Nilikuwa siamini ila leo nIImeshuhudia. Kumbe hata watu wazima wanaogopa sindano!

Kuna kijana wa kiume kama miaka 25 hivi, yuko fiti sio legelege maana namjua huwa anacheza sana mpira uwanja wa mtaa wangu napoishi, tumezoeana kiasi basi asubuhi nilimpa lifti kumpeleka hospitalini.

Hali ilikuwa ni vuta nikuvute kijana alikuwa mbishi kuchomwa sindano, alikuwa anamwambia daktari mara nyingi apewe dawa tu wasimchome😁 ikabidi niingie pale kumshangaa jamaa nikamwambia acha uwoga, yaani na ukakamavu wako uwanjani kumbe unaogopa sindano, basi kinyonge akakubali kuchomwa ila sasa dakatari akaja na sindano kaishika mkono moja anaipiga piga kwa vidole jamaa akaanza ubishi tena 😁.

Ikabidi lugha kali tutumie kwa kumpazia sauti aache utoto ndipo alipotulia, sasa daktari kaaanza kuingiza sindano jamaa akaanza kusononeka kwa kilugha hata sikujua anachomaanisha, machozi yalikuwa yanamlenga nusu alie aisee..

Hivi kweli mtu mzima unaogopaje sindano?
Weka picha basi tuone. Au unamsingizia?
 
Ulizia vizuri sindano ya panadu (sijui kama nimeandika jina la hiyo sindano kwa usahihi). Hii sindano huchomwi kama hujala, huchomwi ukiwa umesimama na huwa huchomwa mara mbili, yaana anachoma kalio moja anaweka nusu ya syringe afu hiyo nusu nyingine humalizia kalio la pili. Hii sindano nuksi sana, all in all, nadhani muda umefika kutafuta mbadala wa sindano.
Duh! Ni sindano ya kutibu nini? 😀😀
 
Nimetamani ghafla niwe mchomaji
Sijawahi ogopa sindano, and sometimes it's better kama kuna opt ya sindano niichague ili niachane na dawa.

Siogopagi ila uwa napata mfadhaiko kidogo tu kama mchomaji ni mwanaume, namuuliza kwahiyo we ndiyo mchomaji? Nurses wa kike wameisha? Akisema ndiyo namuachia tu mzigo 😆
 
Mi nilikutana na nes akanitoboa kama Mara 3 hiv anakosea kosea alaf mi nipo gado tu namuangalia machoni had akaanza kutetemeka yeye
Ni dhahiri alijua utamuharibia kibarua kwa cheti chake cha kughushi.
 
Back
Top Bottom