Nilikuwa nina muelekeo fulani upinzani lakini kwa haya nimewadharau kabisa

Bacore

JF-Expert Member
Oct 20, 2017
222
228
Baada ya muda mrefu kuona muelekeo wa CCM haukuwa mzuri japo kuwa kipindi hiki cha awamu ya 5, naona mabadiliko makubwa kidogo nje na hayo mapungufu mengine. Mbowe amechemsha, nimeamua kuwadharau Chadema kwa kukubaliana kirahisi na maamuzi ya mwenyekiti wao, kwa maana hiyo mwenyeketi akisema jambo basi ni sawa, watu hawapewi hata warning letter, watu hawapewi nafasi nyingine ya kujitetea.

Itikadi ya chama, jina la chama, haliendani na uhalisia wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Chama kina prove failure, kwa kutokujua hata maana ya demokrasia, mwenyekiti na watu wake wote hamna kitu.

Ninapata ukakasi kufanya imagination ya endapo mmepata nchi. Msiniambie mtafanya maendeleo zaidi ya haya ya awamu ya 5 au na ninyi ndio walewale waongea maneno mengi kuliko vitendo.

chadema ni chama chenye uchu wa madaraka, chadema wanapokea watu kutoka CCM, waje kuwa viongozi kwa vile wameshindwa kule CCM wanakuja na huku chadema kujaribu baati zao, chadema kimekuwa chama cha kuchezesha baati na sibu dhidi ya viongozi walio shindwa kutoka katika chama cha CCM, Lowasa, sumaye NK. CHADEMA ni one man fight, akishapata anawapiga chini, miaka nenda rudi, mbowe yeye pekee ndiye mwenyekiti wa chama.

Hivi mwenyekiti wa Chadema anachaguliwa au amejichagua, mbona kama dectator hivi? Design kama hataki wengine washike wadhifa, alafu design kama neno lake ni sheria, hapana, ni uhuni huu sasa.

Nipo njiapanda, sio CCM wala Chadema kwa sasa.
 
Nenda kasome angalau QT ujue tofauti ya 'r' na 'l'. Hakuna neno 'dhalau' bali kuna dharau. Huwezi kipanga sentensi na unatumia herufi ndogo throughout.

Michosho tu kwa sababu bando ni lako
Wewe sema tuu, nilekebishe, mambo ya kujizungusha hayawezi kusaidia kitu, wewe nimwalimu wa kiswahili ni sawa tunatofautia kazi mkuu"
 
Utamsaidiaje!
 
...nimeamua kuwadharau Chadema kwa kukubaliana kirahisi na maamuzi ya mwenyekiti wao, kwa maana hiyo mwenyeketi akisema jambo basi ni sawa, watu hawapewi hata warning letter, watu hawapewi nafasi nyingine ya kujitetea.
Mimi binafsi nimekuelewa, ila naomba kidogo tu uniwekee uthibitisho kwamba yale yalikuwa ni maamuzi ya mwenyekiti wao tu, na wala sio ya maamuzi ya mkutano wa chama au walau wabunge, ili na mimi niungane nawe katika kumlaani mwenyekiti
 
Baada ya muda mrefu kuona muelekeo wa CCM haukuwa mzuri japo kuwa kipindi hiki cha awamu ya 5, naona mabadiliko makubwa kidogo nje na hayo mapungufu mengine. Mbowe amechemsha, nimeamua kuwadharau Chadema kwa kukubaliana kirahisi na maamuzi ya mwenyekiti wao, kwa maana hiyo mwenyeketi akisema jambo basi ni sawa, watu hawapewi hata warning letter, watu hawapewi nafasi nyingine ya kujitetea.

Itikadi ya chama, jina la chama, haliendani na uhalisia wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Chama kina prove failure, kwa kutokujua hata maana ya demokrasia, mwenyekiti na watu wake wote hamna kitu.

Ninapata ukakasi kufanya imagination ya endapo mmepata nchi. Msiniambie mtafanya maendeleo zaidi ya haya ya awamu ya 5 au na ninyi ndio walewale waongea maneno mengi kuliko vitendo.

Hivi mwenyekiti wa Chadema anachaguliwa au amejichagua, mbona kama dectator hivi? Design kama hataki wengine washike wadhifa, alafu design kama neno lake ni sheria, hapana, ni uhuni huu sasa.

Nipo njiapanda, sio CCM wala Chadema kwa sasa.
Mwenzako kafukuzwa uanacha kisa matakwa yake ya kutaka kugombea Urais. Huko ndiko kwenye Democracy unaweza enda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona Membe mwenyewe kafukuzwa kwa kutoendana na matakwa ya CCM hilo hukuliona? Kwa taarifa yako vyama kuvianzisha na kuvi maintain ni gharama kubwa sana hivyo haiwezekani wewe uende kinyume na misingi ya chama halafu uachwe kisa Democracy nadhani utakuwa huelewi maana ya democracy otherwise utakuwa unalitumia neno democracy kinyume na maumbile.
 
Wewe sema tuu, nilekebishe, mambo ya kujizungusha hayawezi kusaidia kitu, wewe nimwalimu wa kiswahili ni sawa tunatofautia kazi mkuu"

Kujieleza kwa maandishi ni kipimo tosha cha kujua thinking capacity yako sasa nenda ccm ukampinge m/kitu uone shughuli yake au watete waliotumbuliwa usikie muziki wake ukishakuwa mwanachama wa chama chochote ni lazima kufuata utaratibu wa chama kama hauwezi anzisha chama chako mbona ya bungeni huyasemi ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom