Nilikuwa nimevaa Savco na lakupanda.. !

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,070
Ni story ya zamani Kidogo, story ya kuchomeshwa mahindi na zaidi kuzomewa na watoto wa kijiweni
Wakati huo hata hz simu hazikuwepo hz za mkononi nikakutana na kimwana mmoja akanipa ahadi ya kumtembelea anapoishi
Siku ilipofika nikatinga savco yangu, shati la ujiuji na raba lakupanda ,kwa Wakati huo Nilikuwa nimetokedhea kwelikweli
Nikaingia kwenye ule mtaa bishoo mimi sikusalimia wala nini wale wenyeji kufika mwisho wa mtaa nikamuulizia mwenyeji wangu nikasubirishwa nususaa nzima mpaka alipokuja
Kuja tu akanishika mkono tukaenda kukaa pembeni ya barabara nikajiona kidume kweli huku wanamtaa wakinikodolea mimacho yao
Wakati tukiwa tumekaa pale tunapiga stori mara ikatokea Nissan patrol ikija mpaka tulivyo na kutimua vumbi la kufa mtu

Baada ya vumbi kutulia nikaona mlango wa nyumba umefunguliwa na kimwana akapanda bila kusema lolote, mlango ukafungwa gari ukaondoka kwa fujo na kuachiwa vumbi

Nikasikia vicheko kila kona ,hakika nilitumia nguvu za ziada kuweza kuondoka pale mtaani, wana walikuwa wanacheka na kuzomea mno, sikutaka kujua nini kiliendelea ila tangu Siku ile sikuvaa tena ile savco yangu na la kupanda
Natumai nawe ulishawahi kuumbuka au kuchomeshwa mahindi kama mimi kuwa huru kutupia kisa chako
 
Sitosahau siku moja kuna binti alinipa miadi nimuibukie kwao.

Mtu mzima arround saa moja moja nikajisogeza. Nikafika salama salmini. Tulizoea nikifika kwao narusha jiwe kwenye bati, basi anajua mlume nimeshatia timu.

Kama kawa nikarusha jiwe kama kawaida. Nikajibanza migombani namsubiria mtoto. Kumbe mama alishausoma Mchezo, mi sijui.

Ghafla mama akatoka na sahani yenye machicha ya nazi. Akanisogelea karibu, akanimwagia Usoni.

Nikaondoka taratibu, kichwa kizima kimejaa uchafu.
 
Hahahaaaaa
 
pole sana ila usivunjike moyo kwenye kuwasaka vimwana.
Nalog off
 
mshanajr na Mzee, poleni! lakini sasa mwaona tofauti mnavyokamatia bila nguvu na wala bila ya kumwagiwa vumbi na machicha ya nazi ....
 
Last edited by a moderator:
mshanajr na Mzee, poleni! lakini sasa mwaona tofauti mnavyokamatia bila nguvu na wala bila ya kumwagiwa vumbi na machicha ya nazi ....


Aaaaaahhhh. Vijana wa kizazi hiki nikukamata tu. Unakula vitu.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…