Nilitumia dawa ya Gono na Kaswende kumwagilia Shambani, viazi vyangu vimeharibika sana

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Mh. Waziri Bashe na timu yako nzima mimi mkulima wa viazi nakushukuru sana Waziri Bashe. Kwa ufupi nimevuna magunia manne ya viazi nikapeleka sokoni narudishiwa mzigo wote wa viazi, vyote vina wadudu.

Nilipopanda viazi hivi nilimfata Afisa Ugani, wakati vilipoanza kuota maana hata rangi ya majani yake sikuilewa. Afisa ugani alipofika shamba akaniambie niende dukani kwake akaniuzie dawa ya kupulizia, inaonekana viazi vyangu vimeathilika na ugonjwa unaitwa Kantangaze kama sio ugonjwa huo basi vitakuwa mbegu ya viazi ilikuwa na ugonjwa wa Gono au kaswende.

Jamani, nikanunua dawa ya Kantangaze, baada ya kupulizia sikuona mabadiliko kwa kuwa Afisa alishaniambia nisipoona mabadiliko nirudi dukani kwake akaniuzie dawa ya Gono au Kaswende. Sikuona haja ya kurudi dukani kwake, nilienda pharmacy na kununua dawa ya Gono na Kaswende na kukoroga vile vidonge na kumwagilia shambani kwangu.

Leo hii naenda kuvuna nilichokutana nacho nadhani umekiona kwenye picha. Nakushukuru Mh. Bashe na Afisa Ugani, Mungu atanilipia.

IMG_20230726_103311.jpg
 
Duuuuh! Wapi huko? Kwanza nilicikiri ni viazi mviringo kumbe viazi vitamu.!! Pole.

Huku kwetu hatutumii dawa wala mbolea ( kanda ya ziwa). Masika ikiisha lazima vioze maana havitaki jua kali.

Ardhi pia inaweza sababisha kuoza haraka.

Msamehe tu Bashe maana na yeye amekuta mabwana shamba ni wale wenye div4 form4.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
It is too narrow to discuss via this still photo
Anachojaribu kuelezea mtoa mada ni kuwa mbolea ya ruzuku waliyotumia wakulima wa viazi imeleta balaa kubwa kwenye mavuno ya mwaka huu (2023). Binafsi ni mkulima wa viazi, yaani kwenye ekari 1 ambayo huwa inatoa magunia 50 ukitumia mbolea ambayo sio ya ruzuku. Ila ukitumia mbolea ambayo ni ya ruzuku unapata gunia 8-10. Halafu viazi vyenyewe vina magonjwa lukuki. Hivyo, wakulima wengi wameazimia kuacha kutumia mbolea ya ruzuku kwa kipindi hiki. Ndio maana mtoa mada anamshukuru Mheshimiwa Bashe pamoja na Afisa Ugani aliyemuuzia dawa ya kuulia wadudu waharibifu wa viazi.
 
Back
Top Bottom