mtani sooo ulifika mpaka pande za kumpitimbi! hongera sana mtani ukija safari nyingine nitafute nipo kijiji kinachofuta bada ya mpitimbi. utakuta tumekutayarishia pombe inaitwa MYAKAYA brewed using mayau (mihogo). msosi utakuta ugali na namgujulu(mboga ya manyonyoli) utauliza huko huko manyonyoli ndo nini. matunda mtani yapo ya kumwaga kuna masuku, madonga, machungwa mapapai mapwete mpaka hapo mtani nadhani utaridhika na kuomba upewe mdala(mchumba) wa kugega(kuoa) hahahaaaa
kaka we kucheka mpaka utekenywe?
Hii imenikumbusha ugomvi mkubwa uliotokea kati ya dreva moja mwenyeji wa mikoa ya bara na mngoni moja. Ni kwamba mngoni alitoka hospitalini yeye mkewe na mtoto mdogo njialikapita lori likiwa na dreva na utingo wake. Kwa kumhurumia mama na mtoto utingo alimpisha sehemu ya mbele yeye akapanda nyuma pamoja na jamaa wa kingoni. Baada ya kuwafikisha sehemu walikuwa wakienda baada ya kuteremka chini yule mngoni kwa nia nzuri kabisa alikwenda kumshukuru dreva kwa msaada aliowapa .Tatizo lilikuwa kwenye matamshi yake ambayo yalitafsiriwa vibaya na dreva. Alisema hivi, nanukuu"bwana dreva asanti sana kwa kuntia nyuma ya gari na mki wangu na mtoto ukawatii mbele ya gari . Asanti sana bwana
Katika pitapita zangu mitaa ya Mpitimbi nilikutana na jamaa yangu Ngonyani nami kwa heshima yangu ya kinyamwezi nikamsalimia shikamoo mjomba,akanijibu "Malihabi mjombi ,hujambi?"Akimaanisha marahaba mjomba hujambo.
Mimi huko huko nilisikia mama mmoja akiulizwa na mzee 'uni uhakika na unichokinena? Nasemi hivii uniuhakika na unichokisimi? Hii ilikuwa ni baada ya kumpa mzee wa kingoni taarifa ambazo alikuwa haziamini.
Katika pitapita zangu mitaa ya Mpitimbi nilikutana na jamaa yangu Ngonyani nami kwa heshima yangu ya kinyamwezi nikamsalimia shikamoo mjomba,akanijibu "Malihabi mjombi ,hujambi?"Akimaanisha marahaba mjomba hujambo.