili ya kudhoofu! Pumzi kama nahisi kuna kitu kinataka kuzikata. sipumui vizuri.

Wenzio wanakula kwa kupochoa Ugali na filigisi, Mtindi, Mayai, Chips! Wana lala fofooo! usiku, Mie usiku kucha najikuna, Naamini mnajua Chloroquine inavowasha jamani, unyayoni, korodani, kichwani, nyaa nk,

Bora zimepigwa Marufuku Mjini, Vijijini bado wana tumia. nazunguka ndani km chizi halafu Mbalamwezi inakusanifu, kwa kuku mulikia mwanga kupitia kidirisha kidogo Juu ya ukuta, kwa namna unavohangaika humo ndani.

Mwili ulidhoofu sina nguvu hata za kwenda kuoga, midomo imekauka kau. sina msaada!! Asubuhi watu wanaeenda kwenye shughuli zao shambani naebaki Home Mwenyewe nimelala,

Muziki wa sauti pekee unaoingia masikioni mwangu na nausikilizia ni sauti za ndege km njiwa, fundi chuma, na sorokobwe ndge hawa wana bichwa km Panki. so walikuwa wakiimba ni kana kwamba wanashangilia Mateso yangu nayopitia , napata hasira ninawafukuza, after short period hao!! wanaanza upya!

But still na sauti za kuku Majogoo yakishindana kuwika huku na huko, sometimes lingine linasogea polepole karibu na dirisha la chumba nilimo lala, linawika kwa kishindoo! kookoo! kooo! ''astagha firuu!!! hawa kuku hawajui naumwa eee!

Mara mtetea Nae anatoka huko anakojua yeye anataga mayai, anapiga kelele za ushindi kuonyesha kuku mitetea wenzie kuwa yeye si Mgumba,

Hapa kuku mtetea huyu anaetoka taga ana wambia hao mitetea wenzie kuwa ''km walidhania ni mgumba kima kosa wasirudie tena, anawatangazia wajue anaweza taga, kuhatamia mpaka kutotoa atamwita jogoo popote alipo njoo Baba unipokee!! uniwekee kizazi kingine,

kweli bana mara utasikia jogoo linaitikia Naam naja!... hali hii ya kuugulia ndani ilinifanya kujua Lugha zote na tabia za ndege na wanyama!

Mara kidogo sababu ya dehydration niliyo i-develop , hapo nikatamani Ka-uji laini ili kulainisha koo na mdomo yangi ambayo ilisha kuwa kavu na mate mazito Mdomoni sababu ya kuto kula na kunywa kwa muda sasa, hkna wa kukuinjikia chungu cha uji, Unaumia kimoyo moyo! km ni kademu unalia machozi, mpaka yanakauka

Hapo sasa ndo uchungu unazidi kipimo unapo mkumbuka Baba mzazi, na Mama yako mzazi, kama wangekuwepo hapa karibu yako ungepona tu kwa kuhisia uwepo wao, but wako mbali kikazi. ulio nao hapo uishipo hawana mpango wala uchungu na wewe!

Utajiuguza weee! mpaka siku ya siku unapona .......

Sasa Mleta Mada wewe ilikuwaje? ilikuwa jipu au!
 
Back
Top Bottom