elyza
Senior Member
- Oct 9, 2016
- 155
- 327
Pole na shughuli za siku wakuu.
Nilikuwa na mchumba ambaye tumedumu nae kwa miezi tisa. Pia uchumba wetu ulishakuwa wazi kwa wazazi wa pande zote mbili, japo bado hakikuwa kimefanyika chochote katika kuhalalisha mahusiano yetu.
Mwezi uliopita nilikwenda nyumbani kwa mchumba wangu bila kumtaarifu, nilikuta mlango umerudishiwa tu, nikataka kuingia mama mwenye nyumba akanifanyia ishara ya kuniita kwa mkono nikaenda kumsikiliza.
Alichoniambia eti nirudi nyumbani nisiingie kwani mpenzi wangu hajisikii vizuri na ameagiza mtu yoyote akija asiingie. Nikatafakari nikaona kama mtu hajisikii vizuri kwanini nisijue shida yake.
Nikamuitia yule mama na kumshukuru kwa taarifa lakini nikaingia ndani, kweli sebuleni hapakuwa na mtu.
Nikasukuma mlango wa chumbani na kuingia. Sikuamini macho yangu nilichokiona inauma sana nilimkuta mpenzi wangu akifanya mapenzi na binti wa mama mwenye nyumba wake.
Niliona hakuna haja ya kugombana kwakuwa hakuwa mume wangu nilichomwambia aendelee na huyo mimi basi tena.
Siku iliyofuata alikuja home alipogonga geti nilichungulia nilipotambua kuwa ni yeye nilimuuliza anasemaje.
Alinijibu kwa dharau kwamba amekuja kunipa taarifa kuwa yule niliyemkuta nae ndiye chaguo lake mimi sina hadhi ya kuwa nae sikuwa na maneno mengi nilimjibu kifupi asante kisha nikafunga geti nakurudi ndani.
Nilipata uchungu sana nililia hata kesho yake sikuweza kwenda kazini
Nikaamua kumtoa moyoni na kwakweli nilimtoa kabisa, nilichukua zawadi zote alizonipa nikamtuma mdada wa kazi ampelekee. Nikajua ndo mwisho wa mawasiliano.
Baada ya wiki kupita akajirudisha nimekataa na simtaki sasa anatishia kuniua nimeripoti polisi na nimepewa RB.
Je, hapo mimi nina makosa?