Mwezi uliopita nilipata ugeni hapa kwangu, alikuja dada mmoja kwa sasa anamalizia masomo yake ya Nursing ktk chuo kimoja kilichopo Mkoani Shinyanga.
Dada huyu ni mzuri balaa na ukizingatia ana asili ya watu wa singida, nilifahamiana naye kama miezi mitatu iliyopita nikiwa SHY kikazi, nilimpenda na nilichukua mawasiliano yake, tuliendelea kuwasiliana hadi mwishoni mwa mwezi wa saba alipokuja kwangu kunisalimia.
Kama kawaida nilimpokea, tuliongea mengi sana na lengo langu kwake lilikuwa kumuoa muda si mrefu, binti huyu alinieleza kuwa ameathirika na virusi vya ukimwi na kama siamini twende muda huo tukapime, nikamwanbia twende, baada ya wote kupima ni kweli damu yake ili-react kuashiria kuwa alikuwa na vvu, alinionyesha hadi vidonge vyake vile ARV anavyotumia.
Moyo wangu ulienda mbio sana kwa sababu sikuamini macho yangu kama kweli duniani bado kuna watu wachache kama huyu atakayekueleza ukweli,
tuliporudi nyumbani alinieleza kuwa yy yupo tayari kuolewa na mm ila lazima nimkubali na ndugu zangu vile vile wamkubali kwa hali aliyonayo.
Alinieleza kuwa yeye ni bikira na alipokuwa na umri wa miaka 7 mama yake mzazi alimpeleka kwa bibi yake huko singida, bibi yake alimkeketa, inahisiwa kuwa kitendo hicho ndicho kilimsababishia maambukizi.
Alianza kuugua tezi akapelekwa hosp. akapewa dawa lkn haikumsaidia ndipo ilipoamriwa apimwe kipimo kikubwa, akagundulika kuwa tyr ameathirika.
Kwel huyo bidada ni mfano wa kuigwa