tamu 3
Member
- Dec 11, 2024
- 88
- 216
NILIME MIMI SHAMBANI
1.............
Nilime mimi shambani, jua kali linawaka,
Majasho yanitokeni, mwili wote umechoka,
Kutwa ninalinda nyani, wanasumbua hakika,
Nilime mimi shambani, bei wanapanga wao.
2............
Ng'ombe wa bwana Shabani, wala mazao shambani,
Yanipasa kulindeni, mawio na machweoni,
Wadudu nao jamani, wanasumbua shambani,

3..........
Pembejeo madukani, beiye haishikiki,
Ila mazao sokoni, bei haitamaniki,
Uwapi wewe diwani, mbona kimya hutamuki,

4..........
Mkulima Afrika, yu duni ni masikini,
Yu peke ahangaika, maisha yake ya chini,
Watu wenye mamlaka, katu hawamthamini,

5.......
Ushuru barabarani, mwingi kuliko magari,
Mageti barabarani, wa mazao ya shambani,

6.........
Bado jembe la mkono, mkulima atumia,
Ni vipi mengi mavuno, shambani atachukua,
Kila siku mgongano, hakuna mbele hatua,

7..........
Kumbuka tena kumbuka, nchi pasi mkulima,
Sawa sasa na kichaka, pasi ndege na wanyama,
Na serikali geuka, kumlindamkulima,

8.........
Lini huyu mkulima, atakuja kukomboka,
Lini huyu mkulima, tapewa yake fanaka,
Lini huyu mkulima, atakuja pumzika,

9...........
Barabara mbovu sana, kijijini kutokea,
Wa gari mtasongana, nauli ajisemea,
Wakupakia vijana, hela wanakuchukua,

10.........
Kusafirisha mazao, gharama kwenda sokoni,
Ila kule ni kilio, mazao ukiuzeni,
Wenye pesa na tuvyeo, bei watulalieni,

11........
Ndiyo kisa mkulima, kila siku analia,
Hapewi yake heshima, japo chakula atoa,
Ukisema mkulima, watu wakuhurumia,

12..........
Wizara hiyo kilimo, mkulima ithamini,
Imutoe kwenye shimo, aondoke utumwani,
Kwenye katiba awemo, asiwe mtu wa chini,

Denny Jeremias kitumbika
Mtunzi wa mashairi na ngano za Kiafrika
Mufindi Tanzania 4.4.2025