Winner80
Member
- Feb 9, 2021
- 20
- 19
Baada ya kuwa mtoto niliyekataliwa na ndugu zangu wote mjini, sikuwa na kwingine kwa kwenda zaidi ya kuanza kufikiria kutorokea mtaani.
Kila mahali nilipodhani naweza kupata msaada ilishindikana.
Baada ya kila ndugu kunikataa, mara nikaanza kuishi mtaani.
Mara nyingi sana nilikuwa nikishinda ziwani, kwenye mabanda ya sinema na kuzurura mitaa mbalimbali ya mji wa Musoma toka asubuhi hadi jioni.
Wakati wa usiku nilikuwa nashinda nje ya ukumbi wa disko, maarufu kwa jina la Metro Po. Kwa wale wenyeji wa Musoma watakuwa wanaufahamu vizuri ukumbi
huu.
Mana ni ukumbi ambao upo katikati kabisa ya mji wa Musoma, mtaa wa Mkendo karibu kabisa na ukumbi wa sinema wa Nyota ya Jaa.
Dada mmoja aliyejulikana kwa jina la Hidaya alinifanya kama ‘mwajiriwa’ wake pale Metro Po.
Hidaya alikuwa anafanya biashara ya chipsi nje ya ukumbi ule wakati wa usiku. Kwa hiyo, ‘aliniajiri’ mimi kama kibarua wake wa kumsaidia kuuza chips, kuosha vyombo, kumenya viazi pamoja na kupeleka chips kwa wateja wake.
Ilikuwa ni angalau kwangu kwa sababu kwa kufanya kazi kwa huyu dada niliweza hata kupata chakula na pesa kidogo kwa ajili ya kununulia sigara.
Mana baada ya kuanza kuishi mtaani nilijifunza hadi kuvuta sigara kwa sababu kwa namna moja au nyingine niliona inanisaidia kupunguza baridi usiku, msongo wa mawazo na kuniwezesha kustahimili maisha magumu ya mtaani.
Mwaka 1996 wakati Nikiwa katika mihangaiko yangu usiku, ghafla nilipata taarifa za kifo cha baba yangu mzazi kuwa amejiuwa kwa vidonge niliumia sana. Sababu baba pamoja na mapungufu yake, yeye ndiye alikuwa kama nguzo katika familia yetu.
Kwa hiyo kufumba na kufumbua, mama akawa amebaki na mzigo mkubwa sana wa kuibeba familia.
Hali ilikuwa mbaya sana kiuchumi kwa mama, na kila mtu alikuwa akimtazama kama ndiye kichwa cha familia kwa wakati huo.
Majukumu yote ya
kuhakikisha watoto tunaishi vizuri yalimwangukia yeye itaendelea...
Pastor Winner Magere
Ukonga
0659-409447
February 18,2021