sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,032
Kuna kijana wa kiume kama miaka 25 hivi, yuko fiti sio legelege maana namjua huwa anacheza sana mpira uwanja wa mtaa wangu napoishi, tumezoeana kiasi basi asubuhi nilimpa lifti kumpeleka hospitalini.
Hali ilikuwa ni vuta nikuvute kijana alikuwa mbishi kuchomwa sindano, alikuwa anamwambia daktari mara nyingi apewe dawa tu wasimchome😁 ikabidi niingie pale kumshangaa jamaa nikamwambia acha uwoga, yaani na ukakamavu wako uwanjani kumbe unaogopa sindano, basi kinyonge akakubali kuchomwa ila sasa dakatari akaja na sindano kaishika mkono moja anaipiga piga kwa vidole jamaa akaanza ubishi tena 😁.
Ikabidi lugha kali tutumie kwa kumpazia sauti aache utoto ndipo alipotulia, sasa daktari kaaanza kuingiza sindano jamaa akaanza kusononeka kwa kilugha hata sikujua anachomaanisha, machozi yalikuwa yanamlenga nusu alie aisee..
Hivi kweli mtu mzima unaogopaje sindano?