Niliokoka baada ya kusikiliza Kwaya ya Makongoro na Uliyankulu!

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
Wapendwa katika Bwana

Leo ni jumapili na nimeona ni vema nitoe ushuhuda wangu jinsi nilivyokata shauri kumfata Yesu!

Nilikuwa msikilizaji mzuri wa nyimbo za Kwaya maarufu ya Makongoro na kwaya ya Ulyankulu nafikiri kutoka Tabora samahani kama nimekosea spelling,

Nilichogundua ni kila nikisikiliza nyimbo zao hasa kama nipo peke yangu machozi yalikuwa yakinitoka na nilikuwa nikilia sana.

Nilienda moja kwa moja kwenye kanisa la Evangelistic Assemblies of God wakanipokea na kuniongoza sala ya toba.

Kuanzia pale nilianza kujifunza neno la Mungu kwa undani na kugundua kumbe Biblia ni kitabu cha ajabu mno na kina mambo mengi ambayo pamoja na kwamba mimi ni mtu mzima na Mkristo niliyekuwa nasali kila jumapili nilikuwa siyajui.

Mungu alianza kujidhiirisha ndani yangu na nikajiukuta nipo karibu sana na Mungu kiasi kwamba hakuna jambo lolote linaloweza kunitokea ambalo silijui,

Pongezi zangu za dhati naomba ziwaendee popote pale walipo waimbaji wote wa kwaya hizo na viongozi wao na kanisa lao,kwa kweli kazi yenu ni kubwa mno japo siwajui lakini ujumbe wenu umejaa upako mkubwa mno.

Nimemwomba Mungu anisaidie niwatembelee siku moja popote pale mlipo,vile vile natamani niwe mmoja wa wadhamini wenu,naomba ujumbe huu uwafikie popote pale mlipo,Mungu awabariki kwani kazi yenu mnayofanya mtalipwa hapa hapa Duniani!
 
Inanekana hukuwa unasali hapo EAGT kabla ya kuokoka,nini kilikufanya ukaenda huko na usiende kwenye kanisa lako ambalo ulikuwa unasali kabla?

Mpendwa
hilo ni swali gumu sana,lakini kumbuka Roho Mtakatifu ndiye anayefanya kazi yote ndani yetu,Makongoro kwaya walipanda mbegu ndani yangu Roho mtakatifu akamalizia kazi iliyoanzishwa ndani yangu,kwa kweli katika watu waliokuwa wakidharau makanisa ya Kilokole basi nilikuwa namba moja
 
Mungu akubariki zaidi. Achana na habari za ulikuwa wapi kabla, chamsingi kwako ni ukristo wako. Mguso wa Roho mtakatifu ni tofauti kwa kila mmoja wetu na kila anapoguswa huwa na sababu. Usijari kuhusu ulikuwa wapi. Hongera kwa ushuhuda
 
Kwanini unadai swali gumu wakati alietenda ni wewe?
Kwa hiyo roho mtakatifu ndio alikuongoza uendehuko EAGT?
 
Huwezi kuona tatizo ambalo inazaliwa kila siku kwa watu ambao wanahama madhehebu

By the way,kimsingi hakuna sababu ya kuhama dhehebu pale ambapo unapoamua kuishi maisha ya Kikristo [kuokoka]
 
Kwanini unadai swali gumu wakati alietenda ni wewe?
Kwa hiyo roho mtakatifu ndio alikuongoza uendehuko EAGT?

kwa hakika pressure niliyokuwa nayo kanisa langu la Roma lisingeweza kunipa msaada wa kiroho,nataka ujue tunaongea mambo ya rohoni zaidi ambayo ni vigumu kuyajua kama unaishi maisha ya kimwili pekee
 
Weye umeona hizo kwaya mlizoimba hazina soko, sasa unakuja na gea mpya unajifanya zimekuokoa.

Siku hizi pamezuka magari ya kwaya zinapiga mitaani na kubembeleza watu kununua cd.

Pole sana, umepotea stepu.
 
rosemarie

"rosemarie" karibu sana kwenye taasisi yetu' utapata UPAKO ZAIDI, kwani tunatumia vifaa mbali mbali kusambaza upako kwa watu mbali mbali...,
31.JPG
 
Last edited by a moderator:
kbm! yote hayo siyo ya muhimu tena kwangu,nina kitu cha thamani ndani yangu kuliko hizo mali ziharibikazo,hazina tuliyo pewa na Kristo ndiyo muhimu zaidi
 
Kulikuwa na dada m1 jamii forum,alikuwa anapenda kuwaingiza watu king kekundu kekunduuuu.
 
kwa hakika pressure niliyokuwa nayo kanisa langu la Roma lisingeweza kunipa msaada wa kiroho,nataka ujue tunaongea mambo ya rohoni zaidi ambayo ni vigumu kuyajua kama unaishi maisha ya kimwili pekee

Najua unachozungumza na ndio maana nimekuuliza

Kanisa la roma nalifahamu,lakini sijui ni msaada upi ambao wewe uliona huwezi kupewa hata kabla ya kuutafuta kwanza!
 
Najua unachozungumza na ndio maana nimekuuliza

Kanisa la roma nalifahamu,lakini sijui ni msaada upi ambao wewe uliona huwezi kupewa hata kabla ya kuutafuta kwanza!

Kaka hao wapo wengi, usishangae hilo kanisa alilookokea sasa sio muumini tena hapo, keshaamia kwa mchungaji mwingine, na unakuta keshapita msururu wa makanisa
 
kwa hakika pressure niliyokuwa nayo kanisa langu la Roma lisingeweza kunipa msaada wa kiroho,nataka ujue tunaongea mambo ya rohoni zaidi ambayo ni vigumu kuyajua kama unaishi maisha ya kimwili pekee

Nilikupa hongera bila kujua unakoenda. Ni kitu gani cha ziada umepata huko? Anyway kuna vitu pia hutavipata eagt, ukivipata kwingine ututaarifu pia wakati unahama.
 
kwa hakika pressure niliyokuwa nayo kanisa langu la Roma lisingeweza kunipa msaada wa kiroho,nataka ujue tunaongea mambo ya rohoni zaidi ambayo ni vigumu kuyajua kama unaishi maisha ya kimwili pekee

Mpendwa,
Hebu tuwekee na sisi hizo nyimbo (if possible) labda zinaweza kutupatia upako na kututoa shimoni..
 
Huwezi kuona tatizo ambalo inazaliwa kila siku kwa watu ambao wanahama madhehebu

By the way,kimsingi hakuna sababu ya kuhama dhehebu pale ambapo unapoamua kuishi maisha ya Kikristo [kuokoka]

Inategemea ni dhehebu gan ulipokuwa mwanzo mengine hakuna upako. Hongera mleta mada
 
Back
Top Bottom