Nilipigwa na kudhurika kiafya nikiwa kazini kwangu Mkolani Sekondari

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
Siku ya jumatano tarehe 18 Oktoba 2017 hapa kituo changu cha kazi majira ya saa Nne asubuhi nilipigwa na fimbo kifuani kwangu mimi Deogratius Kisandu. fimbo hiyo ilikuwa saizi ya mpini wa jembe na kunihatarishia kifua changu na hili tukio limefanywa na mwalimu mwenzangu wa mkolani sekondari, hata hivyo mwalimu mwingine alinifata ofisini na kunipiga ngumi huku hasemi chanzo cha tatizo. Kimsingi nilimwandikia barua Mkuu wa shule kufafanua jambo hili lilivyo kuwa maana hata yeye mkuu wa Shule wa Mkolani Sekondari alikuwepo wakati napigwa na walimu wengi walishuhudia wakiwemo wanafunzi wetu waliokuwa nje.

Nilifika Polisi tarehe 19 Oktoba 2017 na kuchukuwa PF 3 kwa ajili ya matibabu na nikafanyiwa matibabu ya awali, na nilirudisha fomu ya PF3 kituo cha Polisi Nyegezi stand siku ya jana jumatatu tarehe 23 Oktoba 2017. Hata hivyo nimemwandikia Mkurugenzi wangu kama Mwajiri wangu kumpa taarifa juu ya Vurugu hizo ambazo hazikuwa na maana yoyote ile, barua hiyo nimeifikisha Halmashauri ya jiji la Mwanza leo mchana tarehe 24 Oktoba 2017.

Taarifa niliyonayo ni kuwa baadhi ya walimu wenzangu wanatumika na wanasiasa na mmoja wa Kigogo Ikulu kwa lengo la kunidhuru mimi Deogratius Kisandu na wameahidiwa vyeo kama nitakufa au kupewa Ulemavu wowote ule.. Mpaka sasa afya yangu sio nzuri sana japo najitahidi kujikaza kiume na sina pesa yoyote ya kuendeleza matibabu ya afya yangu. Majina ya walimu wahusika nimeyataja katika nyaraka husika. Kwa kuwa naipenda Tanzania naomba kuwasilisha taarifa hii kwa umma wa Taifa la Tanzania.

DEOGRATIUS KISANDU.
 
This is the highest point of alienation and it seems you are about to commit suicide.. Hataree
 
dah! kisandu una mini had I ikulu ikuogope? kwa ulivyo Nazi kuna mpumbavu unadhani anakuelewa? Fanya kazi mwalimu acha kujitafutia umaarufu wa kipuuzi! ishi vizuri na wenzio, acha ujuaji, watakukata makofi na utaishia kupost hapa JF
 
Back
Top Bottom