Nilioneshwa tukio la Oktoba 7 Hamas kushambulia israel mwezi mmoja kabla

Mashaurijr

JF-Expert Member
Oct 8, 2016
885
1,363
Nilishawahi kuletaga thread ya mimi kuwa na hisia zinazonichanganya na wakati mwingine nazitumia kutabiri matokeo ya jambo fulani.

Kama mwezi mmoja kabla ya tukio la October 7 mdogo wangu wa mwisho alienda Israel miongoni mwa vijana karibu 200 waliopelekwa na serikali kupata elimu kwa vitendo na mpaka sasa yupo huko.

Sasa baada ya kumaliza mitihani ya semister ya mwisho alikuja tukawa wote ninapoishi. Kama baada ya siku tatu usiku niliota jambo la kutisha niliona mdogo wangu akiungua moto akilia sana na kuteseka
Alafu nikapata ghafla hisia kuwa mdogo wangu kuna maovu alitenda hivyo asipotubu atakufa na pia anatakiwa akae mbali na mimi kama atakuwa mbishi.

Nilivyokuwa naota nilikuwa na weweseka hata kulipokucha aliniambia usiku kuwa nalia na kujizungusha sana.

Nililazmika kumwambia ukweli nilimwambia nilichoota na maonyo yaliyonijia kuwa asipotubu atakufa. Sasa mimi kwenye kuongea nilijichanganya nikamwambia sijui ni ushirikina gani ushashiriki mpaka haya yananijia . Akashikilia nimemwita mchawi nikajitetea na nikachukua hatua kumwambia aondoke na atubu asipotubu yatakayompata sitahusika wala kuumia maana nilishampa tahadhari . Alichukia na kuniambia hata kaa aongee na mimi tena nikamjibu sawa . Siunajua tena tabia za last born. Hapo tayari alikuwa kwenye hatua za mwisho kwenda Israeli . Basi siku ya mwisho alinitafuta na kuniambia ametekeleza niliyomwambia na anaomba baraka na sapoti ya fedha kiasi basi nilifanya hivyo akasafiri na kufika salama .

Tukio lilipotokea ilikuwa aende kushangaa tamasha lililolengwa na shambulizi yeye na marafiki zake kadhaa ila mwishoni kabla hawajatoka walipewa majukumu waka ghairi. hivyo aliponea kwa staili hiyo na kwa kutii maono niliyoona akatubu

Huu ni ukweli niliomtamkia nilioona
Kabla tukio halijatokea . Asingetubu angekuwa miongoni mwa vijana wa kitanzania walioaga Dunia.

Sio kwamba walioaga Dunia walikuwa waovu hapana ila huenda mdogo wangu alipewa nafasi ya kuishi kutimiza mambo ambayo Mungu anataka yatimie ndio maana akatoa tahadhari mapema na kutoa chaguo kuwa asipojirekebisha basi atatumiwa mwingine kwenye huo mpango wa Mungu hivyo atakufa .

Huenda hii inatokeaga kabla matatizo mengi kama ajali hayaja tokea. Huenda kuna watu au mtu anapokea maono au ishara ila anashindwa kuzitafsiri mapema na kuchukua hatua na kupelekea majanga kutokea
Saa nyingine ni kuhofia watu hawata mwelewa .

Mfano abiria mmoja asimame kwenye basi aseme hili basi litapata ajali mbele tusali na kuomba ndio tuende wangapi watamwamini
Sawa siku ya kwanza akaaminika gari likapita salama . Wangapi wataamini bila ile sala ingetokea ajali . Je wakati mwingine mtu mwingine aseme je ataaminika ?

Niliona maono ya shambulio la hamas Israel October 7
 
Itakuwa ulifanyia kazi ndoto Yako kwa maombi na Mungu alikuonesha kwa sababu
Kinachoendelea kwenye hiyo vita hakitazamiki
 
Hata mimi nikianza kusema kuwa niliona jambo hilo hilo, basi tutaonekana waongo tu.

Ukweli ni kuwa, ukitaka watu wakuamini tabiri jambo husika kabla ya kutokea. Siyo linatokea ndipo useme nililiota. Tutakuona unatembelea tu upepo.

Kwa lugha nyepesi, hizi ni ngonjera. Uwe unaweka maono yako mapema, tutakupa credit.
 
Sawa mkuu mi nahitaji kujua wewe mi nabii, mlokole, mganga au uns mizimu na machale na ni mara ngapi imetokea ?
 
Itakuwa ulifanyia kazi ndoto Yako kwa maombi na Mungu alikuonesha kwa sababu
Kinachoendelea kwenye hiyo vita hakitazamiki
Watu wamekufa sana kuliko hata hesabu vita vikiisha ndio hesabu itapatikana miili mingi bado ipo kwenye vifusi
 
Hata mimi nikianza kusema kuwa niliona jambo hilo hilo, basi tutaonekana waongo tu.

Ukweli ni kuwa, ukitaka watu wakuamini tabiri jambo husika kabla ya kutokea. Siyo linatokea ndipo useme nililiota. Tutakuona unatembelea tu upepo.

Kwa lugha nyepesi, hizi ni ngonjera. Uwe unaweka maono yako mapema, tutakupa credit.
Mdogo wangu na familia yangu ndio mashahidi wa hili maana niligombana na mdogo wangu na kumfukuza kitu ambacho kiliwashangaza na kumwambia asipotubu ataangamia . Sasa alipoenda na kutokea lililo tokea basi familia ndio ikashtuka hee .
Kumbe nilichukua hatua sahihi. Nisinge mwambia na akatekeleza unafikiri ingekuwaje?.
Huenda kuna ishara nyingi hutokea kabla mtu hajafa au ajali kutokea sema hazizingatiwi sana.
Na kulazimisha sana baada ya vikwazo kutokea .

Mfano unataka kusafiri alafu ghafla asubuhi mtoto anaumwa wewe unalazmisha kusafiri sometimes ni ishara
 
Mkuu eb nitabirie Mimi chochote
Mimi siwezi kutabiri. Inatokea tu napata maono ya kabla jambo kutokea au matokeo baada ya jambo flani kutokea naweza kujua hatima yake . Mfano mtu akiwa mgonjwa haswa watu ambao ninawapenda sana . Natumiaga hisia kujua huyo mtu atakufa au atapona na ninapotamka ndicho kinachokuwa . Sitamki tu natumia hisia nikiwa na amani na nikaweka imani basi inakuwa hivyo na hii ilianza utotoni.
 
Back
Top Bottom