Nilimwona Mbongo anakuja na.....

Nilimwona Mbongo anakuja na.....

mkurugenzi1

Senior Member
Joined
Mar 22, 2009
Posts
122
Reaction score
28
Imetumwa via WhatsApp...

Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.

Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.

Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.

Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.

Wakaingia msituni kila mtu njia yake.

Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.

Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala nini... alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.

Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, “Vipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?”

Mkenya akamjibu: “Mkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!”

Dah kungekuwa unaweka Voice basi kicheko ungeki Delete leo hapa duh mkuu hii kali naona Wachina watakuwa waliishiwa nguvu hata za Ku shot duh Tikiti maji sivuti picha The!Teh!Teh!
 
nimechekaje daah cpati picha hahahahaaaaa kwikwikwiiiiiii mmhmmhmmm bwaaaaaa kwaaaaaa
 
Alipofika mbongo yale matikiti yakaonekana yamepasuka kumbe ndani kuna unga walipo mhoji kumbe alikuwa ni r i z o n e, ikabidi babayake aitwe, muafaka uka wekwa TZA ikawekwa rehani. r i z o n e akaachiwa huru. wabongo tunatisha kwa ujanja
 
Mungu ibariki Jf na watu wake!

Yani nimechekaaaa sanaaa!!!!!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wewe mwongo mbona mbongo alikuja na Nanasi. Teh tehe...

huyo atakuwa wewe huyo duh kungekuwa katika hao watatu wote ni wabongo basi mmoja ndio angekuja na hili tikitimaji mwengine angekuja na nanasi lako mwengine na Fenesi.
 
Imetumwa via WhatsApp...

Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.

Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.

Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.

Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.

Wakaingia msituni kila mtu njia yake.

Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.

Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala nini... alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.

Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, “Vipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?”

Mkenya akamjibu: “Mkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!”

Haaaahaaahaaa!! Wabongo noma....iko tamu tikiti maji.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom