Uchaguzi 2020 Nilikuwepo kwenye mkutano, sijapenda kuchangishwa fedha kinguvu

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,176
27,224
Leo kama kawaida niliwahi mapema sana kwenye mkutano kusikiliza sera za mgombea wetu.

Mengi ameeleza vizuri sana japo kuna ambayo ameyarudia rudia sana.

Kingine nilichopenda ni muda wa mgombea umekuwa mrefu sana kapata karibu saa nzima tofauti na 2015 kipindi cha Lowassa ambae alikuwa anaongea dakika 3 tu.

Ila katika yote kubwa ni hili la kutaka kuchangishwa fedha kilazima/kinguvu. Mgombea wetu anatuambia "haya toeni hizo simu zenu za mchina, bonyeza *150*00# kisha chagua namba 4 kisha..."

Baadhi tuliokuwa hapo tukajiuliza kajuaje tuna pesa kwenye simu? Kwa kuzuga tukamjibu hakuna network, akasikia.

HATUJAPENDA HII, WEKENI NAMBA AU ACCOUNT KWA MUDA MTU ATAOTAKA KUCHANGA ATAWACHANGIA.
 
Back
Top Bottom