Nilikuwa siamini ila leo nIImeshuhudia. Kumbe hata watu wazima wanaogopa sindano!

dudu jeupe

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
790
1,000
Kuna kijana wa kiume kama miaka 25 hivi, yuko fiti sio legelege maana namjua huwa anacheza sana mpira uwanja wa mtaa wangu napoishi, tumezoeana kiasi basi asubuhi nilimpa lifti kumpeleka hospitalini.

Hali ilikuwa ni vuta nikuvute kijana alikuwa mbishi kuchomwa sindano, alikuwa anamwambia daktari mara nyingi apewe dawa tu wasimchome😁 ikabidi niingie pale kumshangaa jamaa nikamwambia acha uwoga, yaani na ukakamavu wako uwanjani kumbe unaogopa sindano, basi kinyonge akakubali kuchomwa ila sasa dakatari akaja na sindano kaishika mkono moja anaipiga piga kwa vidole jamaa akaanza ubishi tena 😁.

Ikabidi lugha kali tutumie kwa kumpazia sauti aache utoto ndipo alipotulia, sasa daktari kaaanza kuingiza sindano jamaa akaanza kusononeka kwa kilugha hata sikujua anachomaanisha, machozi yalikuwa yanamlenga nusu alie aisee..

Hivi kweli mtu mzima unaogopaje sindano?
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
14,617
2,000
πŸ˜‚πŸ˜‚ mi naogopa lkn jamaa kazidi kipimo huwa nikimuona tu daktari anafingua sindano naanza kumuongelesha ila sio kilugha Kama jamaa.. hiyo huwa nafanya maksudi ili kupunguza uoga..😜
 

Depal

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
15,854
2,000
πŸ™„πŸ™„ Nyie kuchomwa ndo mpk mpigwe mitama..πŸ˜‚
Kuna dogo kwenye hospitali ya jeshi alitimua mbio aliwazungusha hatari ni kilio tu..
Sijawahi ogopa sindano, and sometimes it's better kama kuna opt ya sindano niichague ili niachane na dawa.

Siogopagi ila uwa napata mfadhaiko kidogo tu kama mchomaji ni mwanaume, namuuliza kwahiyo we ndiyo mchomaji? Nurses wa kike wameisha? Akisema ndiyo namuachia tu mzigo πŸ˜†
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
14,617
2,000
Sijawahi ogopa sindano, and sometimes it's better kama kuna opt ya sindano niichague ili niachane na dawa.

Siogopagi ila uwa napata mfadhaiko kidogo tu kama mchomaji ni mwanaume, namuuliza kwahiyo we ndiyo mchomaji? Nurses wa kike wameisha? Akisema ndiyo namuachia tu mzigo πŸ˜†
Mpk nimetamani kuwa daktari ili uniachie tu mzigo..😜

Mi napenda nichomwe sindano na jinsia yatofauti nami sio me mwenzangu😎😎
 

Sivan

JF-Expert Member
Jul 17, 2020
941
1,000
Aisee malanyingi namalizana na mahoma yangu kwa mapanado kwa kuogopa sindano nikiingia vile vyumba vya daktari tu na kuona vichupachupa, vigrass na vipakiti vya visindano moyo unapiga.

Nakumbuka ile wakati wa kujiunga chuo unahitajika ukapime just kisindano cha kidore tu nilifikiria sana mwezi wote nilijiona kama nina deni kichwani.
 

Depal

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
15,854
2,000
Mpk nimetamani kuwa daktari ili uniachie tu mzigo..😜

Mi napenda nichomwe sindano na jinsia yatofauti nami sio me mwenzangu😎😎
Na mlivyo na makalio magumu yasiopakwa mafuta yamepaukaa na kukakamaa πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† ndiyo maana hampendi sindano
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom