mkuu itakuwa vigumu kupata ushauri wa moja kwa moja kwa sababu,suala la kukoseana kwenye mapenzi ni jambo la kawaida,ila linategemea na mkosewaji,akiombwa msamaha,atasamehe na kusahau? kuna kusamehe,na kuna kusamehe na kusahau...
Mkisameheana,mara nyingi huyo mtenda kosa huwa hathubutu kurudia ujinga kama ule wa mwanzo.
Na zaidi ya hapo,we ulishatoa adhabu kali kwa hao wote,unashindwaje kumrudia mkeo? Na pia uhusiano uliouanzisha na huyo shoga yake,hata uwe mtamu vipi,jua tu kwamba si uhusiano sahihi kwako.
Kila la heri...