Nilimfadhili huyu mwanamke lakini aliyoyatenda ni ajabu

EL ELYON

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
1,563
1,886
Wakuu mmebarikiwà Sana na Mungu WA mbinguni hakuna laana huu yenu.

Wakati NIPO chuo mwaka WA Kwanza nilipata mawasiliano na dada mmoja wa kiha ambaye tulipotezana tukiwa a level alihama shule nilitokea kumpenda. Ila ye alikuwa chuo kingine mkoa mwingine AMBAKO huko alipokuwa ndo kulikuwa nyumbani.
SA wakati WA likizo alikuwa hapendi KWENDA kwao yaani atoke dar aende tabora Kwa madai kwamba mama yake anazingua Sana.
Kwahiyo nilipokuwa nikirudi home likizo naye akifunga chuo anakuja nilipokuwa kwani nilikuwa naishi KWENYE nyumba ya bro peke yangu bro alikuwa mkoani huko kikazi na familia yake.

SASA kuna siku tukiwa likizo bro alisema anakuja na familia yake likizo mmmh nikamwambia Yule mdada aende Kwa ndugu zake maeneo ya mwenge akakataa kwamba nao huwa hawaelewani nikapata akili kwamba basi Kwa kuwa nyumba ya bro NI kubwa Sana na hawanaga tabia ya kuja room kwangu nikamwambia Yule mdada watakapofika wenye mji we ukae ndani Tu yaani room ustoke mpk nikupe mwongozo ukizngatia Choo kipo ndani. Mambo ya msosi nilipata akili kwani walikuja na beki 3 nikajenga naye urafiki kabla ya kupeleka Chakula huko meza kuu basi sahani moja anivushie nipeleke room ndo ukawa mchezo huko takribani wiki 3.
Sasa bro alikuwa na Ka shemeji kangu hako kahaya Roho mbaya Sura ngumu kwelikweli aisee. Kalikuwa hakataki sikia mlango umebamizwa iwe Kwa bahati mbaya au makusudi lazma kalalamike ukizngatia Ile NI nyumba yake na mumewe Mtu lazma UWE mpole Tu ufate maelekezo. Kalikuwa kanambonda beki 3 na mwiko misiri ya kuua nyoka.

SikU moja usiku Kila Mtu akiwa room kwake mdada niliyekuwa naye nikampa mwongozo WA kutoka kidogo nje apunge upepo Ile anatoka akabamiza mlango puuu. Mmmh nilimind maana ye anajua kabisa mle yumo kimagumashi na nilishampa maelekezo tatzo nini eeeh naye si akanimind hapo tumerudi room aisee hasira zilinipanda eeeh si mdada kaanza kuongea Kwa sauti kabisa alivyo mjinga mle room kwangu kulikuwa na kopo la cd kaanza kuvunjavunja zile cd kama haitoshi kashika deki yangu kaanza igonga gonga chini puuu puuuu kweli niliishiwa pozi kabisa nilishindwa nimpe adhabu Gabi maana ningesema nikurupuke kutoa adhabu uwenda bro na mkewe wangesikia wakaja.

Kweli nilimuacha ksho yake asubuhi Sana bro na mkewe walitoka nilichoamua baadae na Mimi nilitoka na mdada niliyekuwa naye ndani tumezunguka jijini weee lengo likiwa ifike usiku nimwambie hawezi ingia pale Kwa bro so aende Kwa ndugu zake mwenge kweli ikifika usku nikamwambia nenda Kwa ndugu zako si unajua mazingira ya pale. Akakubali mi nikasepa zangu Kwa bro eeeh ile naingia ndani nashangaa Yule mdada ananipigia simu anasema kafika pale Kwa ndugu zake wamemtimua kwahiyo vp aje na ukumbuke usiku alinifanyia fujo aisee.

Nikamwambia hapana NGOJA nakuja nikukute stand huko. Kweli niligeuza tukakutana tukaenda mahali tukapata Chakula Kisha nikatafuta lodge tukalala. Hapo mnaweza sema Kwa tukio alilofanya why sikutemana naye hapana mi nilimpenda na nilijitoa kwaajili yake niliamua kumsamehe Tu.

Pili kuna siku tukiwa palepale KWENYE nyumba ya bro tena nakumbuka siku hiyo walikuja ndugu zangu wanne SA nyumba ina vyumba vitatu Ila vyumba viwili ndo vilikiwa na kitanda ukiacha master room ya bro Tu.

Usiku niliwaomba wabanane Tu KWENYE room moja na kitanda kimoja mi nilale na yule mdada. Eeeh usiku tukazinguana na Yule mdada SA KWENYE kubishana bishana baadae nikaamua kunyamaza Tu ye akiwa amekaa chini mi nikaamua kulala eeeh kumbe mwenzangu ananivizia nipitiwe usingizi si akakurupuka pale chini akachukua peni Aina ya Bick akanichoma nayo tumboni mpaka ikakatika nilikuwa nimelalia mgongo huku nmejifunika shuka zito ndo ikawa ponapona yangu usiku ule sjui kama angepata akili ya kunitoboa macho ingekuaje.

Aliponichoma vile akatoka nje anakimbia mpka ndugu zangu wakashituka nikawatuliza baadae alirudi akalala nilimnyamazia Tu Ila sikulala kabisa usiku ule.

Tukio lingine tukiwa tumemalza chuo niliamua KWENDA kupanga rasmi usiku mmoja tuliznguana eeeh mdada Acha aanze kuniporomoshea matusi mazto mpaka watu majirani wakawa wanasikia natukanwa matusi kama shoga, msenge, fala NK.
Hapa kuna raia wanaweza sema labda nilikuwa sina hela NI kweli sikuwa na hela nyingi nilikuwa na hela ya Kula na kulipa Kodi wkati mwenzangu hakuwa hata na Mia maana ndo tulikuwa tumemalza chuo Tu wakati huo nilifungua biashara maeneo ya home.

Tukio lingine tulipata Mtoto WA kiume naelezea baada ya Yule Mtoto kufariki akiwa na miaka miwili. Aisee mpaka Leo nashangaa Yule mwanamke huko alipo anatangaza Kwa watu nilimuua Mtoto wangu na hasemi nilimuua vipi Ila anasema Tu nilimuua cha ajabu siku moja nilitoka kazini mapema maana huwa nawahi kabla yake nikamkuta Mtoto kalala baadae akawa ameamka akawa kabebwa na binti aliyekuwa anatusaidia Kazi mi nilikuwa najiandaa kutoka kweli nilitoka nikamuacha Mtoto Yuko na Yule binti wanabembelezana Kula.

Nikirudi usiku kwenye Saa nne nikamkuta Mtoto analia kabebwa na mama yake nikamuulza shida nini akasema amekuta analia jioni Ila anamuona kama ana shida ya tumbo nilimind Sana nikamwambia kwani hakumpeleka hospital akajibu majibu ya kipuuzi Tu by Saa nane usiku naona Hali bado ileile tukampeleka hospital ikaonekana ana upungufu wa Damu akalazwa maana pia alikuwa na shida ya sickle cell.

Akikaa nae hospital takribani wiki Kwa bahati mbaya alifariki Mtoto wangu. Cha ajabu Yule mdada akawa anatangaza Kwa ndugu zake na baadhi ya ndugu zangu kwamba Mimi ndiye nimemuua Mtoto na akiulzwa hasemi kwanini anahisi hivyo Kwa kweli mpaka Leo najiulza kwanini Yule mdada alikuwa anayasema Yale maneno naumia Sana.

Cha ajabu toka tulipomzka Yule Mtoto hakuwahi kukanyaga kaburini kwake mpaka nahama kikazi huko DSM to mkoani taarifa zilizopo HAJAWAHI kanyaga huko kaburini sjui tatzo NI nini Ila ndiyo Hali halisi.

Wakuu NI hayo mwenye maoni karibu mwenye povu au matusi pia karibu.

NB: mdada tulishaachana miaka sasa sjui kama Alishaolewa ama vpi Ila mi nilishaoa kitambo kidogo.
 
Mbona story ni kama haijaisha, Hadi leo bado Upo nae au Mshaachana, Na Nini Kinaendelea kati yenu? Huyo Hukupaswa hata kuendelea nae Tangu alipoanza kuonyesha makucha yake
KuhuSu kuachana mbona nimeeleza hapo hata sjui kama Alishaolewa huko alipo nasimulia kidogo kidogo mkuu maana bado yapo mengi tasema maana alinitenganiaha na ndugu na rafiki zangu karibia wote
 
KuhuSu kuachana mbona nimeeleza hapo hata sjui kama Alishaolewa huko alipo nasimulia kidogo kidogo mkuu maana bado yapo mengi tasema maana alinitenganiaha na ndugu na rafiki zangu karibia wote
Pole sana kwa Mitihani ndugu yangu, Ila sasa Ndo Ujifunze ku Balance upendo, Maana Kwa Mwanamke akionyesha hakutaki au Kukudharau basi Jua huyo si Mtu sahihi kwako achana nae fasta
 
Wakuu mmebarikiwà Sana na Mungu WA mbinguni hakuna laana huu yenu.

Wakati NIPO chuo mwaka WA Kwanza nilipata mawasiliano na dada mmoja wa kiha ambaye tulipotezana tukiwa a level alihama shule nilitokea kumpenda. Ila ye alikuwa chuo kingine mkoa mwingine AMBAKO huko alipokuwa ndo kulikuwa nyumbani.
SA wakati WA likizo alikuwa hapendi KWENDA kwao yaani atoke dar aende tabora Kwa madai kwamba mama yake anazingua Sana.


NB: mdada tulishaachana miaka sasa sjui kama Alishaolewa ama vpi Ila mi nilishaoa kitambo kidogo.
Kwa yeyote mwenye nia ya kupata maarifa, mtu haelewani na Mama yake, haelewani na ndugu zake, wewe ni nani wa kuweza kuishi naye?
Wanasema mapenzi ni upofu, nafikiri na ujinga pia. Bora mmeachana, kama hakuwa na matatizo ya akili, basi ana roho mbaya sana.
 
Siyo kumfadhili, mlikuwa kwenye mahusiano.

Inaonekana hamkuwa mkiendana. Ulifanya vizuri kumuacha/kuachana.

Usijisikie hatia juu ya kifo cha mtoto as long as hauhusiki na uwe ulifanya vema sehemu yako kama baba.

Pole sana mkuu, ndiyo ukubwa huo.
 
Mtoto kafariki, wewe na mdada mshaachana kitambo. Story imeisha vizuri.

Ulijipendekeza tu kusaidia jitu ambalo halikuwa tayari kusaidika. Ungefanya la maana sana kama hizo pesa ungelekea yatima na ombaomba.
 
Aiseee kuna watu mna mioyo vimbwanga vyote hivyo na ulikua unavumilia bado aah

Au ndo alikua anakupea vizuri
KuhuSu kunipea vizuri Hana fundi wowote kitandani Ila alikuwa na umbo la kitusi hips na matako hatari umbo kama nyigu Ila Hana maajabu kitandani otherwise mi nilimpenda Tu na nilijitoa kwaajili yake Kwa Hali zote nilikuwa NIPO tayari Mimi nisiwe hata na Mia chuo Ila nimtumie hela yeye.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom