Nilimkosea kumwomba msamaha nashindwa...Nahisi atanitesa!!

Nilimkosea kumwomba msamaha nashindwa...Nahisi atanitesa!!

Rabboni

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2015
Posts
1,193
Reaction score
1,731
Wakuu heshima kwenu!
Nimejikuta napata wakati mgumu sana kukutana na mtu ambaye niliwahi kumsumbua hata kujaribu kumtishia kwa namna moja...

Kuna dada mmoja, ambaye tulifahamiana kwenye workshop moja hivi mwanzoni mwa mwaka huu, ilikuwa inafanyikia mkoa wa Tanga nilikuwa nae kiukundi kimoja katika kazi na kwa bahati nzuri mimi na huyu dada tulikuwa tunatoka mkoa mmoja.
Offcoz ile kazi ilikuwa ngumu kidogo na ilihitaji akili na nguvu kuifanya!! Sasa huyu binti akawa anatega sana, na unakuta kazi zote nafanya mimi, ni binti mrembo! na kwa kweli anajua kutega kazi. Workshop ilikuwa ni ya muda mrefu kidogo, almost 4weeks!.

Kazi ikaendelea but ilifika mahali ikabidi nimbane binti ili afanye kazi, na nikajaribu kumlimit hata kwenye maswala ya muda, muda wa kula na muda wa mapumziko.

Hali ilimwia ngumu kidogo na ilifika kipindi akaamua kutofautiana na misimamo yangu katika kile kikundi chetu! akawa anawaambia members wengine kuwa mimi namdharau sana namwona legelege!! Mrembo kila akiniona lazima aongee maneno ya kulalamika na kusema namwonea, nilianza kumdharau kimtindo so kuna baadhi ya sehemu ilibidi nimpuuze na nilijaribu kuwaambia baadhi ya wadau pale wasimsaport, kuna kazi nyingine ni za serikali lakini ni ngumu.

Kwenye hiyo workshop tulikuwa tunalipwa 80,000/= per day malazi na meals excluded. Kadri siku zilovyokuwa zinaenda kazi ikawa inaongezeka ugumu, hapo ilibidi watu tuwe serious kweli kweli, kulala saa 5 usiku kuamka saa kumi na moja asubuhi.

Sasa msaada kwa huyu mrembo ukazidi kupungua kwa wale members wachache waliokuwa bado wanampampa support, sasa ikabidi aliamshie kwangu seriously kwa sababu alinichukulia mimi kama chanzo cha yeye kukosa msaada na mara nyingi akawa anatishia kujitoa kwenye ile project!!

Asubuhi moja mdada ikabidi ashuke tuu, aongee na mimi vizuri ili mambo yaende, nikaamua kukaza ili kazi iende na tuimalize kwa wakati.
Hakupenda nilivyomkazia, kuna wakati nilikuwa namaliza mapema nampiga tough kimtindo!!
Wakati tunakaribia mwisho hee, mrembo akaanza kuniletea kashfa sikupenda ile hali, nilimjia juu sana kidogo nimkate vibao mbele za watu! bahati nzuri mratibu alikuwa karibu na ndiye aliyeokoa kile kisanga.

Kazi ikaisha kila mtu akasambaa kivyake!!
Sasa leo mchana nakutana na yule mrembo ofisini afu ndiyo mkuu wa idara (sijui kapandishwa lini cheo)...

Afu kuna kaworkshop kengine tena kanguvu kuliko kale ka kwanza na huyu binti kwa namna moja au nyingine anashiriki kwenye kuratibu!!
Sijui itakuwaje yaani huyu binti sasa anapower regardless kazi yake alikuwa anafanya kivivu sana!!
Nimeshindwa ku define hali yake juu yangu kwa sababu hatujaongea sana zaidi ya salamu na mambo ya kazi.
Hapa wakuu mnashauri nini? niuchune tu, au nimwombe msamaha kwa kujaribu kumpiga? ili mambo yaende sawa...
Najua nilimkosea kwa kushindwa kutuliza hasira zangu kwake!! Nahisi anaweza kunisumbua na nikatemana na kazi yenyewe, japokuwa ni deal la maana...
 
Kama kweli roho yako inaona ulimkosea then ongea naye ila kama unahisi ulikua sawa na actions zake then achana naye! Mbona simple tu
 
kwani kosa lako ni nini adi uombe msamaa kijana jiamin bhana cheo kitu ganii ad nzi wana vyeo vyao huko....

najiamini aisee, ile kujaribu kumpandishia labda!! alitia hasira lakini, alichukulia uzuri wake kama silaha yakusaidiwa kazi sasa kwangu ikawa tofauti...
 
Usimuombe msamaha kwanza ww kausha ujifanye haujui kitu ila akikumbushia ndio umuombe msamaha kwa sasa ww piga kazi kwa kwenda mbele
 
hamna kosa apo yani ningekua na kampuni we ungeshapewa ukurugenzi...

swali ni je ulimpandishia kwanini?! kama ni sababu ya utegezi wake unaomba msamaha wa nini? ye ndo akuombe msamaa alaah....
cheo cha mtu kisikuinamishe kichwa afu uwaache wakipandie kwa juu wasimame...

ha ha ha nimekusoma mkuu, jumatatu nitakuwa tena ofisini kwake bado kuna mambo ya kikazi sijayakamilisha!!
leo muda ulikuwa umeenda sana.
 
Usimuombe msamaha kwanza ww kausha ujifanye haujui kitu ila akikumbushia ndio umuombe msamaha kwa sasa ww piga kazi kwa kwenda mbele

good advice! jumatatu nitakuwa tena ofisini kwake!!
 
Msalimie usionyeshe tofauti yoyote ile ht yenye kimoyomoyo anakukubali ila ni vile tu saga za cheo kikubwa, atakuelewa tu muda si mrefu.
 
Hujakosea kitu ile ni kazi na ili kazi ifanyike inabidi muwe serious xo kwa upande wngu coni kama umekosea msalimie na uendelee na shughuli za kazi
 
Jifanye Kama Nothing Happen Akikusalimia Mchangamkie Ila Uwe Na Kias Usije Kuonekana Unajipendekeza Sababu Ya Cheo Kikubwa Zaidi Jiamin Usianze Kujiongelesha Kuomba Msamaha Kabla Ye Hajagusia Itakupunguzia Credit Zote Atakushusha Na Umbea Wa Kazin Unavyonoga Akimwambia Shost Yake May Be Utapaona Pachungu Job Just Act Like A Man
 
Mkuu we piga kazi ila tu usionyeshe utofauti wowote ule juu yake..Kila la kheri.
 
msimamo unapimwa hapo..komaaa huna kosa la kuomba msamaha
 
Tatizo ni nafsi yako inakusutaa au kuna jengine ?
 
Deep down wanawake wanawakubali mno wanaume kama wewe wenye msimamo,so the choice is yours.
 
Mwanaume hawekahi rohoni ________ Hata huko juu alipo akizingua piga tu hakuna namna
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom