Nilikuwa siamini ila leo nIImeshuhudia. Kumbe hata watu wazima wanaogopa sindano!

Tunachoogopa ni ile hofu tu ya kuchomwa sindano lakin kuchomwa kwenyewe wala hakuumizi
 
aisee mimi kazi yangu nacheza sana na sindano ila ni kwa viumbe wafugwao...
Ila ikija suala la mimi kuchomwa sindano hapo tutatafutana, namshukuru sana MUNGU kwa kuniweka salama kiafya na kiakili
Mara ya mwisho kuchomwa sindano ni 2005 na mpaka sasa sijawahi chomwa..
Naogopa sana sindano aisee
 
Kuna kijana wa kiume kama miaka 25 hivi, yuko fiti sio legelege maana namjua huwa anacheza sana mpira uwanja wa mtaa wangu napoishi, tumezoeana kiasi basi asubuhi nilimpa lifti kumpeleka hospitalini.

Hali ilikuwa ni vuta nikuvute kijana alikuwa mbishi kuchomwa sindano, alikuwa anamwambia daktari mara nyingi apewe dawa tu wasimchome ikabidi niingie pale kumshangaa jamaa nikamwambia acha uwoga, yaani na ukakamavu wako uwanjani kumbe unaogopa sindano, basi kinyonge akakubali kuchomwa ila sasa dakatari akaja na sindano kaishika mkono moja anaipiga piga kwa vidole jamaa akaanza ubishi tena .

Ikabidi lugha kali tutumie kwa kumpazia sauti aache utoto ndipo alipotulia, sasa daktari kaaanza kuingiza sindano jamaa akaanza kusononeka kwa kilugha hata sikujua anachomaanisha, machozi yalikuwa yanamlenga nusu alie aisee..

Hivi kweli mtu mzima unaogopaje sindano?
sasa akaanza kusononeka kwa kilugha ndo nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona kawaida tu boss wangu, mimi na umri wangu huu NAOGOPA sana sindano. Siku nachomwa sindano nadhani nitakuwa mahututi.
 
Kwa tetenas hio haipo mkuu,kama una mke,ndugu wa kike(wakati wa ujauzito lazima wachome)au kiume aliyechomwa msumali,katwa panga au kitu chochote cha kutu akaenda choma hio sindano muulize atakwambia
Kutobolewa kwa aina zote lazima ufutwe na spirit kuzuia maambukizi.
 
Katika maisha yangu kati ya dozi ambayo sikuwahi kumaliza siku zote ni dozi ya vidonge hasa hasa vikiwa ni vingi, lakini dozi ya sindano hata zikiwa 100 namaliza na kutoboa kwa raha sana lakini huwa sikubali kabisa kuchomwa sindano ya tako na mhudumu wa kike, hapo hata kwa sururu sikubali
 
Nimewahi kushuhudia binti wa 20+ akipigankelele Kama anabakwa!
Tuliokuwa Ni mtoto wangu wa miaka 5 alishangaa saana!
 
Kuna kijana wa kiume kama miaka 25 hivi, yuko fiti sio legelege maana namjua huwa anacheza sana mpira uwanja wa mtaa wangu napoishi, tumezoeana kiasi basi asubuhi nilimpa lifti kumpeleka hospitalini.

Hali ilikuwa ni vuta nikuvute kijana alikuwa mbishi kuchomwa sindano, alikuwa anamwambia daktari mara nyingi apewe dawa tu wasimchome😁 ikabidi niingie pale kumshangaa jamaa nikamwambia acha uwoga, yaani na ukakamavu wako uwanjani kumbe unaogopa sindano, basi kinyonge akakubali kuchomwa ila sasa dakatari akaja na sindano kaishika mkono moja anaipiga piga kwa vidole jamaa akaanza ubishi tena 😁.

Ikabidi lugha kali tutumie kwa kumpazia sauti aache utoto ndipo alipotulia, sasa daktari kaaanza kuingiza sindano jamaa akaanza kusononeka kwa kilugha hata sikujua anachomaanisha, machozi yalikuwa yanamlenga nusu alie aisee..

Hivi kweli mtu mzima unaogopaje sindano?
NILISOMA NA JAMAA ADVANCE ANACHEZA MPIRA KWA UKAKAMAVU WOTE MA ACROBAGIC FUTI KILO ZOTE KWENDA JUU KUMBE JAMAA CHAKULA.
 
Back
Top Bottom