Wakuu, nawasogezea stori (mkasa ulionikumba mwaka 2013).
Nisisahau jadi ya watanzania, hamjambo wote? Watoto wenu hawajambo?
Wakuu, ilikuwa hivi, mwaka 2013 mwezi wa 11, kipindi hicho nikiwa nimeingia mwaka wa 3 wa masomo chuoni, wakati 'bumu' la kwanza likiwa limetoka, siku hiyo bumu linatoka lilinikuta nikiwa nje ya chuo, nilikuwa mjini.
Hivyo, niliamua kuchukua 'bumu' la matumizi ya siku kadhaa huko huko mjini.
Pale mjini (Dodoma), kulikuwa na eitiem mashine mbili za benki ya siradibi (nilizokuwa nazifahamu), huenda kulikuwa na eitiem nyingine tofauti na hizi, na eitiem hizo nilizokuwa nazifahamu zilikuwa zifuatazo.
1. Kwenye buranchi kubwa ya siradibi Dodoma (kwa kipindi hicho ilikuwa oppoziti na Nyerere square).
2. Kulikuwa na tawi lililokuwa likiitwa Chamwino, hili lilikuwa katika barabara ya kutokea Benjamini Mkapa Tower (kulipokuwa na ofisi za Tamisemi enzi hizo, sijui kwa sasa) kuelekea hospitali ya General. Hili tawi lilikuwa katikati ya ofisi hizo za Tamisemi (enzi hizo) na makao makuu enzi hizo ya CCT (umoja wa makanisa ya kikristo Tanzania.
Binafsi nilikwenda pale oppoziti na Nyerere square, lakini nilipofika, nilikuta kwenye eitiemu kulikuwa na watu wengi, kwa kuwa nilikuwa nataka kuwahi kipindi chuoni, niliona bora niende hilo tawi la Chamwino (maana mara nyingi sikuwa naona wateja wengi kwenye hilo tawi kila nilipopita mitaa hiyo.
Nilipofika kwenye hilo tawi, bahati ikawa upande wangu, nilikuta mtu mmoja tu akiwa ndani ya hiyo eitiem mashine, na wakati nafika, ndiyo muda alikuwa anatoka ndani ya EITIEM mashine hiyo.
Wakati huo, ile ananipita karibu, nikamwangalia usoni, nikamtambua. Alikuwa kichaa mpayukaji ndani ya eneo lililokuwa na vichaa wengi ndani ya mji wa Dodoma.
Alitoka mikono mitupu, lakini wakati anatoka akawa anashika shika suruwale yake kwenye rugusi hasa usawa wa babu, ishara ya kufunga mkanda, moyoni nikasema "kupatwa kwa hela/fedha/pesa".
Kwa kuwa kwenye foleni ya kusubiri nilikuwepo peke yangu, hivyo taratibu nikajisogeza ndani ya 'eitiem' ili niduroo pesa nikaspendi kwa matumizi ya hapa na pale.
Lahaula! Ile naingia ndani ya mashine, kwanza nilitekewa na pili nilibutwaika na tatu nilifadhaika, nikaanza kujiuliza, nimeingia ndani ya 'eitiem' mashine ama nimeingia cholonini. Kulikuwa na kichuguu kama siyo mlima wa kimba (mavi) na pembeni yake kulikuwa na shilingi mia ikiwa imeandikwa jina la kichaa huyo upande wa juu(head) na kukiwa na sahihi upande wa chini(tail), maandishi yalioneka dizaini kama yameandikwa kwa mkaa au makapeni.
Wakuu, pale pale niligeuza ili nitoke nikiwa nimekata shauri la kwenda kutoa pesa kule kule chuoni (kwenye eitiemu zilizokuwepo chuoni), lakini kabla ya kutoka, nikasikia sauti Mungu akiniambia kwa upole, upendo na utaratibu mwingi;
"mwanangu, unatakiwa kutoa pesa ndani ya 'eitiem' mashine hii hii, lakini kabla hujatoa pesa, zoa kwanza hilo kimba na uchukue hiyo hela hapo chini umpelekee huyo kichaa maana ni hela yake iliyodondoka kutoka suruwaleni wakati anaachia kimba"
Wakuu, nilitaka kumhoji Mungu maswali mengi sana, ila ilibidi nitii maelekezo yake pasipo kuuliza uliza.
Kwanza, niliamua kuchukua ile hela na kwenda kumpatia mwenye nayo, nilipotoka nje nikakuta yule kichaa anamalizikia kufunga mlango wa gari na ikaanza kuondoka kwa kasi sana, kumbe kichaa yule alikuwa amekabidhiwa gari kabisa (na nani, sijui), ilibidi nianze kutimua mbio kulifukuzia gari lile kwa kutimua mbio, lakini ndiyo hivyo, "unatumia damu kushindana na chombo kinachotumia peteroli", mbingu na ardhi.
Pili, nilitafuta jembe, mchanga na mfagio na kurudi ndani ya ile "eitiem" nikazoa kimba hilo, na kisha nikatoa pesa na kwenda kufanyia matumizi yaliyotakiwa kule chuoni.
Ile hela ya yule kichaa niliitunza, na kila nikienda mjini, ilikuwa lazima nipite mitaa niliyokuwa nauona kichaa yule hapo kabla, lakini mpaka nahitimu sikuwahi kumuona.
Ikabidi nimuulize Mungu hivi. "Mungu muumbaji wa kila kitu, ile hela ya kichaa nimeitunza mkononi mwangu, nimehitimu chuo, hivyo natakiwa kuondoka hapa kwa wagugu, naomba ruhusa ya kuitupa maana mwishowe itatoboa mfuko wangu"
Ndipo sauti ya Mungu, ya upole, upendo na utaratibu mwingi ikasikika masikioni mwangu ikisema,
"Itunze hiyo pesa, wakati niliouamuru, nitakukutanisha na kichaa huyo na utampatia hela yake."
Leo ni miaka 12 tokea tukio hilo, bado sijakutana na kichaa huyo ili nimpe hela yake. Hivyo, wakati wote natembea na hela hiyo ili nikikutana naye nimpatie.
Sabato njema.